Tatizo sio polisi wala CCM.
Tatizo upinzani hauna viongozi waliokomaa kisiasa ,kijamii na kiusalama.
Kidogo ACT naona kuna uongozi makini kiasi Fulani lakini pia wajitahidi kuwa na intelijensia ya kutosha.
Wakubali kuwa Kufa kwa CUF na Chadema ni mpango wa Mungu kwani hivyo vyama viliwaabudu wenyeviti wao wakasahau kuwa mageuzi na mabadiliko sio suala la Mbowe na Lipumba bali ni suala la Watanzania wenyewe.
Mbowe kujitapa kuwa yeye ndiye Chadema na Lipumba kuwa yeye ndiye CUF ,mwenyezi Mungu amewaumbua na vyama vyao vimesambaritika wakiwa wanaviongoza huku wakibaki na aibu kubwa na ACT na NCCR vikichanja Mbuga.
Nawashauri ACT na NCCR wazingatie sheria na kanuni za Jeshi la Polisi zinazowataka kutoa taarifa polisi wakati wa shughuli zote za kisiasa kwenye maeneo ya nchi yetu.
Hii ni kwa faida yao wenyewe.
Mfano kwa sasa ni wazi kuwa kuna uadui mkubwa sana kwa wanasiasa ndani na nje ya vyama vyao.
CUF una uhasama na ACT.
Chadema ya Mbowe inauhasama na CCM inayoshikiliwa na waasisi wa mageuzi ndani ya nchi hii na wapinga ufisadi. Kumuunga mkono Mbowe ni kuunga mkono Ubeberu, ulevi wa pombe,ulevi wa madaraka , uongo, udikteta , umangi meza ,ubinafsi ,uchoyo ,ufuska,uhuni,usaliti, kuabudu mizimu , ubabe na wizi. Huyu na wote wanaomuunga mkono mwisho wao ni Mwaka huu.
Hatutaki kusikia Chadema ikiwa chini ya huyu Mtu mwovu.
Salama ya Chadema ni kumtoa msaliti wa Demokrasia Mbowe.
Zito Kabwe wajenge vijana wako wawe Jasiri lakini wafuate sheria na kuhakikisha hawakwaruzani na vyombo vya Dola.
Kutoa taarifa kunawafanya watu wa ulinzi kuwa na utayari wa kuhakikisha hakuna chama kinachovamiwa na wahuni wa vyama vingine.
Hivi ni Mkuu gani wa Polisi atakubali kuona wanasiasa wanaopanga mikakati ya kushika dola wanaifanya kwenye eneo lake na kutoa matamko makali bila kujua kuwa walikuja lini na wanaifanyia wapi na kwa muda gani?
Haiwezekani tukubali tu kuwa ni busara kwa kipindi hiki vyama vyote vitoe taarifa na sio kuomba kibali Bali ni kutoa taarifa iwe ni kikoa cha ndani au cha nje. Hii itaepusha vurugu za polisi na wanasiasa.
Zito amekomaa kisiasa nadhani anaelewa umuhimu wa kuepuka hii mitego.
ACT imewashika pabaya wote ikiwemo Chadema na Msaliti Mbowe na wasaliti wenzake akina Lipumba ,Mrema,Cheyo,Mbatia, Rungwe, na wengineo wanaongangania uenyekiti wa maisha.
Asiyetaka kutoa taarifa polisi basi ajue ataendelea kula Bakora mwanzo Mwisho Mwaka huu.
Toeni Taarifa,kisha simamieni haki yenu ikiwezekana mfikisheni mahakamani kwa mtu yeyote anayekiuka katiba na anayewazuia wakati mna nakala ya barua ya taarifa na haki ya kukusanyika kwa amani.