Hivi huyu dada Joyce Kiria ana shida gani?

Hivi huyu dada Joyce Kiria ana shida gani?

Kuweni makini na maamuzi yenu kabla ya kuoa....huyo dhahiri ni aina ya mwanamke ambaye hastahili kuwa mke wa mtu.

Kwa tabia hiyo anaweza kuanika kila kitu hata kama ulikuwa na jibu m....kund.....uni.
Kuna uwezekano kabisa jamaa kamkimbia na kukata mawasiliano na ndio dada kaona njia ya kumpata ni insta..tusimlaumu anapitia pagumu
 
ukikosea kujenga si utabomoa mkuu ivo ivo ukikosea kuoa utaacha tuu-kamanda aje tu muazimie talaka kwa masheh wa bakwata aachane na mzigo huu wa misumari ya kutu
Kubomoa nyumba na ''kubomoa ndoa'' ni vitu viwili tofauti. Kama mna watoto na unawapenda ndipo ugumu unapokuja. Mbaya zaidi nu kuwa mwenza mmoja eg mwanamke anaweza kuwa ni mapepe na wewe bwana unaona kabisa hata tukiachana watoto wangu watakulia kwenye mazingira mabaya. Hapo ndiyo shida huanza. Ila kama hamjazaa ni rahisi kuachana.
 
Dada yangu joyce hujachelewa nenda kamuone bashite private mueleze kilakitu kuhusu kileo naamini atakusaidia juzi siumeona wanaume walivyokimbilia kwa mkuu wa mkoa kuitikia wito maana mwanzo waliukaidi .Hakuna kinacho shindikana kwa yule jamaa.
 
Swali moja kwa joyce.kungekua hamna insta wala fcbk angetuandikia barua tanzania nzima? Tutumie vizuri maendeleo ya kiteknolojia
 
Wanaume MNA roho mbaya sana, hivi hakuna hata mmoja humu anayevutiwa na supawomani akamliwaze? Hebu acheni hizo
 
Hawa wanawake wengine ni shida, ya ndani analeta hapa mtandaoni kweli dah. somenihapo chini (instagram)

View attachment 688048

  • joycekiriasuperwoman
    Kilewo baba Watoto wangu, yaliyotokea ilibidi yatokee ili kila Mmoja aanze upya safari ya Maisha Yake. Wakati tunaanza huu mwaka nilikuambia huenda mwaka huu tukaachana! Unakumbuka? Well, Lakini jambo moja nakusisitiza hapa, Nimekuomba sana uniachie biashara zangu nisimamie, ili na wewe usinamie biashara zako kutokana na Changamoto zetu hasa za kiuchumi. Wewe Pesa zako unazopata kwenye biashara zako hutaki kushea, Ila Pesa zinazotoka kwenye biashara zangu unataka tushee. Najua ni ujinga wangu wa kukupenda sana ndo umeniponza. Labda ningetenganisha Mapenzi na biashara tusingeishia huku.

    Wakati mimi nasajili Kampuni Yangu nilikuweka kwenye kampuni bila shida yoyote na wakati nafungua akaunti za bank nilikuweka pia. umekuwa ukijua kila ela inayoingia pamoja na matumizi yote kwa sababu lazima tusaini Wote na ndiyo Raha ya Mapenzi.

    Wewe ulipofungua Kampuni yako uliweka pia jina langu kitu ambacho nilipenda sana, lakini ulipokwenda kufungua akaunti ya bank HUKUNIWEKA. Kiukweli SIKUPENDA, mbaya zaidi ukataka kuwa unasaini Pesa zako kivyako.

    Japo nilianza kuona mashaka Lakini nilijipa Moyo, labda ukipata utanishirikisha pia kama Mimi nilivyoamua kukushirikisha kila kitu changu. PESA MWANAHARAMU buana, pale tuu ulipoanza kazi na kampuni yako Ndipo SHIIIDA ilipoanzia, hukutaka kushea hata senti Nyumbani wakati biashara zangu kwa Kipindi chote cha Miaka NANE zimeendesha familia yetu bila tatizo.
    Kuna Miradi mbalimbali ambayo ulikuwa ukionyesha NIA ya kuifanya lakini yote ilifeli. Hivyo haikuwa rahisi KUKUJUA kwa upande wa KIUCHUMI sura yako ikoje... Ulijaribu biashara hizo kwa mtaji wa Familia bila kuona matokeo chanya, Pesa zikawa hazirudi lakini tukajipa Moyo biashara ndivyo zilivyo. Mwisho nikakushauri mtaji wa biashara tukope Bank labda utakuwa na nidhamu zaidi ya Pesa ya Mkopo kuliko kutoa ela Nyumbani. Hukupenda huo Ushauri, ukaona nakubania.

    Sasa MWAKA huu 2018 tuliongea mengi pale Bahari beach, juu ya mahusiano Yetu na Changamoto zake! Pamoja na yote tuliyoongea nikakuomba kila mtu asimamie biashara zake, kisha tukubaliane kwenye MAJUKUMU ya Familia kwamba nani atafanya Kipi. Lakini pia nikakuambia kwamba Niko radhi kuendelea kutimiza hayo majukumu. [HASHTAG]#SIR[/HASHTAG]
Nilifikia uamuzi huo baada ya kuona unaficha PESA zako. Ile Siku niliyokubamba unatoa Ela kwenye akauti yako kwa Siri na hapo tulikuwa hatuna ela kabisa NILIUMIA kuliko hata ningekufumania. Yaani nilikuona huna NIA na Mimi, HUNIPENDI, HUNIJALI. Najua Kazi ulizofanya hata kama NI Ndogo hukukosa hata mkate au sukari ya kuleta Nyumbani. Lakini ukaamua kula bata, hutoki na Mimi, Mara nyingi ukiwa na ela unatoka peke yako unarudi mpaka asubuhi... ukijua kuna punda wako hapa nyumbani atafanya kila kitu.

Kilewo najua Haya siyo mageni kwako, tumeyaongea kwa muda mrefu sana. Tumewashirikisha watu wa karibu. Pamoja na hayo yote Kilichonishangaza sasa ni wewe kukataa kuniachia biashara zangu wakati wewe una za kwako. Tena unasaini akaunti yako peke yako halafu akaunti Yangu nimekuweka tunasaini Wote.

Kilewo kwa staili hiyo ya maisha nilianza kukosa Furaha sana na wewe kwa kuona unanitumia wala huna NIA Njema na Mimi, HUNIPENDI, HUNIJALI, huku Ndani MAPENZI YAKAPOTEA KABISA. Mpaka juzi birthday yako sikuwa najiskia kukuwish. Lakini kwa ajili ya Watoto nikajilazimisha. Ngoja niishie hapa.

KILEWO baba Watoto wangu, Dunia inajua NINAVYOKUPENDA. Tatizo langu kubwa na wewe unajua fika siyo wewe kutokuwa na Pesa, BALI KUTUSHIRIKISHA KWA KIDOGO UNACHOPATA wewe kama BABA wa Familia. kwa Sasa nina tatizo kubwa na wewe la kunipiga baada ya kuamua 2018 nitakuwa natoka peke yangu kujipa raha. Unajua sehemu ninazokuwaga nikiwa nimetoka na ndo sababu ulikuja ukanikuta, lakini uliamua kunipiga. Kesi ipo Dawati.

Kilewo ningekuwa na NIA mbaya nisingekuweka kwenye biashara Yangu, nimenunua Viwanja Goba na Bagamoyo, bila uwepo wako, lakini nilikuja kukushirikisha na wewe ukaenda kuongeza majina yako. Sikuwahi kulalamika maana NAKUPENDA na wewe ndo Baba Watoto wangu. Nimetamani kuzaa mtoto wa Tatu lakini kwa ambushi zako nimeogopa. Mambo ya KOMAA KAMANDA hapana. Nikasema Wawili wanatosha.

Kilewo wangu nakuomba tena na tena uniachie biashara zangu niweze kuendelea kutunza hawa Watoto wetu. Toka unipige umeondoka siwezi kutoa ela, hatuna Chakula nyumbani, Madeni ya wafanyakazi, Nyumba nadaiwa n.k
[HASHTAG]#SIRIZANDANI[/HASHTAG]
Da uzur pasipo akili nisawa saa bila betry
 
Back
Top Bottom