Hivi huyu ni MZAZI kweli?

Hivi huyu ni MZAZI kweli?

Dreamliner

JF-Expert Member
Joined
Jan 17, 2010
Posts
2,034
Reaction score
214
Tunaishi na Msichana wa kazi karibu miaka 2 sasa, Mwezi huu my wife wangu alifiwa na shangazi, hivyo tukaenda kwenye msiba kwao. Ambako ndio anakotoka binti yetu. Nikamwambia Wife ni muhimu twende kwao na binti. Bahati nzuri tulimkuta Mama yake Mdogo... Ambapo yeye husema Mama yake mzazi alifariki akiwa bado mdogo... Baada ya mazungumzo marefu na huyu Mama mdogo, alianza kwa kusema kuwa, Huyu binti hawana undugu kabisa, ila alipokuwa msichana mahali fulani, alikuja Mama mmoja na mtoto wa miaka mitatu na AKAMTUPIA huyo mtoto akidai ya kuwa, amesikia huyu Dada (Wakati huo) anatembea na Mume wake.... Juhudi zote za kumhakikishia kuwa si kweli, ziligonga mwamba.

Mpaka hv leo, huyu binti anafahamu Mama yake alifariki akiwa mdogo, kwa hiyo hamjua Mama yake Mzazi. Na Mama mzazi wa binti huyo, anaishi umbali usiozidi km tano. Lakini hajawahi kuulizia habari yoyote kuhusu Mtoto wake, na anakaribu miaka 20.... Na huyu binti, anampenda sana sana Mama yake mdogo..

Wakuu wanaJF, Je huyu binti aelezwe ukweli? au mnaonaje?
 
Jamani...inasikitisha kweli!!

Ubaya wa kumwambia ni kumuumiza binti kwasababu mama yake kwanza hakumtaka na hata sasa hivi hana muda nae.Kitakachofuata ni binti anaweza akapenda kuwasiliana na mama yake alafu mama akamwambia kabisa kwamba hamtaki wala hamhitaji maishani mwake japo ameshakua.Hii inaweza kumfanya binti akaathirika sana kisaikolojia!

Asipoambiwa nayo inamkosesha nafasi ya kuweza kuwajua watu ambao ni ndugu zake wa damu!Kitu ambacho kwakweli ni kizuri kufahamu!Binafsi siwezi kumchagulia kama aambiwe au la ila ingekua mimi ningependa kujua ili hata kama hanitaki niendelee na maisha yangu!!Na hivi ana matatizo na mama mdogo.....nwy pole yangu imfikie!
 
Infact hana matatizo na Mama yake mdogo, wanapendana sana Lizzy.
 
Infact hana matatizo na Mama yake mdogo, wanapendana sana Lizzy.

Ahhhhh kumbe mama mzazi ndo alidai ‘‘mama mdogo“ alitembea na mumuwe?!
Basi aachwe tu...au ikibidi mtu aongee na mama mzazi kwanza kujua kama angependa kufahamiana na bintiye au la!Kama ataprnda basi binti aambiwe alafu nae akipenda wakutanishwe...mama akikataa basi mnamwacha aendelee kuamini alikufa!!
 
lizzy una taaluma ya hii fan maana ushauri wako unanivutia sana.
 
Huyo bint aambiwe ukweli,ili ajue uozo wa mama yake.na yeye asijefanya hivyo.
 
Kama mama hamtaki mtoto, watu wengine wamemkubali mtoto na kumlea mpaka kawa mkubwa, mtoto anajua mama yake alikufa zamani, ukitaka kumwambia mtoto mama yake yupo utakuwa na rationale gani? Utatibua mambo tu kwa maoni yangi.

1. Utatibua amani ya mtoto, ambaye anafikiri mama yake alishafariki, sasa atajua mama yake ni mnyama aliyemtupa tu.
2. Utatibua amani ya mama ambaye anajua kashamtupa mtoto na sasa maisha yanaenda kama alivyotaka.
3. Utatibua amani ya wote wanaozunguka kwa kufufua mzozo mpya uliokwishazikwa.

Haya mambo yaachwe tu kama yalivyo, mambo yakija kugundulika kwa bahati hilo ni swala lingine. Lakini kutibua mambo hakuna tija.
 
Back
Top Bottom