Jacob Steven huyu JB mwigizaji au?
Kama uliambiwa kwamba ni Nabii wa kweli bhasi wote mmeingiwa na Pepo Mchafu kutoka kwa Mungu ili mtabiri uongo...
Yeremia 14:14
“Hao manabii wanatoa unabii wa uongo kwa jina langu. Mimi sikuwatuma, wala sikuwaamuru, wala sikusema nao. Wanawatabiria maono ya uongo, maaguzi yasiyo na maana yoyote, uongo wanaojitungia wenyewe"
Unahisi watu hawaitukani Imani yenu Ya Ukristo au Dini kwa Ujumla kwa Hoja dhaifu mnazotoa na Utabiri mnauotoa hayo ndo Petro aliyowahi kuwaandikia..
2 Petro 2:2-3
"Na wengi watafuata ufisadi wao; na kwa hao njia ya kweli itatukanwa.
Na katika kutamani watajipatia faida kwenu kwa maneno yaliyotungwa; ambao hukumu yao tangu zamani haikawii, wala uvunjifu wao hausinzii."
Unakumbuka Kipindi cha Ahabu , Mfalme wa Yuda Yehoshafati, mfalme wa Israel na Kipindi cha Mikaiya, Kulitokea Nini??
1 Wafalme 22:22-23
"BWANA akamwambia, Jinsi gani? Akasema, Nitaondoka, na kuwa pepo wa uongo kinywani mwa manabii wake wote. Akasema, Utamdanganya, na kudiriki pia; ondoka ukafanye hivyo.
Basi angalia, BWANA ametia pepo wa uongo kinywani mwa manabii wako hawa wote; naye BWANA amenena mabaya juu yako."
Nakutakia Asubuhi Njema kabisa