Hivi, huwa ukiongea peke yako unaongea na nani?

KUNA TIME ROHO MBILI ZINAVUTANA

MWINGINE ANASEMA NENDA MWINGINE ASEMA USIENDE
Fanya hivi kiurahisi, ili ufanikiwe kuzing'amua ipi ndiyo ipi siyo;

1, Fuata ile Roho ya kwanza, iliyo kunong'oneza awali. au

2, Fuata Roho ile tulivu, isiyo kuwa na kiherehere cha kukumbusha mara kwa mara, na kukupa sababu za hapa na pale za unafuu wa jambo lako husika, au kuhusu jambo unalo taka kulifanya Mfano;

Bwana weye unaendesha gari lako toka nyumbani kwako let say Mbezi Beach/ Africana, unaelekea Manispaa ya Temeke Via njia panda Mwenge but imetokea sasa unapambana na Roho mbili tata na za ushawishi kama ifuatavyo;

Roho ya kwanza; inaanzia pale tu ulipo panga safari yako. au tuseme umeamka kitandani kwako, ikakusemesha kuwa ''ukitoka nyumbani endesha gari hadi City centre then to Manispaa ya Temeke via Mwenge junction.,
Haya ndiyo mawazo yako ya kwanza kabisa, tangu unapanga safari yako ya Temake, unaamka, unaoga, unakunywa chai mpaka unawasha gari nk, ni wazo hilo hilo tu moja la kuhusu mwelekeo wa safari yako, but kadri unavoendesha gari, na kukaribia Lugalo jeshini unapata wazo la Roho ya pili kinzani na wazo la ile Roho ya kwanza kama hivi ifuatavyo;,

Roho ya pili sasa; inakushawishi kwa kupitia mpango wako uleule wa kufika Manispaa ya TMK.
Eti ''bwana sasa si katisha hapa tu Ubungo-Buguruni kuelekea Tmk?
Tena hili wazo la pili linakuja kwa mbwembwe na msisitizo zaidi ''si pita Ubungo-Buguruni bana?'' Kwanza si unaona mwenyewe ni njia nyepesi hii, na rahisi halafu hakuna foleni kubwa'',
si unaona Magari yanavo kwenda faster huko, kuliko huku?''

Hapa tayari wewe ni victim wa Roho mbili kinzani, tena itakuwia wepesi sana kufuata wazo la pili, ufanye nini sasa kama mwana JF mbobezi wa Threads?
''Haraka sana bila kuchelewa rejelea wazo la awali,linasema nini, usilifuate wazo hili la roho ya pili utapotea mbaya''

Wewe Komaa tu na lile wazo la Roho ya awali, tangia pale ulipoanza kupanga safari yako tu baas, na ukaamka kitandani, na kuanza safari yako, hata km utakapo fika hapo njia panda- Mwenge na kuona foleni tata ya magari ya kuelekea City centre ni ndefu zaidi ya ile ya Ubungo-Buguruni usibadili mawazo. its much better than kufuata wazo la pili la kupita Ubungo-Buguruni to Temeke ukitokea Mwenge. .

Endapo sasa utaamua ku-violet wazo ya Roho ya kwanza, na kufuata wazo la pili kwa namna yeyote ile lazima hapo kuna baadhi ya majanga utayowezapata. kwa mfano mdogo tu;

Mji-Lori wa mkoa umefunga njia kwa ajari. hasara ni lazima utakaa/kuchelewa

Trafick kukuchelewesha kwa makosa madogomadogo, Au kukamatwa kabisa,-utapoteza muda.

Mara utakaa, nakusikia wanasubili msafara wa Rais Museven upite nk.

Yeyote humu ndani akitaka kuhakikisha haya maneno yangu nayosema , Fuata utaratibu huu mdogo hapa chini kama ifutavyo;
''Jaribu kukinzana na wazo la awali'' maksudi tu uone mabaya yatakayo kupata. then utuletee mrejesho hapa.

USHAURI WANGU;
Nasisitiza kwa wote humu ndani, Mabibi na mabwana mnaopitia uzi huu mwanana!, ni vema, tena mara nyingi kuliko zote kusikiliza na kuheshimu sauti ya Roho ya kwanza inavo kunong'oneza na kukushawishi, au la ni ile fikra tulivu, ambayo imekupitia mara moja tu akilini mwako ukaiona ni nzuri mwanzoni. but ikafifia mahali bila sababu za msingi na ukaipotezea kabisaa!

Ifufue hiyo fikra, na ifanyie kazi uone matokeo yake, kumbuka ''you will never know till you have tried'', na hii fikra chanya, ina tabia fulani hivi za kukatisha tamaa, ambayo naweza kuuita, '' Sneaking Negativism entities (hasi)'', kwa mfano endapo fikra chanya utaamua kuifanyia kazi, sometime, inaweza ambatana na matukio hasi kama haya yafuatayo hapa chini;

1.Unakuwa mvivu mvivu hivi, bila sababu za msingi,mpaka unajiuliza ''why am like this?

2.Nusra unakosa mahitaji muhimu ya kukamilisha jambo nyeti maksudi, mfano unakosa muhuri wa barua ndogo tu ya kukupa go ahead, kwenye mipango yako.

3.Au labda tuseme Forms na makarabrasha ya PassPort yako hayaonekani ndani kwako, wakati unaishi chumba cha peke yako na ni kidogo, at the same time unataka safiri nje ya nchi haraka iwezekanavyo,
hapa naomba niseme kwamba matukio kama haya ni ushawishi wa roho ya pili. ambayo itakupelekea kughahiri mipango yako mizuri kimaisha.

Cha kufanya hapa sasa lazima ung'ang'anie ushawishi wa Roho ya kwanza, rudia tena na tena mpaka kieleweke. na hii yaweza tokea ofisini kwako yamkini hata Boss wako kazini anaweza kukukwamisha kiuonezi hasa mpaka ukalia, bila sababu za maana, zaidi atakukwepa kwepa tu kukupa reasons za maamuzi yake.

Summary;
Ukiona mara tu! ''Roho mbili kinzani'' usipoteze muda, kubabaika na kutafakari kwa kina, fuata ile Roho ya kwanza. kiulainiii!. hata kama ni ngumu kumeza.
 
Summary;
Ukiona mara tu! ''Roho mbili kinzani'' usipoteze muda, kubabaika na kutafakari kwa kina, fuata ile Roho ya kwanza. kiulainiii!. hata kama ni ngumu kumeza. [emoji123][emoji123][emoji123][emoji109]
 
"KUMBUKA HASI INA NGUVU KULIKO CHANYA" now i get the answer!
 
Summary;
Ukiona mara tu! ''Roho mbili kinzani'' usipoteze muda, kubabaika na kutafakari kwa kina, fuata ile Roho ya kwanza. kiulainiii!. hata dwmkama ni ngumu kumeza. [emoji123][emoji123][emoji123][emoji109]
unamaanisha jibu linalokuja la kwanza
 
voice within.... Sauti ndani yako,! Isikilize kwa makini imebeba uhalisia wako..
Imebeba ukweli wako.. Imebeba haiba yako


Jr[emoji769]
 
"bsdhhbddbbdfdfjcdhfbbnsssjssjxxj jdmcjjjfcncshfhhhdh fkffjjsvjjdhuhffdhs"- nilijikuta naongea hivi vipi nifate wazo LA kwanza???
Mshana Jr
 
[emoji44][emoji44][emoji848][emoji848][emoji848][emoji144][emoji144][emoji144][emoji144]
"bsdhhbddbbdfdfjcdhfbbnsssjssjxxj jdmcjjjfcncshfhhhdh fkffjjsvjjdhuhffdhs"- nilijikuta naongea hivi vipi nifate wazo LA kwanza???
Mshana Jr

Jr[emoji769]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…