Hivi huwezi piga rangi gari bila kupiga puti?

Hivi huwezi piga rangi gari bila kupiga puti?

Rangi za magari zina namba....kwa mfano gari yangu ni grey na namba yake ya rangi ni K21 G.

Hizi namba huwa wanaziandika pale kwenye mlango wa dereva. Wasipoweka pale basi wataziandika under hood wanapobandikaga kibandiko flan hivi cha aluminium kinaonyesha details muhimu za gari..

Kwa hiyo ukishachukua namba ya rangi, aina ya gari na mwaka iliyotengenezwa ukaenda kwenye maduka yanayieleweka, unapata rangi saafi kama iliyotoka na gari.

Garage za wahuni huwa wanafananisha rangi kwa macho
wanachanganya na kijiti...pearl white inachukuliwa nyeupe inadondoshewa matone ya njano mpaka inaenda kwenye u pearl 😂😂😂 white
 
Kwaio mkuu unaweza kwenda na hio color code kwa mchina na akakutolea hivyo hivyo au? Maana mwaka 2013 jamaa aliiangalia gari rangi yake kuja kuchanganya rangi ikawa tofauti kidogo na ya sehemu zingine...kuna sehemu huku dar wachina wanachanganya rangi..
Hio gari rangi yake iliwahi badilishwa mkuu
 
Gari ikiwa inatengenezwa kiwandani, ikija kwenye habari ya Rangi huitaji ku apply puti, Wana apply Primer then Painting....!
 
Ukitaka ifanywe hivo bei yake bora ununue gari mpya unaezajikuta inalamba 5 mil
Hakunaga bei ya hivyo labda kama unafufua gari iliyooza kila kitu. Rangi nzuri kabisa imenyooka kwa mchina haizidi milioni 1.5
 
Wakuu salam,
Naomba kujua kama kuna yeyote mwenye mawasiliano (jina la Kampuni) za wahao wachina au wahindi wanaotengeneza rangi kwa kutumia Color Code ya Gari yako.

Ahsante
 
Back
Top Bottom