Hivi hiki ndicho Kiingereza cha Profesa Ndalichako?

Yes! lazima waongee! ndiyo kazi yao, kuongea siyo ubaya unaousema wewe, ni bahati kwa muhusika ili ajitambue, akikasirika kwa sababu tu tumesema anapiga mateke bahati

kama hutaki asemwe akakae na nyani wasio sema!
 
Eti kaweka tafsiri ya moja kwamoja kwamba "utakaa ndani" aiseee!! Huyu ndo msomi daaah bongo nehinehi!

Profesa Nguli kabisa Prop Ndalichako, wewe unataka kusema nini..

Mama anapiga kazi balaa, Mama anapiga ung'eng'e balaa mpaka watu wanaona wivu humu. Elimu ya Tanzania imekua kwa kasi toka huyu mama amekapata wizara, Heko Dr JPM kwa kumuona huyu mama na kumpa wizara.
 
Kwahiyo unataka nikubaliane na watu humu kwamba profesa hajui lugha ya kiingereza?

Naomba niseme kitu, huwa kuna vitu siku hizi naamua kujitoa akili ili katika hili ngoja nikwambie kitu fulani..

Kama umesoma toka shule ya sekondari mpaka Chuo kikuu ukapata degree, ukasoma masters degree, ukasoma PHD na mwisho ukawa Profesa.. Huko kote Lugha ya kufundishia ni KiEnglish ambayo wewe huijui kiufasaha, swali, UNAWEZAJE KUUTHIBITISHIA UMMA KAMA WEWE UNAKIJUA IPASAVYO ULICHOSOMEA WAKATI LUGHA ULIYOITUMIA KUSOMEA HUIJUI?, UNAWEZA KUELEWA ULICHOFUNDISHWA WAKATI LUGHA INAYOTUMIKA KUKUFUNDISHIA HUIJUI? Elimu ya juu kwa kiasi kikubwa inahusisha presentation ambazo hufanyika kwa KiEnglish, sasa kama huwezi hiyo Lugha unawezaje kusimama masaa mawili ukatetea projects zako na kuonyesha umahili ili waone kweli unastahili?

Ukitafakari sana utagundua ni kwanini Wataalamu wa kitanzania hawana tija, inawezekana huwa watu wengi tunakalili tu huko mashuleni na kufaulu mitihani lakini tulikuwa hatuelewi vinavyofundishwa..

Tufanye kimoja katika hivi kwa manufaa ya vizazi vyetu..
1. Tuache kabisa kutumia kiingereza kama lugha ya kufundishia, watu wasome kwa kiswahili mpaka vyuo vikuu.
2. Tuamue kutumia Kiingereza kama lugha rasmi kuanzia msingi mpaka vyuo vikuu na mkazo uwekwe.

Tuache janja janja tuliokoe Taifa kwenye suala zima la Elimu ili tuhakikishe tunatoa wataalamu competent na sio wasanii wanaowaza kuwa wanasiasa, Ni elimu pekee itakayookoa taifa hili kama kweli mkazo utawekwa kwa manufaa ya Tanzania na watanzania.
 
communication skills bado ni shida nakumbuka wakati naanza chuo nikiongea english nilikua nachekwa, You've taught me so much more than the subject that you teach. Thanks very much Mr.Bob😘😘😘
 




Very interesting, hivi kama nataka kuanzisha biashara je inawezekana nyinyi "factual scientists" mkachambua na kunipa projection kama biashara yangu italipa??.

Nauliza hivyo ili siku fulani nikutafute.
 
Huna aibu, au una joke?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naamini ule msemo kua wanasayansi hawajui kiingereza....
 
ok mfano mtu achukue phd ya kilimo kwa kutumia lugha ya kiswahili tunategemea hajui kiswahili kabisa mtu ametunga kitabu kwa kiswahili fasaha kikakubalika na maprofesa kwa nondo alizoandika kwa kiswahili cha kuandika makala za kisomi nakufundisha wanafunzi wa masters kwa kiswahili.maana hapa unahamishia kuwa tunaabudu kiingereza
 
Duuuuu, haya bana. Ila nadhani kwenye huu uzi kaupata mrejesho, zile nyodo itabidi akajipange upya.
Hayo ya nyodo atajua mwenyewe nachojua hata akiongea kiswahili huwa naona shida kujieleza ila mie nazungumzia kiujumla tatizo la watu kushindwa kumudu kuongea vizuri kiingereza.
 
Uprofesa wa bongo ni kukaa chuoni miaka mingi kuzidi wengine...sio uelewa au kujua mambo....kwahiyo undergraduate ulie field uko vizuri kuliko hao wakaa chuoni....ndio maana field maprof wanachemka
 
Hapa Waziri wa Elimu, Profesa Ndalichako akitoa maagizo ya kukamatwa Mhandisi Mchina.

View attachment 1315270

Sent using Jamii Forums mobile app
Mbumbumbu hupoteza muda mwingi kuongelea lugha hasa kiingereza lakini hao hao wazungu huwa wanakosea kuongea hiyo lugha yao lakini huwezi ona wanaanzisha thread kuongelea hayo mapungufu. Slavery mentality sijui lini itatutoka vichwani mwetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…