Mzee wa kupambania
JF-Expert Member
- Aug 14, 2022
- 21,111
- 53,092
Mwanaume atamuacha baba yake na mama yake naye ataungana na mke sio single mazaOohh kwahiyo kipimo cha ujinga na upumbavu ni kushusha standards zako ili uwe na mtu wa aina fulani kwenye mahusiano, kwamba boss wa kampuni ambaye kaoa single mother ni low value man kuliko kibaka wa mitaani ambaye kaoa mwanamke asiye na mtoto, na kwa mantiki hiyo hata mwanamke ambaye kashusha standards zake ili aolewe na mwanaume fukara na masikini ni low value woman siyo
Kwamba jibu la hilo swali lako ndio lingeamua whether single mother anafaa au hafai, kwani baba yangu ni role model wa wanaume wote duniani kiasi cha kumtolea yeye kama mfano, sidhani kama baba yangu kutomkuta mama yangu akiwa single mother ndio sababu tosha inayodhihirisha kuwa single mothers hawafai kuoa
Sasa unatolea mfano wa hao binadamu wa kwanza kuumbwa ulitaka Hawa atumike na nani haya kwani Adam ndio alikuwa ameshatumika, naye si alikuwa bikira ishu hapa ni kwamba wanaume ndio hamko tayari kujitunza, hata wanawake wote wakisema wajitunze hadi ndoa ninyi mtakosa wa kufanya nao na hamtaweza kuvumilia na kusubiri hadi ndoa
Kwahivyo mtazidi kutafuta mbinu za kuwarubuni ili muendelee kuzini nao na kumbuka wanawake nao ni binadamu siyo malaika, mkishawatumia ukifika wakati mnataka kuoa ndio mnajifanya eti mnatafuta bikira wakati ninyi wenyewe ndio mliozitoa, tunapowaambia kwamba mkitaka bikira basi hakikisheni na ninyi mnakuwa tayari kujitunza muwe mnaelewa sasa
Siyo kila kitu mnaleta ubabe na ubishi wa kipumbavu wakati mwisho wa siku mnaumia wenyewe kwa kukosa aina ya wanawake mnaowataka, kisha wenzenu wakiwaoa mnasema wameshusha standards wala siyo kwamba wameshusha standards, bali wameacha kuishi kwenye fantasies wamekuja kwenye reality yani wameamua kukubaliana na matokeo na uhalisia
Sir God kashamaliza kusema