Naomba niseme kitu, huwa kuna vitu siku hizi naamua kujitoa akili ili katika hili ngoja nikwambie kitu fulani..
Kama umesoma toka shule ya sekondari mpaka Chuo kikuu ukapata degree, ukasoma masters degree, ukasoma PHD na mwisho ukawa Profesa.. Huko kote Lugha ya kufundishia ni KiEnglish ambayo wewe huijui kiufasaha, swali, UNAWEZAJE KUUTHIBITISHIA UMMA KAMA WEWE UNAKIJUA IPASAVYO ULICHOSOMEA WAKATI LUGHA ULIYOITUMIA KUSOMEA HUIJUI?, UNAWEZA KUELEWA ULICHOFUNDISHWA WAKATI LUGHA INAYOTUMIKA KUKUFUNDISHIA HUIJUI? Elimu ya juu kwa kiasi kikubwa inahusisha presentation ambazo hufanyika kwa KiEnglish, sasa kama huwezi hiyo Lugha unawezaje kusimama masaa mawili ukatetea projects zako na kuonyesha umahili ili waone kweli unastahili?
Ukitafakari sana utagundua ni kwanini Wataalamu wa kitanzania hawana tija, inawezekana huwa watu wengi tunakalili tu huko mashuleni na kufaulu mitihani lakini tulikuwa hatuelewi vinavyofundishwa..
Tufanye kimoja katika hivi kwa manufaa ya vizazi vyetu..
1. Tuache kabisa kutumia kiingereza kama lugha ya kufundishia, watu wasome kwa kiswahili mpaka vyuo vikuu.
2. Tuamue kutumia Kiingereza kama lugha rasmi kuanzia msingi mpaka vyuo vikuu na mkazo uwekwe.
Tuache janja janja tuliokoe Taifa kwenye suala zima la Elimu ili tuhakikishe tunatoa wataalamu competent na sio wasanii wanaowaza kuwa wanasiasa, Ni elimu pekee itakayookoa taifa hili kama kweli mkazo utawekwa kwa manufaa ya Tanzania na watanzania.