Hivi, huwa ukiongea peke yako unaongea na nani?

Kwanza lazima nikukumbushe kitu..! Unapoongea pekeyako uwe makini kwakuwa unasikiliza....halafu unajikosokoa halafu unajiuliza na kujijibu ni wazi unaongea na wewe mwenyewe au na wengine kupitia wewe mwenyewe
a2a56dd25eefb7584698bdd41949c9cc.jpg
wewe huko pekeyako uko wanne kwenye jumba moja
1.wewe jina
2.wewe mwili
2.wewe nafsi
4.wewe wewe
Kivipi
1.utambulisho wa jina/Muhuri kiapo cha kutambulika (ID)
2.wewe mwonekano haiba yako sura yako nk nk (AVATAR)
3.wewe nafsi. Uhai na ufahamu(SOUL)
4.Wewe utatu katika moja (me myself and I)
Utambulisho ndio mzizi kisha unakuja umiliki wa vitu na mali na mwili nk, kisha anakuja coordinator wako (ufahamu)halafu unakuja wewe mwenyewe
Kwahiyo unapoongea pekeyako unaongea na wewe mwenyewe
5be5b1dbcb358308879a5a521861d34a.jpg
unaunda maumbo unaunda roho za visasi unafanya mambo machafu au mema unapanga hili na kupangua lile. ..ni wewe mwenyewe huyo uko pekeyako
Matokeo ya dunia tuliyonayo leo hii kwa uzuri ama kwa ubaya kwa huzuni ama kwa furaha kwa kushindwa ama kwa kushinda ni matokeo ya mazungumzo yetu wenyewe kishapo kwenda kwa wengine yakitoka na kupitia kwetu wenyewe
Kumbuka kitu kimoja bila muunganiko wa vitu vitatu hakuna wewe yaani bila utambulisho mwili na roho wewe haupo na hujulikani...tunapozungumzia u mimi hapa ndio penye asili yake
Mwili unapoachana na roho wewe unatoweka na kubaki
1.mwili wako
2.roho yako
3.vitu vyako
4.familia yako
Nk nk
Upo kama wewe wakati mapigo ya moyo yanafanya kazi tofauti na hapo ni habari nyingine
Ni wazi hapo ulipo muda huu umezama kwenye fikra nyingi kuhusu maisha unaongea na wewe mwenyewe unajiumbia hofu na mawazo ya kutisha na kushindwa...unautesa mwili na ufahamu wako bure kwakuwa wewe sio wewe hivyo vitu vikishatengana
Jiulize tena huwa ukiongea pekeyako unaongea na nani?utapata jibu la kushangaza mno
eba2bf1c4f1fef9ac2f7baa0224a954e.gif
Somo zuri sana hili Mr.Mshana,wengi tunashindwa maisha sababu tukiwa peke yetu tunaongea peke yetu mara nyingi roho ya kukata tamaa.
 
Na roho ya kukata tamaa ni sauti hasi iliyo ndani yetu wenyewe. ..unaisikia kabisa inakwambia hicho kitu hutabeba au haiwezekani kabisa kushinda kwenye hilo....tungeweza kuzitengenezea picha hizi sauti ungekuta nyingine zina sura mbaya kweli
 
Ndio maana mara nyingi mimi jambo likiwa linanisumbua huwa nakaa peke yangu halafu nasema NITALIKABILI na kweli nguvu ya maneno yangu haya yamekuwa yananipa ushindi kwenye vita vyangu vingi sana vya kimaisha navyo kumbana navyo.
 
Huku kwetu tunaongeaga wenyewe ili tusiliwe na simba yani njia nzima unaongea ongea tuuuuu hadi ukifika karibu na nyumba ndio unanyamaza.
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Ndio ulimwengu wa ndani ni roho ni nafsi ni ufahamu
Roho ni kama betri
Nafsi ni kama nguvu itokayo kwenye betri
Ufahamu ni kama ile nguvu ya nafsi kusambaa na kufanya kazi husika
Hii package ndio inaunda ulimwengu wa ndani
Je ungependa kufahamu na ulimwengu wa nje?
Ufahamu unapofanya kazi husika mara nyingi huanzia hapo kwenda ulimwengu wa nje
Kama ni simu utampigia mtu au kutuma msg
Kama ni gari litatoka hapo lilipo na kwenda pengine
Kama ni mashine itafanya kazi husika
Na kama ni mawazo utawaambia wengine au utafanya kitendo

Sijui huu uchambuzi umekaa tu ukaandika unachoamini wewe binafsi? Kama unaamini ni kweli ulichokiandika hiyo tunaita hallucinations kuna researches na studies mbalimbali zimefanywa kuhusu mind hadi bwana Watson yeye aliamua kutafiti kwa nini watoto wakiulizwa kitu huwa wanajibu jibu ambalo si sawa? ILA kama umeandika katika mlengo wa dini may be ni sawa.

Well, jiridhishe kwa kugoogle Freud unconscious mind au google different explanations of Schizophrenia. Angalia Biological au family ( biochemistry, season of birth or birth complications, Genetic, Brain structure kama enlargement of ventricles, Behavioural, Cognitive na Freud tena katika Psychodynamics utaelewa unachotaka kuzungumza.

Good luck.
 
Hiki ulichoandika ni kwa mujibu wa vyanzo na tafiti za wengine hiki nilichoandika mimi ni kwa mujibu wangu mwenyewe na utafiti wangu binafsi baada ya kusoma hizo tafiti na mabandiko ya wengine
Vema tusilemazwe na kuamini kitu eti kwasababu tu kaandika mzungu..nina hakika hiki nilichoandika ungekikuta google kimeandikwa na mzungu usingekiita hallucinations. .kwa njia hii kuendelea kutumia vyanzo vya wazungu bado tuna safari ndefu sana ya kusimama wenyewe
 
Kama unaweza angalia hamna study iliyowahi kufanywa na mtu au kikundi kimoja then ikawa na ecological validity!!
 
Mimi nitakuwa wa kwanza nilichoandika kiko very precise na nimejirishisha nacho na kiko wazi na rahisi..kwa kiasi kikubwa ninachojaribu kufanya ni ule utumwa wa kutegemea mabandiko ya kizungu na ndio maana wengi huku ukiandika kitu utaombwa chanzo hata kama muda mwingine chanzo ni wewe mwenyewe
Tumesoma ili tuwe na fikra huru na si fikra za kutegemea na kuamini vya wengine
 
Hahhahahaaaa kajitengenea replica na colabo
Ndugu yangu mshana jr
Ni kwani kuna vitu tunavitamani kwenye ulimwengu wa roho ila hatuwezi kuvipata kwenye ulimwengu wa mwili..
Na baadhi hasa malengo tukiyatimiza bado roho inakataa inshort kwa nini ROHO HAIKINAI NA MAHITAJI YETU...
Hata biblia inakiri hivo...pale yesu alipowaambia wana wake..
"Laiti kama mngalijua yale yaletayo amani lakini yamejificha msiyaone"
Ina maana kaka kuna vitu hata tuvihitaji vip hatutavipata..kwenye ulimwengu wa mwilim.
Nieleweshe kaka..
Bado namaswali mengi yakuku uliza kama hutojali
 
Kwanza lazima nikukumbushe kitu..! Unapoongea pekeyako uwe makini kwakuwa unasikiliza....halafu unajikosokoa halafu unajiuliza na kujijibu ni wazi unaongea na wewe mwenyewe au na wengine kupitia wewe mwenyewe
a2a56dd25eefb7584698bdd41949c9cc.jpg
wewe huko pekeyako uko wanne kwenye jumba moja
1.wewe jina
2.wewe mwili
2.wewe nafsi
4.wewe wewe
Kivipi
1.utambulisho wa jina/Muhuri kiapo cha kutambulika (ID)
2.wewe mwonekano haiba yako sura yako nk nk (AVATAR)
3.wewe nafsi. Uhai na ufahamu(SOUL)
4.Wewe utatu katika moja (me myself and I)
Utambulisho ndio mzizi kisha unakuja umiliki wa vitu na mali na mwili nk, kisha anakuja coordinator wako (ufahamu)halafu unakuja wewe mwenyewe
Kwahiyo unapoongea pekeyako unaongea na wewe mwenyewe
5be5b1dbcb358308879a5a521861d34a.jpg
unaunda maumbo unaunda roho za visasi unafanya mambo machafu au mema unapanga hili na kupangua lile. ..ni wewe mwenyewe huyo uko pekeyako
Matokeo ya dunia tuliyonayo leo hii kwa uzuri ama kwa ubaya kwa huzuni ama kwa furaha kwa kushindwa ama kwa kushinda ni matokeo ya mazungumzo yetu wenyewe kishapo kwenda kwa wengine yakitoka na kupitia kwetu wenyewe
Kumbuka kitu kimoja bila muunganiko wa vitu vitatu hakuna wewe yaani bila utambulisho mwili na roho wewe haupo na hujulikani...tunapozungumzia u mimi hapa ndio penye asili yake
Mwili unapoachana na roho wewe unatoweka na kubaki
1.mwili wako
2.roho yako
3.vitu vyako
4.familia yako
Nk nk
Upo kama wewe wakati mapigo ya moyo yanafanya kazi tofauti na hapo ni habari nyingine
Ni wazi hapo ulipo muda huu umezama kwenye fikra nyingi kuhusu maisha unaongea na wewe mwenyewe unajiumbia hofu na mawazo ya kutisha na kushindwa...unautesa mwili na ufahamu wako bure kwakuwa wewe sio wewe hivyo vitu vikishatengana
Jiulize tena huwa ukiongea pekeyako unaongea na nani?utapata jibu la kushangaza mno
eba2bf1c4f1fef9ac2f7baa0224a954e.gif
Mshana nakushauri utunge kitabu hii elimu itakua msaada Kwa wasioingia huku pia
 
Ndugu yangu mshana jr
Ni kwani kuna vitu tunavitamani kwenye ulimwengu wa roho ila hatuwezi kuvipata kwenye ulimwengu wa mwili..
Na baadhi hasa malengo tukiyatimiza bado roho inakataa inshort kwa nini ROHO HAIKINAI NA MAHITAJI YETU...
Hata biblia inakiri hivo...pale yesu alipowaambia wana wake..
"Laiti kama mngalijua yale yaletayo amani lakini yamejificha msiyaone"
Ina maana kaka kuna vitu hata tuvihitaji vip hatutavipata..kwenye ulimwengu wa mwilim.
Nieleweshe kaka..
Bado namaswali mengi yakuku uliza kama hutojali
Ngoja nikitulia nikujibu kwa kina jioni tafadhali
 
Back
Top Bottom