BICHWA KOMWE -
JF-Expert Member
- Jul 21, 2022
- 6,373
- 16,073
Unamkuta mtu anajiita daktari, au nesi, au mwalimu, lakini hana umahiri wa kazi yake. Hajui anachokifanya wala hana hamasa katika kazi yake.
Anasubiri kutafuna mshahara na kuchati WhatsApp huku watu wakimngojea.
Unawezaje ukawa mwalimu na usijue kuandika? Nimepokea barua na ripoti ya matokeo ya mtoto kutoka kwa mkuu wa shule, na barua hiyo imeandikwa "LIPOTI YA MWANAFUNZI WA KIDATO CHA PIRI".
Nimejiuliza maswali mengi, inawezekanaje mtu anayetakiwa kuwatoa watoto ujinga akawa mjinga yeye mwenyewe?
Shule za kusomea ujinga ni kama gurudumu linalozunguka kizazi hadi kizazi. Mjinga mmoja anasambaza ujinga wake kwa mamilioni ya vizazi nyuma yake.
Unafika kwa daktari anakwambia tiba ya kansa ni KUBANIKWA KWENYE MIONZI! Tena anasema kwa kujiamini huku akipiga kizungu kingi cha ugoko, "You know this, i mean, of coz, exactly".
Hivi hizo shule mlienda kusomea ujinga?
Unawezaje ukambanika mtu kwenye tanuru la moto halafu ukamwambia hiyo ni tiba? Who does that?
Kuna haja ya kupitia upya ubora wa kila shule ili kujiridhisha kama yale yanayofundishwa huko ni elimu kweli au ni kapu la ujinga linaloitwa syllabus.
Cc: FaizaFoxy