Hivi hizi taa za kuongozea magari zinazofungwa sasa hapa Dar zimefanyiwa Tathmini au ni Upigaji?

Huna exposure aisee
 
Bado taa za magari na bajaji, dereva bajaji anakuwashia full halafu taa kali kafunga km ya treni unaweza kuhama barabara usipokuwa makini.!! ๐Ÿ˜น๐Ÿ˜น
Wanakera sana asee yani mtu anawasha mataa full kama anawinda, bado honi siku hizi hadi bodaboda wanafunga honi kama za mabasi na malori, ukipigiwa hilo lihoni unashituka unajua kuna mbasi au mlori unakuja nyuma yako kumbe ni kabodaboda yani wanaweza kukusababishia ajali hivi hivi
 
๐Ÿ˜น๐Ÿ˜น๐Ÿ˜น Mwenzio last week bado kidogo nile mbanga, kuna bajaji alinichomekea nusu nipate ajali.!!
Zile honi zao sijui wamefunga za New force yani tafrani km sio mzoefu unaweza kuhama njia ukajikuta korongoni.!!

Sasa siku jaribu kwenda mkoa ukutane na big boyz mabus na milori halafu kuna wale madereva wa IT unaweza kupaki gari upumzike hizo fujo zao ๐Ÿ˜น๐Ÿ˜น๐Ÿ˜น
 
Hahaha yani huko highway madereva wa mabasi na malori Neno kukupisha kwao ni msamiati, wenyewe wanawaita madereva wa magari madogo eti wamama wa nyumbani, unakutana na mtu anaovertake yuko kwenye lane yako sasa uchague moja umpishe au akuvae uingie uvunguni ๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€
 
Hapo kwenye IT unatusingizia kwa kweli
 
Aisee udongo unalamba sana kwa kweli.
 
Jadda inaonekana ww muoga sana.!!
Kuna siku nilikuwa nadrive night kali naenda mkoa, kuna sehemu inaitwa senjere kuna mlima lori lilikuwa mbele yangu.!!
Kila nikiliomba nipite linanigomea linacheza cheza babarabara nzima.!!
Ghafla likaniruhusu ila likawa halina utulivu, sijatulia likaanza kurudi reverse halafu linarudi zigzag weeehh.!! Nikasema hapa tayari dude lishabuma hili bila kutumia akili ya ziada naondoka.!!
Nikaanza kulivizia lilivyoingia kushoto nyingi nikanyoosha goti speed niliyotoka nayo haina kugeuka wala kuangalia pembeni.!!
Ile siku niliandika kwenye diary sikuamini km ningechomoka.!!

Njoo siku tutafute trip hata za chalinze tufanye fujo. Nimemiss vurugu za road trip siku nyingi sijagombana na trafic ๐Ÿ˜น๐Ÿ˜น
 
Hapo kwenye IT unatusingizia kwa kweli
Weeeh!! Tena IT ndio mna visa sijaona aisee.!!
Hapa nimetamani kuongea kwa voice note nikucharule ๐Ÿ˜น๐Ÿ˜น๐Ÿ˜น

Kuna siku nilikuwa nampeleka dogo shule mkoa, nilikuwa mdogo mdogo.!
Mbele si nikaona IT imeniuzia kicheche nilimind, nikapotezea.
Nikaja kukutana naye mbele nikamuovertake si akafanya ligi akanichomekea tena.!!
Nikasema manyoko wewe usintanie gari yenyewe ya boss unaipeleka Congo huko ngoja nikuonyeshe.!! Nikapaki pembeni nikamwambia dogo hamia seat ya nyuma nimuonyeshe kibuyu huyu ananizoea.!!
Nilinyoosha goti na mimi nikamchomekea aliyumba nikaona anapeleka gari kichakani kuchimba dawa ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
Akajitahidi akachomoka akarudi road nikamsubiri mbele akanipita kwa speed na honi za kukubali yaishe nikacheka sanaโ€™a nikaona kajifunza hataki ugomvi huyu.!!

Nilichofanya na mimi nikamuovertake kwa speed nikashusha kioo nikampa middle finger alishangaa kuona ni demu akacheka akanipa salute mi huyo nikamuachia manyoya.!! ๐Ÿ˜น
Tukaja kukutana tena check point waliponisimamisha kwa muda wananiuliza unaenda wapi mbona unaendesha gari km limeibiwa? Halafu ni mdada?
Wakanikagua yule jamaa anacheka, anasema niwaambie ulichokifanya?? Nikamkata jicho la โ€œmwana ukomeโ€ walivyoona niko na mwanafunzi wakaniruhusu.!!
Yule jamaa wa IT akaniita โ€œOyaah road trip Queen nisubiriโ€ nikamsonya nikamwaga moto hatujaonana tena mpk naingia Mbeya.!!
 
Aisee
 
Mbona kama unanitamanisha sasa.
Anyway nishazeeka na nina familia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ