Hivi idara ya usalama wa taifa wa Tanzania inahusika na kila kitu hadi uuzaji wa nyanya na vitunguu magengeni?

Siyo mjuzi sana wa habari za idara ya usalama wa taifa, Tanzania.

Lakini katika pitapita zangu humu JF, nimekutana na mada kadhaa zilizonishangaza kidogo.

Mtu akienda dukani akikuta bidhaa ambayo haipendi, lawama anabebeshwa usalama wa taifa.

Msanii Diamond umaarufu wake ukianza kupungua, lawama zinaenda kwa usalama wa taifa!

Timu za mpira za Tanzania zisipofanya vizuri kwenye mashindano ya kimataifa, lawama kwa usalama wa taifa!

Ni mimi tu ambaye sielewi dhima nzima ya usalama wa taifa au inakuwaje?

Kwa mfano, usalama wa taifa wanahusikaje na uwepo wa bidhaa za Kenya kwenye maduka ya Tanzania?

Kwa akili zangu hizi za panzi, waamuzi wa mafanikio ya bidhaa ni wateja/ wanunuzi.

Kama wateja/ wanunuzi wanaona bidhaa fulani ni bora kuliko bidhaa ingine, basi wataendelea kuiunga mkono kwa kuinunua.

Na ubora wa bidhaa sidhani kama unahusiana chochote na idara ya usalama wa taifa.

Ubora wa bidhaa unatokana na ubunifu wa mzalishaji. Mzalishaji anapotengeneza bidhaa iliyo bora halafu akaitangaza kwa umma, umma huo ndo utaamua mafanikio ya hiyo bidhaa.

Sasa kama makampuni ya Tanzania hayatengenezi bidhaa zilizo bora kutokana na kushindwa kuwa wabunifu, lawama kwa usalama wa taifa zinahusikaje?

Hmm…..yawezekana ni mimi tu na hizi akili zangu za panzi ndo maana labda sielewi.

Wajuvi na wajuzi wa mambo nijuzeni, tafadhali.
Wewe ulifikiri kazi za usalama wa taifa ni zipi?
 
Sasa naanza kuelewa kwa nini Tanzania ni banana Republic!

Ni kwa sababu ya ujinga kama huu.

Kudhani kuwa usalama wa taifa ndo watengeneza sera za kiuchumi.

Kudhani kuwa usalama wa taifa ni wataalamu wa uchumi na maendeleo!

Hapa tulipo kiuchumi si bahati mbaya wala si ajali.

Ni matokeo ya kutojua cha kufanya.
TISS kuna taaluma zote unazozijua wewe Duniani na ndiyo maana wakapewa pia jukumu la kufanya vetting ya viongozi!

Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app
 
Wewe kweli junya.

Hata hujui tofauti ya R na L.

Hujui R uitumie wapi. Hujui L inatumika wapi.

Sasa ndo utajua dhima ya usalama wa taifa kweli?
Mkuu umekunywa pombe gani mbona leo unaandika hoja za kijinga sana.Mimi siyo Mwalimu wa Kiswahili na wala sijajitambulisha humu jukwaani kama mtaalamu wa lugha.
Ila kwa muda ambao nimekuwepo hapa jamvini leo umeandika mashudu!

Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu umekunywa pombe gani mbona leo unaandika hoja za kijinga sana.Mimi siyo Mwalimu wa Kiswahili na wala sijajitambulisha humu jukwaani kama mtaalamu wa lugha.
Ila kwa muda ambao nimekuwepo hapa jamvini leo umeandika mashudu!

Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app
Kumkosoa mtu kwa matumizi ya kimakosa ya herufi si ujinga.
 
Mi najiuliza tuu hadi huu ubadhilifu unafanyika ngazi ya halimashauri wao ofisi ya DSO huwa ipo busy na majukumu gani?
Kurundikana kwenye misafara ya Mama, Majaliwa, Mpango....
Kujimwambafai mitaani..
Kutumia blank cheques...
 
Nilishangaa nilipoona stick za kuchokonolea meno (Tooth Sticks) zinatoka china, tissue yani yale makaratasi yanatoka china. Sasa hiyo financial intelligence unit sio tu kufuatilia miamala ya Chadema na wapinga serikali walipaswa wawe silaha ya kuandaa sera ya maendeleo na kushauri na kusimamia utekelezaji wake, lasivyo tutajeuzwa wategemezi na hii hasara yake tushaiona kwakua hela yetu haina nguvu tunakua forced kununua vitu nje kwa Dola mwisho wa siku ipo siku mkate tutaunuua kwa Million moja ya Tsh, usishangae maana leo hii mkate unauzwa 4000/=, wakati huo ulikua mshahara wa miezi minne wa Mwl. Nyerere alipokua Mwalimu.
Ushauri mzuri sana lakini una madhara ya aina mbili
1. Hali Maisha ya watu kuimarika
2. Watawala kupoteza madaraka
Hapo kwenye namba mbili ndio utata ulipo(Hofu)
 
Siyo mjuzi sana wa habari za idara ya usalama wa taifa, Tanzania.

Lakini katika pitapita zangu humu JF, nimekutana na mada kadhaa zilizonishangaza kidogo.

Mtu akienda dukani akikuta bidhaa ambayo haipendi, lawama anabebeshwa usalama wa taifa.

Msanii Diamond umaarufu wake ukianza kupungua, lawama zinaenda kwa usalama wa taifa!

Timu za mpira za Tanzania zisipofanya vizuri kwenye mashindano ya kimataifa, lawama kwa usalama wa taifa!

Ni mimi tu ambaye sielewi dhima nzima ya usalama wa taifa au inakuwaje?

Kwa mfano, usalama wa taifa wanahusikaje na uwepo wa bidhaa za Kenya kwenye maduka ya Tanzania?

Kwa akili zangu hizi za panzi, waamuzi wa mafanikio ya bidhaa ni wateja/ wanunuzi.

Kama wateja/ wanunuzi wanaona bidhaa fulani ni bora kuliko bidhaa ingine, basi wataendelea kuiunga mkono kwa kuinunua.

Na ubora wa bidhaa sidhani kama unahusiana chochote na idara ya usalama wa taifa.

Ubora wa bidhaa unatokana na ubunifu wa mzalishaji. Mzalishaji anapotengeneza bidhaa iliyo bora halafu akaitangaza kwa umma, umma huo ndo utaamua mafanikio ya hiyo bidhaa.

Sasa kama makampuni ya Tanzania hayatengenezi bidhaa zilizo bora kutokana na kushindwa kuwa wabunifu, lawama kwa usalama wa taifa zinahusikaje?

Hmm…..yawezekana ni mimi tu na hizi akili zangu za panzi ndo maana labda sielewi.

Wajuvi na wajuzi wa mambo nijuzeni, tafadhali.

Mie sijawahi kuona au kusikia mtu analaumu usalama wa taifa mtaani
Mimi naona ni serikali tuu kiujumla sijajua mtaani kwako huko[emoji23]
 
Back
Top Bottom