Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
demokrasia, sidhani kama uko sawa! Naamini umechanganyikiwa kwa mapenzi ya huyo Kicheche. aliyokutukana hakuwa amekudharau na hakuwa mstaarabu?Sasa kwa upande wa huyo mpenzi wangu, ananilalamikia kuwa nimefanya kitendo ambacho sio cha kistaarabu na nimemdharau.
Mimi ni mwanaume. Nina mpenzi wangu ambaye bado yupo chuo anasoma. Nimekuwa nikijitahidi kumsaidia mambo mengi sana pale hali yangu ya uchumi inaporuhusu. Hivi majuzi ilitokea huyu binti alipata tatizo la kutaka kuzuiwa kufanya mitihani kwa sababu alikuwa hajamaliza kulipa ada, hivyo akaniomba nimsaidie. Kutokana na majukumu mengi niliyokuwa nayo wakati huo, kiasi cha pesa alichokuwa anahitaji ndicho kilichokuwa nimebaki nacho kwenye akaunti yangu. Nilimweleza hali halisi, lakini yeye akaniambia kuwa nimpatie tu hiyo hiyo kwa sababu anategemea kupewa hela hiyo na mzazi wake wiki inayofuata halafu atairejesha. Kutokana na uzito wa jambo hilo, nilikubali kukausha akaunti yangu nikampatia pesa hiyo. Baada ya kumaliza mitihani, nilimwambia kuwa baba yake akimpatia hiyo pesa, asinirudishie yote bali aigawe, nusu anirudishie na nusu abaki nayo ili imsaidie kwenye matumizi yake binafsi. Cha kusikitisha huyu binti alianza kunirushia maneno ya kashfa kuwa mimi ni mshamba, maskini, limbukeni, kwa sababu eti kuna wanaume wanahonga magari lakini hawadai. Pia alifikia hatua ya kunikatia simu pamoja na ku-block namba yangu.Wana JF hayo maneno yaliniuma sana kwa sababu ni mambo mengi sana nimemsaidia siku za nyuma na sijawahi kumdai anirudishie. Sema tu this time ilitokea hivyo kwa sababu uchumi wangu ulikuwa umebana. Kutokana na jinsi ambavyo nilichukia kwa maneno yake ya kashfa aliyonitolea, niliamua kuwaeleza wazazi wake kuhusu anayoyafanya binti yao. Wazazi walinishukuru sana kwa kuwapa hizo taarifa na walisikitika sana na kuahidi kuchukua hatua ya kumuonya binti yao. Sasa kwa upande wa huyo mpenzi wangu, ananilalamikia kuwa nimefanya kitendo ambacho sio cha kistaarabu na nimemdharau. Wana JF naomba mawazo yenu, je hapo nimekosea kuwaeleza wazazi wake?
Demokrasia
Ni kweli unamakosa, you had NO right to go and tell her parents what transpired between you two. If you were legally bound kweli, Kwani ni mkeo huyo? This is nothing but the case of "Cant stand the heat, dont be in the kitchen" :angry:!!!!! So what if umpempa blah blah blah , na kutoa msaada including zeroing your acc?Kama despite all that anakudharau and shouldnt the obvious action be leaving her!?? Unang'ang'anie mwenyewe while huwezi kummudu kifedha, kiushauri wala tabia halafu you want to play the victim,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,urgh~!!!!!!!!!!!!!?
Wewe utakuwa ni wa aina hiyo hiyo ndio maana umetoa ushauri wa kipuuzi kama huu.