Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Bora kunguni sio chawa,chawa wana kupa kiminyo kaa umelalia miba vile uwezi ukalala kwanza utakimbia kitanda,ila kunguni wananyonya damu kimyakimya.
Mkuu mimi ni mwamba wa hao wadudu nimedumu nao kwakweli chawa ni msumbufu sana anadunga ipasavyo kunguni sio kivile.Eti kimya kimya hivi unajua kunguni wewe..
Mi kipindi nachimba madini kule mererani tulilala geto moja kwa mshikaji maana kule mmoja akipanga tunalala hata 20 chai na chakula utajua mwenyewe kuoga ni mtoniiii unafua nguo unaanika unaoga huku unasubiri nguo zikauke ndo uzivae tena kule geto ***** kunguni ni kama wote yaani ung'ataji wao ni kama mtu akutoboe na sindano ile ya kushonea magunia [emoji2][emoji2]
Mkuu mimi ni mwamba wa hao wadudu nimedumu nao kwakweli chawa ni msumbufu sana anadunga ipasavyo kunguni sio kivile.
Niliwahi kuchanganya omo na maji nikapita kwa watu naangamiza kunguni...tangu nipite hawajarudi tena.Utamaliza kiwanda but hawajawahi kufwaaa!!
Nilitumia omo wakaishaSoma hii....[emoji115][emoji115][emoji115][emoji115]changanya na mafuta na chumvi wasipoisha ila hata rungu inawaua pia
chumba chote unamwagia maji moto na unapulizia rungu kama yoteemazaria hubaki kwa kitanda&ktk nyufa za kuta!
kama mimi mkuu kipindi niko boarding chawa walinitesa nachemsha nguo na kufua daily ila washkaj wachafu wananiambukiza!Nakumbuka wakati nipo secondary bwenini kwa wavulana kulikuwa na balaa la chawa huku wasichana ni kunguni....sijawah ku experience hawa viumbe wengine[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] ila sekeseke la chawa nalijua vilivyo...hebu waliokumbwa na adhma zote mbili watupe uzoefu...Maana chawa yuko na wewe 24/7 asubiri ulale yeye anagawa dozi muda wote...kauli mbiu yake ni Kama ya #Chadema "ULIPO TUPO"...KUNGUNI VS CHAWA...Nani zaidi[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Wanaume wa dar nyie!Nilienda kupiga mishemishe kijiji flani huko Kondoa ndani ndani sana, mwenyeji wangu wakaniabdalua chumba na kwa kukiangalia kilikuwa poa kabisa kisafi vizuri tuu. Nikashusha zangu net nikalala kuja kushtuka baadae usiku naona kama shingo na mgongo unawasha hivi nikatulia mara naona kama nachomwa sindano sehemu tofauti za mwili nikaona isiwe shida ngoja niwashe taa nicheki ile kuwasha naona wadudu kama 50 na kidogo kitandani wamesambaa kila mahali nilishtuka hatari wakaanza kujificha sababu ya mwanga wa taa. Hiyo ndio ilikuwa mara yangu ya kwanza kuona kunguni, ilikuwa saa 8 usiku ila sikulala mpaka asubuhi nikaaga mapema nduki nikaona isiwe tabu kabisa mambo gani haya ya kulala nusu nusu.
😂😂😂 Hapana Mkuu hao wadudu sio wazuri kabisa ndani ya masaa machache weshanivimbisha namna ile nikawafikiria wanaolala humo mwaka mzima masika kiangazi mbona wana tabu kwa kweli.Wanaume wa dar nyie!
Nilitumia omo wakaisha
wanasubiri ukiwahi mbele za watu ndio wanaanza kukuarest[emoji23][emoji23]kama mimi mkuu kipindi niko boarding chawa walinitesa nachemsha nguo na kufua daily ila washkaj wachafu wananiambukiza!
ila kunguni sijawahi ona, chawa nawajua vizuri wanakaa kwenye mapindo ya nguo hususani boksa na mayai yao ni meupe na yanagandia nguo
haloo hawa wadudu wanamajina mengi mtaani tulikuwa tunawaita vocha au gofu.[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]
Hawa jamaa tulikua tunawaita difenda
[emoji30] [emoji30] , hapo kuambukiza Kwa kiasi kidogo hatari hii,Niliwahi skia wanaambukiza ukimwi ktk kiwango kidogo sanaa...sio uchafu kunguni ni wadadu tu Mimi mwenyewe nilizani ni uchafu lakini niliwakuta sehemu jamani mpk nilishangaa nyumba nzuri balaa....
Mara nyingine lakini mrundikano wa vitu, haswaa maeneno ya uswazi ndo wamejaa kibao!!!