Dreamliner
JF-Expert Member
- Jan 17, 2010
- 2,034
- 214
Tunaishi na Msichana wa kazi karibu miaka 2 sasa, Mwezi huu my wife wangu alifiwa na shangazi, hivyo tukaenda kwenye msiba kwao. Ambako ndio anakotoka binti yetu. Nikamwambia Wife ni muhimu twende kwao na binti. Bahati nzuri tulimkuta Mama yake Mdogo... Ambapo yeye husema Mama yake mzazi alifariki akiwa bado mdogo... Baada ya mazungumzo marefu na huyu Mama mdogo, alianza kwa kusema kuwa, Huyu binti hawana undugu kabisa, ila alipokuwa msichana mahali fulani, alikuja Mama mmoja na mtoto wa miaka mitatu na AKAMTUPIA huyo mtoto akidai ya kuwa, amesikia huyu Dada (Wakati huo) anatembea na Mume wake.... Juhudi zote za kumhakikishia kuwa si kweli, ziligonga mwamba.
Mpaka hv leo, huyu binti anafahamu Mama yake alifariki akiwa mdogo, kwa hiyo hamjua Mama yake Mzazi. Na Mama mzazi wa binti huyo, anaishi umbali usiozidi km tano. Lakini hajawahi kuulizia habari yoyote kuhusu Mtoto wake, na anakaribu miaka 20.... Na huyu binti, anampenda sana sana Mama yake mdogo..
Wakuu wanaJF, Je huyu binti aelezwe ukweli? au mnaonaje?