Hivi hili jina Mwendazake wanalomuita Magufuli ni official?

Hivi hili jina Mwendazake wanalomuita Magufuli ni official?

Duh!Asalamaleko!Napo sijui...!Maana mwingine ataongezea "Nenda mwana kwenda"![emoji120][emoji23]
Screenshots_2023-04-10-18-17-14.jpg
 
Hili neno linaukakasi kulitumia kwenye kadamnasi ndio maana hakuna kiongozi mkubwa amewahi kulitamka hili hadharani...

Hilo neno lilianza kushika trend kwenye hii nchi,baada ya KIGOGO2014 Alipoanza kulitumia akimkebehi hayati..
Neno hilo siyo la tarehe 17/03/2021.Ni neno la siku nyingi.Ni namna baadhi ya watu wanavyolichukulia,kulitafsiri kivyaovyao na kutoa hitimisho la "ladha" ya neno kimatumizi.
 
Neno hilo siyo la tarehe 17/03/2021.Ni neno la siku nyingi.Ni namna baadhi ya watu wanavyolichukulia,kulitafsiri kivyaovyao na kutoa hitimisho la "ladha" ya neno kimatumizi.
Ni la muda kweli sijakataa lakini limevuma baada ya kigogo kulitumia kama kebehi kwa magufuli...

Hivi kwanini anapoongelewa mkapa hatusemi mwendazake ila kwa magufuli kila mtu anajua kuwa ni mwenda zake...
Ni dharau na kiburi,majivuno,chuki na ushamba uliokithiri wa kigogo ndio umeondoa busara ya hili neno.
 
Kwani uliona watu wamefurahia Mkapa kufa? Lakini kwa Mwendazake ilikuwa burudani mpaka Manji akarudi. Vitendo na tabia za Dikteta Magu ndio maana hili jina limemkaa.
Ila sio majina mazuri pamoja na lile la dikteta uchwara...
Sio ya ki ugwana
 
Walitakiwa wamuite Hayati ila si wajua tena mkuu siku hizi watangazaji wanaokotwa tu mitaani bila kujali wana taaluma hio ama la
Maana halisi ya hayati ni mtu aliye hai na ndiyo maana siku hizi huwa halitumiki (likitumika kimakosa).

Bakita wameondoa neno marehemu kutokana na kuwa na asili ya kiarabu, ndiyo wakaleta hilo mbadala la mwendazake.

Mwendazake siyo la kejeli wala nini lakini limepata umaarufu zaidi kipindi cha JPM.
 
Limekaa kikejeli sio official.. Mbona mkapa hakuitwa hivyo wala Nyerere?

Wauni walimtungia Hilo Jina likawa kama msimu Sasa watu washaanza kuzoea
Sikuwa namwelewa magu ila yule mtangazaji kumuita mwendazake sijapenda
 
Hiyo ni dharau, halafu EARADIO ni media kubwa ila watangazaji wake hawana haiba kabisa.
Kile kidada kina mdomo Sana huwa siwezi sikiliza kile kipindi Ni Leo nimechelewa toka na nililala nikisikiliza hio radio hivo Hadi kipindi Cha Mama Mia kinaanza nilikuwa sijatoka
 
Kwani magu hajaenda zake au mnadhani bado yupo tushawaambia mkazikwe nae hamtaki alafu mnamtetea tetea kizembe
 
Tunahitaji walimu watufundishe kiswahili humu JF!Kwani wakitamka hilo neno "MWENDAZAKE" unapata picha gani?Kwamba:
  • Aliondoka kwa kutoroka bila kuaga?
  • Aliamua aende zake tu bila mpango?
  • Alifukuzwa akajiondokea zake?
  • Alichukia tu akaamua aondoke zake?
NB:Ni neno la kiswahili lenye maana ya marehemu au mtu aliyefariki.Lakini,kama unaona haulipendi,unaweza kutumia lingine lifaalo.
Kwa hio mwendazake inamaanisha marehemu et?
 
Back
Top Bottom