Hiyo sera iko midomoni mwa viongozi wa Serikali na CCM. Ila, kiuhalisia hakuna kitu kama hicho nchi hii.
Licha ya Serikali kutoa maelezo kuwa Huduma za Afya kwa Wazee zinatolewa Bure kwenye Vituo vya Afya, uhalisia katika utekelezaji wake umekuwa haueleweki na hivyo, kusababisha kero kwa Wazee wanaofika katika baadhi ya Vituo kupata Huduma.
Mamlaka zitoe maelekezo sahihi kuhusu Huduma hizo kwa Wazee ili ziwe Wazi na zisizo na Milolongo kwa lengo la kuepusha vishawishi na mazingira ya Rushwa. Kinyume na hapo, Huduma zitakuwa chini ya Kiwango au kusababisha usumbufu unaoweza kuepukika.