Wickama
JF-Expert Member
- Mar 8, 2009
- 1,466
- 1,196
- Thread starter
- #41
Bulldog yuko sahihi! tunapoongelea likes given hapo tunaangalia response za watu na kwa mtazamo wangu wote wenye likes given kidogo na kwa kuzingatia post zake hapo unapata jibu kwamba huyo mtu ni mchoyo au kinyume chake.
Mkuu, awali ya yote shukran kwa umakini mkubwa katika kuweka mada na mawazo yako. Kilicholeta msukumo wa kuanzisha mada mama ni kuwa nikikuta mtu ana postings 40,000, kisha ana Likes 850 huwa nachukulia kuwa huyu ni wale wanaoandika "ngoja waje...", "nimepotea...", "duh..." nk kifupi ni kuwa uzito wa mchango wake kama mtoa mada across hizo threads ni mdogo sana. Mimi namuona huyu kama mtu ambaye SIO SERIOUS hata kwenye mada nyeti. Namuona kama uwezo wake wa kupekua mambo na kuyaweka ili wengine wanufaike ni mdogo sana. Kifupi huyu ni Kilaza wa kutupa. Kisha napokuta mtu haswa mwenye ku-post mara nyingi na kusifiwa na kusomba Likes za watu across JF in thousands (mfano 19,000 likes) eti yeye ana Likes given 644, huwa naona huyu jamaa ni mbinafsi na hajali watu wengine na yuko pre-occupied na kutaka sifa. Singependa awe jirani yangu. Sitataja IDs lakini tembeleeni pages za vinara wa postings na kusomba likes za watu wakati mwingine kwa kigezo kuwa ni watetezi wa umma au makundi fulani kisha mfanye malinganisho. Wengi sio wenye hata kurudisha hisani kwa kuwatunuku mashabiki wao "likes". Hawa nawahisi kama watu wachoyo wapenda sifa na singependa wawe jirani zangu.
Lakini wapo wachangiaji ukipima Likes walizopewa na walizotoa unakuta ratio ya > 0.8, mfano rahisi ni kama kina Mamndenyi, Mkuu wa chuo, FaizaFoxy, na hata wewe mwenyewe wote wana ratio hadi 1.2 and above. Hawa nawaona kama ni watu kareem sana ambao ningependa sana wawe majirani zangu.
Njemba yoyote yenye ratio < 0.2 kama ni jirani itanifanya nijenge fence mapema (not really hahahahah).
In essence hii ndio spirit ya mada. Dada Mamndenyi, nina ushahidi wa ukarimu wako kwa hiyo huenda kigezo cha Likes Given/Received kipo sahihi.