Hivi huku Mbweni wanaishi Watanzania? Haya majengo sio poa

Wa mama wameshavuka daraja linalotenganisha Dar na bagamoyo, maeneo hot sasa hivi ni kusogea mapinga, zinga na kiromo... Bagamoyo port ipo njiani
 
Kiwanja kinauzwa wastani wa bei gani ?
 
Nipo Mdogo wangu...Nilichukua break kidogo humu nimerudi...

Umenikumbusha Kuna sehemu pia Goba huko kunaitwa Goba Maghorofani...Hakuna nyumba ya chini hata moja....nyumba huko ni Maghofa tu.
 
Kiwanja chako kina ukubwa Gani kiongozi?
Kama itakupendeza baada ya kutaja ukubwa wake na utahitaji pesa ngapi, basi tunaweza kuyajenga ukaenda chanika tu mkuu!!

kuna hiki kiwanja hapa kipo... karibia na kitunda, kivule kilomita chache ukiwa unatokea banana.... kina ukubwa wa MITA 25*30 kinahitaji 25m tu...!

urefu wake ni kuanzia hiyo nguzo u nayo iona hadi ile nguzo ya juu kule ya umeme...0759170794​
 
Sehemu kama hiyo ukijenga Kibanda utapewa ujumbe wa nyumba kumi au Mwenyekiti wa serikali ya mtaa maana utaonekana una muda wa kufuatilia mambo ya watu,
Mkuu angalia sana nyumba yako isije kua ya mfano mbaya kwa wageni Yaan wakifika hapo wanaambiwa utaona nyumba ndogo chafu chafu 😂,
Uza hapo njoo Kigamboni ule upepo wa bahari bila bughza
 
Ukiwa na mke pamoja na watoto ni hatari sana kujenga maeneo ya watu waliokuzidi kipato sana.

Lifestyle creep inaweza kukupata kuanzia shule za watoto utalipa $1000/monthly international schools pia kutakuwa na influence mbalimbali za kimaisha ili uendane nao.

Ushauri wangu hapo uza haraka sana huendani nao kama umehoji juu ya uraia wao maana yake umezungukwa na wazito. Nenda kajenge eneo la watu wa kawaida ambao maendeleo yao ya vitu utayaona kawaida. Hapo hutakuwa na lifestyle pressure ya kuendana nao.
 
Ila kweli kuna maeneo mbweni na goba ukipita kuna mijengo ya hatari sanaa ,sijui wenzetu wanapata wapi hizi pesa wakati wengine vinyumba vidogo vinatuendesha sana kuvimaliza
 
Fanya urudi kijijini kwenu
 
Zungusha uzio wawe wanapaki hayo madungu sijui nini
Mkuu sio kila aliejenga hapo ni mwizi hapana kuna watu wako nje wanahangaika usiku na mchana na wanaweka hadi 4m/m ili wajenge hapo

Hiyo dhana ya wote mafisadi sio kweli halafu nashangaa mbongo umesahau uchawi

Amua moja niuzie au waegeshe magari yao
Kujenga watu wengine inawachukua hata miaka 10 ila akimaliza ukaona kwa mara ya kwanza lazima uanze na Ramli zetu ooh jizi kumbe amepambana miaka 10
Wapo mafisadi na majizi ila sio wote maana hata wewe ungeweka malengo ya miaka 15 mbona ungepasua tu
Tatizo lenu mnataka paap paap
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…