Hivi hiki ndicho Kiingereza cha Profesa Ndalichako?

Hivi hiki ndicho Kiingereza cha Profesa Ndalichako?

Mbona kajitahidi sana kuongea kizungu, tatizo ni mifumo yetu ya elimu ni mibovu, watoto tunapokuwa nyumbani ni kiswahili kwa kwenda mbele, tukifika shuleni (sekondari) ni kiswahili kwenda mbele tukiingia darasani ni Kiswanglish (kiswakinge) kwa kwenda mbereee, sasa ni lini tunaweza kuwa good at English??!🤣
Huyu mbona kasoma Canada, alighafirika tu, hatamie ukiniboa huwa nafoka kisukuma nachanganya na kiitaliano siunajua kazi za barabara zimetuathiri
 
Awamu ya Tano inapiga kazi balaa, mama Prop yuko site anatimiza kauli mbiu ya Hapa kazi tu, soon Tanzania itaanza kutoa misaada kwa mataifa masikini, Mama Profesa Mtaalamu anapiga ung'eng'e balaa mpaka huyo mchina anashangaa shangaa hiyo English ya ndani kabisa pale London na kama hujakaa UK huwezi kuelewa kabisa, HIVI HUYU MAMA NI PROFESA NA NI WAZIRI WA ELIMU..?? haya twendeni tu..

Uchumi unakua kwa 7% watanzania wanafurahia maisha mitaan. machinga, mamantilie hawasumbuliwi tena.. Pato la Mtanzania limekua na linazidi kukua kwa kasi..
 
Huyu mbona kasoma canada, alighafirika tu, hatamie ukiniboa huwa nafoka kisukuma nachanganya na kiitaliano siunajua kazi za barabara zimetuathiri



Mleta mada anadai kiingereza cha huyo professor ni kibovu au sub standard, mimi ndio nasema kwamba licha ya huo ubovu bado kajitahidi ukizingatia misingi yetu ya kitanzania ni mibovu kwenye kiingereza ni tofauti na kenya kwa mfano ambapo na wao kiswahili ni wabovu kwa sababu ya misingi mibovu ya Kiswahili.
 
Huyu ndalichako ana kakiingereza kakavu sana!

Hiyo aina ya Kiingereza anaongea mtoto wa form two anayejifunza sarufi.

If a PhD holder's linguistic competence is equivalent to that of a form two student, then you know how big the problem really is.

Nimekutana na maprofesa na wakufunzi wengi na wazuri mno wenye umahiri mkubwa wa lugha zote mbili humu humu Tanzania.

Hivyo, sidhani kama ni tatizo la "mfumo" wa elimu [entirely].

Huyu mama ni kilaza tu katika personal capacity yake mwenyewe (na ni waziri wa elimu?).



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unajua, nyakati hizi ni za ku'impress' boss.
Iga kama bosi anavyojulikana angefanya. Hapo wewe ni mchapakazi.

Kuna wachahche sana katika baraza hilo wanaofanya kazi wanavyoamini inatakiwa ifanyike bila kuanza kufikiria bosi angefanya nini katika hali inayowakabili.

Niwataje wachache.: Makame Mbarawa, Philip Mpango, na nani tena...

Huyu mama sikujua... Alini-'mpress' sana alipokuwa Baraza la mitihani.
 
Back
Top Bottom