Hivi huyu Joti huwa anawachekeshaje watu?

Hivi huyu Joti huwa anawachekeshaje watu?

Bongo hapa wale stand up comedian ndo best kina Nalimi, haleluya, leonardo na wengine wengi na ukija kwa best script writer kuna steve mweusi na clamcriss
 
Kilichokufanya umponde Joti ni coz ametaja issue ya katiba,unaonekana umetawaliwa sana na issue za kisiasa,relax mkuu,life is very short.
Mtu unaanzaje kuwa mshabiki wa siasa miaka hii!! Huo si ujinga mwingine? Ila nimesikitika sana kusikia kuwa Joti huwa anakuchekesha.
 
Inawezekana wewe hakuchekeshi ila kuna anao wachekesha watu sio maroboti kwamba watachekeshwa na kichekesho cha aina moja
Jamaa wa Cheka Tu wanajitahidi sana. Wanakaa na kuumiza vichwa.
 
Inawezekana wewe hakuchekeshi ila kuna anao wachekesha watu sio maroboti kwamba watachekeshwa na kichekesho cha aina moja
Kuna clip wako na mzee wake wameenda kuagiza chips. Wanasema wanamuagiza muuzaji, "Weka pilipili, weka kachumbali, weka chumvi, weka majivu, temea na mate!!" Mtu mwenye akili timamu anachekeshwaje na mambo kama hayo?

Kenya wametuacha mbali kwenye comedy sijui sisi huku ni nini tunafanya. Mfano Njugush, Wilibroda, Awinja nyamwalo, Crazy Cennar, na wale wa kule Churchill show wanafanya kazi nzuri kwa kweli. Tanzania tuige huko.
 
Mtu unaanzaje kuwa mshabiki wa siasa miaka hii!! Huo si ujinga mwingine? Ila nimesikitika sana kusikia kuwa Joti huwa anakuchekesha.
Kwahiyo unataka mchekeshaji asiye kuchekesha wewe ndio asiwachekeshe watu wote?

Hatufanani hisia,unajipa kazi ngumu sana aisee yakuwachagulia watu furaha zao.
 
Kwahiyo unataka mchekeshaji asiye kuchekesha wewe ndio asiwachekeshe watu wote?

Hatufanani hisia,unajipa kazi ngumu sana aisee yakuwachagulia watu furaha zao.
Humu hakuna anayeweza kumchagulia mtu mwingine cha kufurahia. Nashangaa na kuuliza watu wanachekeshwaje na Joti? Mpaka sasa sijapata jibu.
 
Masanja ni mara 3 ya joti kwenye kuchekesha
 
Siku hizi kwa kweli hachekeshi kivile. Atafute
mtu wa kueleweka amuandalie contents. Na naona hajalenga sanaa yake iende mbali. Hii ni mbaya kweli, maana haya ya aina ya enzi za Kaole huwa yanapitwa na wakati. Anavichekesho / videos za kilocal sana, namna ile ile ya miaka nenda rudi.
 
Back
Top Bottom