sangaone98
Senior Member
- Apr 16, 2024
- 160
- 288
Heshima yenu wakuu, niende direct kwenye mada.
Alizongwa na zimwi aliskika jirani akitoa hoja kwa kijiji, sababu ya kukosa elimu ya maambukizi walihisi kulogwa ndio tafsiri ya gonjwa la ukimwi.
Huo ni ugonjwa jamani kama magonjwa mengine alisema mwalimu,
Mwenyekiti alifoka na kumwambia kaa kimya sio unaropoka kama mwenda wazimu.
Elimu ya mwalimu ilikuwa ni nuru potevu, nuru ambayo haifiki gizani ikawekwa idhini mezani, kuwa mizimu imechukia mgonjwa afukuzwe kijiji cha mbali.
Akasindikizwa njia panda mwisho wa makazi mwanzo wa msitu mkubwa wa sanza akatengwa kama walivyo tengwa wengi kwa mila na desturi zilizo wekwa tangu enzi.
Kibuyu cha maji furushi la matunda na makubazi yaliyo waalika funza,
Hakuna hodi inapofika kihama, mama na nyika nyika na mama na alikuwa pekeyake na ule mzigo mdogo mgongoni wasi wasi usoni mtoto tumboni.
Alitamani matawi yaanguke yamtunze zidi ya baridi ya mji ulio sahaulika na wabunge. Umauti aliuhisi alijitazama na hakuona tofauti na maiti alilia pekeyake polini huku sauti yake ikisindikizwa na sauti za fisi.
Wadudu wenye sumu nyingi walimvizia alikutana na visiki alipo hisi njia mvua kubwa ilinyesha kuonyesha hata hali ya hewa ilimsaliti pia
Alivuka sama mpaka ng'ambo akajikongoja mpaka kando,
Kando kweny mti mkubwa uchungu ulimshika akazaliwa mtoto mdogo huku mama anakufa
Ujinga ulio tamalaki kwa kijiji ndio ujinga ulio myima haki ya kuishi alipambana mpaka ilifika tamati pumzi akamuacha mwanae na zawadi ya virusi.
Natoa nukuu kalili mtoto alifunikwa na nguo kuukuu kwenye mwili alikuwa na madoa makuu mawili katikati ya mgongo mfano wa tatoo ya asili
(DIZASTA VINA)
cc dizasta vina.