Hivi inakuaje dagaa wamekuwa ghali kuliko nyama?

Hivi inakuaje dagaa wamekuwa ghali kuliko nyama?

Habari zenu,

Miaka ya nyuma tulizoea kuwa dagaa ni mboga ya watu wa hali ya chini lakini nimeshangaa sehemu ninayoishi kwa sasa nyama ndio imekuwa mboga watu wa hali ya chini tunaweza kuimudu.

Mfano huku kwetu 1kg ya nyama ya ng'ombe ni tsh 6,500/= wakati kilo ya dagaa ni tsh 10,000/=, samaki 11,000/=.
Imekuaje dagaa wamepanda bei ghafla?
Kilo Moja ya dagaa mtakula zaidi ya siku 5.ila nyama huwezi kula zaidi ya siku 1kwa hyo kg 1
 
Hii ID yako kama inamaanisha kyagata kile kijiji kinachopatikana huko wilaya ya butiama, ni sahihi kilo 1 ya nyama iwe 6,500/=.

Kwanza hata hapo bado mnapigwa. Ilitakiwa iwe 5,000/= maana hapo ni jamii ya wafugaji na ni kijijini.
 
1.Inategemea na eneo ulilopo
2. Upatikanaji wa aina kitoweo ni rahisi kiasi gani
Nyama zipo nyingi na nirahisi kupatikana kila maali na zinahitajika watumiaji ni wengi pia
Dagaa nayo imekuwa hitaji kubwa sana kwa watu wengi ila hupatikanaji wake ni mdogo ukilinganisha na nyama
 
Sisi huku kwetu hatununui kwa kilo ila ukweli ni kuwa kwa sasa kula nyama ni nafuu kuliko kula samaki na tupo karibu na ziwa
NB: hii ni kwa upande wa familia yetu
 
Habari zenu,

Miaka ya nyuma tulizoea kuwa dagaa ni mboga ya watu wa hali ya chini lakini nimeshangaa sehemu ninayoishi kwa sasa nyama ndio imekuwa mboga watu wa hali ya chini tunaweza kuimudu.

Mfano huku kwetu 1kg ya nyama ya ng'ombe ni tsh 6,500/= wakati kilo ya dagaa ni tsh 10,000/=, samaki 11,000/=.
Imekuaje dagaa wamepanda bei ghafla?
Dalili za ushindi kwa motivational Speakers siyo bure.
 
Back
Top Bottom