Kuna siku nilimsikia kuna mama alikuwa anaongea na simu hatua chache kidogo kutoka katika eneo husika akiomba atumiwe hela ili apeleke pale ili ajipatie nini sijui daah, itakuwa tayari alishapigwaPale ni kamali
Usije kujaribu kwenda
Na serikali inawaangalia tu sasa sijui nao wana leseni from Gambling board?Utapeli tu
Anha wa pale Kijazi Interchange upande wa kulia ukiwa unatokea mataa kuelekea Riverside siku hizi siwaoni kabisaYaani unapita zako mtu asiekujua anakushika mkono anasema njoo hapa ushinde TV.
Matapeli hao. Wapo wengine wa karata Ubungo unavoelekea Riverside kutoka Mataa.
Mnazi mmoko napo wapoHabari za jioni Wakuu
Kwa wale ambao wapo Dar ama wanapafahamu vyema Dar, basi sio wageni na kitu hiki kabisa lazima watakuwa washawahi kuona ama kusikia
Kuna baadhi ya sehemu ukipita hasa maeneo ya mjini au sokoni huwa unaona kuna kundi limejikusanya wakimzunguka mtu anayetangaza vitu fulani hivi.
Sehemu hiyo inakuwa imetawaliwa na mziki mnene ukipiga kwa sauti na ukichungulia kwa mbali unakuta mbele pale wameweka maTv, subwoofers etc pamoja na vibao kuonesha thamani zao
Kingine ukiwa unapita maeneo hayo kuna watu kazi yao ni kukuita na wewe ujumuike nao tena ukipit karibu sana wanakushika hata mkono na wewe uungane nao
Nimeanza kuwaona kitambo sana tangu napiga kitabu pale Karia KOO wapo maeneo ya Karume TFF sanasana ukiwa unapita tu pale utawaona wapo barabarani kabisa,zamani nilikuwa nawaona sana Manzese pale Bakhresa
Hivi ni nini pale kinachoendelea kwa anayefahamu
Umeielezea vizuri sana hapa umetutoa tongotongoMatapeli hao, usije kujichanganya wala kukubali kumsikiliza hata mmoja wao pale.
Huwa wanadanganya kuwa wapo kwa ajili ya kupromote bidhaa fulani ambayo inatarajiwa kutolewa labda na tajiri fulani kama Mo dewij n.k, kinachofanyika watakwambia kwamba kuna tiketi wanauza pale, ukibahatika utajishindia zawadi ambazo wanakuwa nazo pale, tiketi moja 5000 wanauza , kwahiyo kama utashiriki, kuna uwezekano tiketi utakayo nunua utajishindia labda TV, redio au pesa taslimu.
Ukishanunua tiketi usitegemee kushinda kwa sababu wanachokifanya wao ni kuhakikisha haushindi, ili uzidi kununua tiketi zaidi ukiamini round ijayo utashinda labda, na ukiona upo na wenzako labda mmoja au wawili wakashinda, wale ni watu wao ambao mwisho wa mchezo huwa wanarudisha vile vitu kama kawaida.
Wajinga wengi sana wanalizwa pale, mtu anaondoka hana hata nauli ya kurudia kwake, kuna siku nilimsaidia nauli kijana fulani ndo akanielekeza kinachofanyika pale.