Hivi huku ni kujivuna au?

Dejane

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2014
Posts
50,587
Reaction score
71,492
Kuna mkaka kanunua gari used ya kawaida tu lakini kabadilika jamani.

Najiuliza angenunua yale magari mazuri haswa kama Range, BMW, sijui ingekuwaje nahisi angepaa.

Zamani alisalimia kila kila mtu sasa hivi hasalimii anajikweza sijui anaona kamaliza kila kitu. Sasa si angeacha kuwa kusalimia tu toka zamani.

Kwanini ubadilike si watu lazima watakusemaa, zamani alijichanganya na watu sasa hivi sijui anajionaje..

Sitaki kumhukumu aisee huwezi jua yaliyompata. Maana kuna rafiki yangu walikuwa wanaongea sana na kuchangamkiana siku hizi siyaoni hayo kama hamjuii ahahahahah..
 
Huyo kaka yupo humu?

Au ulimuomba lift akakausha? (Kidding)
 
Kuna mmoja alipata kazi jaman wootee waliomsaidia akawaona hawana maana,kuja kusalimia ndugu mpaka awe na nguo mpya,simu au pochi mpya kuja kuwakonga napo hakai sana anaaga na visababu mara ooh nina kikao mahali,mara nafatilia dili la hela sehemu.
 
ukinunua gari ukapita kitaa ukiwapa hi wadau lazima waseme unaringa ukifunga vioo ukapita kimya kimya ndio kama hivi....ila sijajua sisi waswahili tatizo letu ni nini?
Tatizo wakati huna gari ulisalimia na kuwapa hi washkaji umenunua gari lako tena la kawaida tu ndio husalimii kwanini toka zamani usalimiee?
 
Tatizo wakati huna gari ulisalimia na kuwapa hi washkaji umenunua gari lako tena la kawaida tu ndio husalimii kwanini toka zamani usalimiee?
shida iko hivi jamaa angeendelea kusalimia waswahili wangeanza kumsema anaturingishia, na wengine kama mimi tungesema jamaa mshamba wa gari kila akipita anapiga honi na kusimama......dawa ni kupita kimya kimya
 
Tatizo wakati huna gari ulisalimia na kuwapa hi washkaji umenunua gari lako tena la kawaida tu ndio husalimii kwanini toka zamani usalimiee?
Hivi niwaulize; unaweza kuendesha Gari km 6 ukawa unasalimia kila unayeonana naye?
 
Hivi niwaulize; unaweza kuendesha Gari km 6 ukawa unasalimia kila unayeonana naye?
Hiv hujawah ona mtu yupo ndani ya gari akapungia mkono watu,,mbona zamani alisalimiaa angeacha toka zamani ,,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…