Hivi inakuaje gari namba C halafu mile-age ni ndogo sana

Hivi inakuaje gari namba C halafu mile-age ni ndogo sana

Kuna gari naifahamu imenunuliwa mileage 9000km.. Ina mwaka na nusu sasa inasoma km 27000.. Sasa huyu MTU akiichoka mpaka anaiuza itakuwa bado mileage iko chini Sanaa.. So inategemea alinunua ilisoma ngapi na matumizi yake yako vipi...
 
Yard pembezoni mwa Jangwani Sekondari along Morogoro Rd. Ni ya Wazanzibari wanachomekea (baadhi) ya magari toka ZNZ ukijichanganya inakula kwako nilishawahi kununua gari 3 kwao 2015 (enzi za dili) kidogo zinifie nikawasukumia walugaluga huko ZOOM na KUPATANA. But gari yangu ya 2006 namba AAU bado ipo poa
 
Wakuu kuna ka gar flan hapa nipo kwenye ku negotiate,.namba C ila sasa mile age ni 70000,body nzuri,.ila sasa mmh,..na bei sio kivile sana,kawaida,na sio yard...msaada puliz
Labda alikuwa hatembei nayo sana au ilikuwa imepata ajali ikawa haitembei au alininunua km zikiwa chini sana eg 25000
 
Hiz heruf znaweza kukuambia umri wa gar kwa maana,ina mda gan toka imesajiliwa,mfano A,ni ya mda mref na D is almost current,pia mile age itasema kama hii gar imetumika saaana,..sasa mim hii gar ni ya mda ila haijatumika sana,sasa ndo sjaelewa scenario hii.anyways ngoja nijue nafanya nin

You are getting it all wrong..
Mfano; ukifanikiwa kuingiza gari ya mwaka 1987; rarely used from Japan; je utapewa namba A, B, C au D??
 
Binafsi nilinunua gari namba A, mwaka 2012 mwishoni, kwa mtu ambaye alikuwa na gari 5. Nilikuta ina km 73,000+. Ila mpk sasa ina 145k.

Sina safari nyingi za kutumia private car, ni mizunguko ya town tu.

This makes a lot of sense
 
Mkuu acha ushamba, mileage ya gari ni matumizi na sio imenunuliwa au imesajiriwa lini, ukifuatilia gari kama range rovers utakuta zina mileage chache sana hata 20,000km lakini unakuta ina namba A. Binafsi niliwahi kujiuliza sana mpaka nikafuatilia kama kuna namna mtu anaweza punguza mileage nikakuta ni kitu kisichowezekana.
 
Magari ya wahindi mara nyingi hayana mileage kubwa hasa wale walioko katikati ya mji, mfano Dar,unakuta ofisi yake ni duka,liko chini kwenye ghorofa anamoishi,sokoni na maduka ni walking distance,gari linatumika weekend tu kwenda Coco beach na kurudi nyumbani,kwahiyo wiki nzima gari halitumiki limepaki garage..
 
Back
Top Bottom