Hivi inakuaje unanunua gari halafu unalifungia kibandani badala ya kulitumia?

Hivi inakuaje unanunua gari halafu unalifungia kibandani badala ya kulitumia?

Kuna jamaa yangu amestaafu hivi karibuni. Kanunua Harrier, hajui kuendesha, kuendeshwa Mara moja kwa wiki akienda kanisani, kwenda sokoni kwa mguu! Hivi jamani ni salama kweli hapo?
Hata kama unayo matano si vizuri kuzoea magari hata kwa safari fupifupi.. Kutembea ni mojawapo ya mazoezi bora kabisa ya mwili

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Iko poa tu ,mi gari naenda nayo out na family ,au kwenda mkoani ,kwa mitaa ya nyumbani na sokoni unapanda tu bajaji kwa jero na kurudi kwanini uweke mafuta ya 10,000
 
Kuna jamaa yangu amestaafu hivi karibuni. Kanunua Harrier, hajui kuendesha, kuendeshwa Mara moja kwa wiki akienda kanisani, kwenda sokoni kwa mguu! Hivi jamani ni salama kweli hapo?
Huyo atakuwa alikuwa afisa mwandamizi alizoea kuendeshwa na pia siyo mtu wa misifa,nadhani siyo mtu wa lake zone huyo,atakuwa labda ni mkinga,maana hawa watu wako low profile.Otherwise namuona akiishi miaka mingine mingi sana yenye furaha baada ya kustaafu.Hasa ukizingatia ni mtu wa Ibada Maana hapo akina Manka wameshayakosa mafao yake,maana ni watalaamu sana wa kutumia mafao ya wastaafu halafu mafao yakikata unatolewa mkuku,unarudi zako kwa Bi-mkubwa kuuguzwa kabla ya kufa.
 
Mkuu wanyakyusa wote mpo hivi kwa tabia...?
Umejuaje? Wanyakyusa ndivyo walivyo! Wanapenda sana kuona wastaafu wanarudi wachovuu halafu wanakuwa waleviwalevi wa pombe! Basi hapo roho zao zinakuwa kwatu!
Ukienda na vitu kama hivyo wanakuchukia bila sababu.
 
Ni salama sana. Hana mambo mengi na ataishi muda mrefu Inshaallah.

Na angepiga ruti nyingi za kula bata ungemlaumu.

Jamani hadi wazee mnafuatiliana kama kina mwijaku na Lokole[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Matumizi standard ya kistaarabu kubajeti gharama ya mafuta.Kwani akipaki linapotea au? Gari lake akiamua au akiishiwa anapaki anavyotaka.
 
Daah bongo kiboko mtu kanunua gari lake unaenda kulichungulia kama leo limetoka au laa mpaka unakuja kuanzisha Uzi..
 
we jamaa, em muache msukuma wa watu na 'hariya' yake., hiii!
 
Daaaa!! Kweli jamii forum imepotea !!!
Mada gani hizi jamani!?? Mbona nchi INA mambo mengi tuu!??
Hivi MTU kanunua gari hajui kuendesha INA kuumiza kichwa!?? Dahhh
 
Sasa wewe vinakuhusu nini jamani? hata akisema alibebe mgongoni acha abebe si lake jamani kwanini tunapenda kupangiana jinsi ya kuishi?
 
Back
Top Bottom