Hivi hili deni ambalo Tanesco wanakata ukinunua Luku, wanakata kwa ajili ya nini?

Hivi hili deni ambalo Tanesco wanakata ukinunua Luku, wanakata kwa ajili ya nini?

GOSSO MZEKEZEKE

Senior Member
Joined
Dec 13, 2013
Posts
180
Reaction score
204
Habari zenu JF
Screenshot_20250203-004644.png

Naomba kuuliza mwenye kuelewa anijuze, nimenunua LUKU mwisho mwa meseji nimeona wameandika DEBT COLLECTED, Hili deni wanalokusanya ni deni Gani?, Kodi ya nyumba au ni Nini?,
 
Habari zenu JFView attachment 3223023

Naomba kuuliza mwenye kuelewa anijuze, nimenunua LUKU mwisho mwa meseji nimeona wameandika DEBT COLLECTED, Hili deni wanalokusanya ni deni Gani?, Kodi ya nyumba au ni Nini?,
Wanakusanya hela za kampeni. SAA hizi mtaona tozo na makato yasiyo na kichwa wala miguu kila sehemu. Kwenye miamala ya simu, miamala ya benki, mafuta, maji, Umeme etc. Polisi nao hawatakuwa nyuma kufanya KAZI za TRA Tanzania huko barabarani.
 
Uhuni wa ccm na mwigulu wao
Hata mimi nimejiuliza sana tu...serikali isiyoona haya kuwaibia wananchi wake!

Cost 6,967.22
VAT 18% 1,254.09
EWURA 1% 69.67
REA 3% 209.02
Debt Collected 1,500.00

TOTAL 10,000.00

Fikiria unalipia LUKU ya 20,000, unapata LUKU ya 6,967.22 ! Asilimia 35% imeliwa!
 
Imebidi niangalie miamala yangu. Mbona LUKU yangu debt collected ni zero kwa Dec na January....? Hiyo ni nini?
 
Imebidi niangalie miamala yangu. Mbona LUKU yangu debt collected ni zero kwa Dec na January....? Hiyo ni nini?
Inakatwa kila mwanzo wa mwezi. Kama wewe hukatwi, labda una ubia na TANESCO! Tarehe 2 December, 2024 nilikatwa deni la 1,500!
 
Mimi pia naomba tu nipewe elimu, hilo deni ni la nini?
  • Kama ni la jengo, jengo gani linaongelewa hapa?
  • Je kama mimi ni mpangaji tu, mwenye jengo pia anakatwa?
  • Na kwa kuanzia tu kwa nini linaitwa deni?
Deni kwa kuwa Tanesco wanakusanya kwa niaba ya halmashauri/TRA.

Kinachochanganya kichwa ni mpangaji kulipa kodi ya nyumba ambayo mmiliki anatakiwa kulipa.

Kama nyumba moja ina luku 4 kila mpangaji atalipa hiyo hela. Ila kama luku moja wapangaji wote watalipa 1500.

Ni kizungumkuti.
 
Back
Top Bottom