Hivi huwaga kuna biashara gani inafanyika pale?

Foffana, umeuliza swali la msingi sana na ni vizuri sana umelileta hapa! Ni kweli kabisa kama ulivyosema wewe na Mad Max, hao ni matapeli tu.

Kazi yao kubwa ni kuwarubuni watu ili watoe pesa zao kwa ahadi za kushinda zawadi kubwa kama TV au simu, lakini mwisho wa siku unajikuta umepoteza chako bila kupata chochote cha maana. Wanatumia muziki na makelele mengi kuvutia umati na kuwafanya watu wasifikiri vizuri.

Onyo lako la kutokujichanganya nao ni la muhimu sana na linapaswa kuzingatiwa na kila mmoja. Ni rahisi sana kuangukia kwenye mtego wao kama hauko makini.

Asante sana kwa kulileta hili Foffana, umesaidia wengi kujua ukweli na kuepuka hasara!
 
Mkuu umetoka matombo leo nini? Maana hata maandishi yako yanajieleza unajuakinachoendelea.

Kesho nenda hiyo mitaa na wewe kajumuike halafu utakuja kutupa ushuhuda.
 
Dogo, hao wanatimiza tu masharti ya mganga.
 
Matapeli, pita nao mbali.
 
Hili la kutumia mziki na makelele kuwafanya watu wasifikiri vizuri hapa umenisanua aisee sikuwaza hili kabisa
 
πŸ˜‚πŸ˜‚

Hiyo michezo ukifika chakwaza waambie wewe ni bingwa wa hiyo michezo. Na juzi tuu ulishinda TV smart 43'. Alafu mtazame huyo jamaa usoniπŸ˜„ usikilizie matusi
 
Sasa kiongozi ilitakiwa upitie uangalie harafu uje utasanue sisi ambao hatujawahi waona hao watu.
 
Polisi hupita kuchukua posho kwani wanajua kinachoendelea pale
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…