Nakumbuka mwaka Juzi alikuja kijana mmoja toka mkoa akafikia kwangu, kiukweli kunguni sikuwa nawajua ,basi nilikaa na kijana siku mbili then aliondoka kwenda alipotakiwa kufika. Basi baada ya wiki moja hv nimelala usiku nikahisi mdudu ananitembea mguuni nikastuka ,nikaona anakimbia ,nikapuuzia nikajua kamdudu ka mungu katakuwa kamejisahau tu kamekatiza kakanipandia mguuni, basi mwezi ukakata, siku moja juma mosi nafanya usafi nikatoa kava la godoro ili nibadilishe bwana eeeh kwenye angle ya kitanda nakuta vidudu vingiii af vinaona aibu vinajificha ,nikamwita mshkaji wangu nkamuuliza hawa ndio wadudu wanaokula mbao za kitanda?? Akaniambia wewe boya hawa kunguni dah nilijisikia vibaya sana nikamwqmbia sasa wameingiaje na humu hamna uchafu, akasema hata mtu akija kwako kambeba mmoja atazaliana mara elfu asee. Nilirudisha godoro nikaenda job ,sasa usiku nimelala nasikia kitu kinatembea tumboni kuwasha taa wale wajomba asee sinkamuuwa, hiyo harufu nilisikia kutapika. Niliomdoka nkawa sikai ili nikae hata mwenzi nje na nyumbani ilia wakufe ,duh kurudi hamna kitu wapo mpka wametengeneza na base kwenye kona za vitanda, siku moja nikasiki jamaa anapita dawa ya mende, viroboto ,kunguni na wadudu watambaaao, nikamwita jamaa akanipa dawa ya maji akaniambia weka na maji lita kumi na pia tafuta spray .nikatoa kila kitu ndani nikabakiza kitanda tu chumba kizima sasa wamejificha kila kona ya chochoro ya kitanda yani nilipuliza ile dawa mpka kukajaaa maji chumbani yani ukiwaangalia hapo chini kama sisismizi walivyo kufa, basi nkapuliza na godoro siku hyo hyo nilinunua kitanda kipya na godoro. Nikasema sasa hv akija mgeni naenda mlaza gest nimeteseka sana na hao wadudu, maana mpka ikawa ukikaa kwenye daladala na begi lako kama uliliweka kitandani wanadandi ,ukikaa kwenye daladala na mrembo umekumbatia begi yeye ndio anatoka unamwona anakatiza mpka unasikia aibu, au kwenye shati dah watu wanakuona umependeza ila una kunguni .wanakera sana hao wadudu.