Hivi huwaga kuna biashara gani inafanyika pale?

Foffana

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2022
Posts
3,240
Reaction score
5,625
Habari za jioni Wakuu

Kwa wale ambao wapo Dar ama wanapafahamu vyema Dar, basi sio wageni na kitu hiki kabisa lazima watakuwa washawahi kuona ama kusikia

Kuna baadhi ya sehemu ukipita hasa maeneo ya mjini au sokoni huwa unaona kuna kundi limejikusanya wakimzunguka mtu anayetangaza vitu fulani hivi.

Sehemu hiyo inakuwa imetawaliwa na mziki mnene ukipiga kwa sauti na ukichungulia kwa mbali unakuta mbele pale wameweka maTv, subwoofers etc pamoja na vibao kuonesha thamani zao

Kingine ukiwa unapita maeneo hayo kuna watu kazi yao ni kukuita na wewe ujumuike nao tena ukipit karibu sana wanakushika hata mkono na wewe uungane nao

Nimeanza kuwaona kitambo sana tangu napiga kitabu pale Karia KOO wapo maeneo ya Karume TFF sanasana ukiwa unapita tu pale utawaona wapo barabarani kabisa,zamani nilikuwa nawaona sana Manzese pale Bakhresa

Hivi ni nini pale kinachoendelea kwa anayefahamu
 
Matapeli hao, usije kujichanganya wala kukubali kumsikiliza hata mmoja wao pale.

Huwa wanadanganya kuwa wapo kwa ajili ya kupromote bidhaa fulani ambayo inatarajiwa kutolewa labda na tajiri fulani kama Mo dewij n.k, kinachofanyika watakwambia kwamba kuna tiketi wanauza pale, ukibahatika utajishindia zawadi ambazo wanakuwa nazo pale, tiketi moja 5000 wanauza , kwahiyo kama utashiriki, kuna uwezekano tiketi utakayo nunua utajishindia labda TV, redio au pesa taslimu.

Ukishanunua tiketi usitegemee kushinda kwa sababu wanachokifanya wao ni kuhakikisha haushindi, ili uzidi kununua tiketi zaidi ukiamini round ijayo utashinda labda, na ukiona upo na wenzako labda mmoja au wawili wakashinda, wale ni watu wao ambao mwisho wa mchezo huwa wanarudisha vile vitu kama kawaida.

Wajinga wengi sana wanalizwa pale, mtu anaondoka hana hata nauli ya kurudia kwake, kuna siku nilimsaidia nauli kijana fulani ndo akanielekeza kinachofanyika pale.
 
Mnazi mmoko napo wapo
 
Umeielezea vizuri sana hapa umetutoa tongotongo

Wale wanaoshika watu mikono ipo siku nitamzaba mtu ngumi ya Jicho

Kuna mama mmoja nlimsikia akimuomba mtu aliyekuwa anaongea naye kwenye simu kuwa amuongezee hela akaendelee kucheza basi itakuwa walimwambia kuwa bahati yake ya kushinda iko karibu
 
Back
Top Bottom