Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,699
- 22,598
Ni kitu ambacho siku zote sijakielewa, na labda ndugu zangu Waislamu watanisaidia hapa. Kufunga najua ni suala la kujipa muda wa kutafakari matendo na maisha yako na kuboresha uhusiano wako na Mwenyezi Mungu. Sasa sielewi kwa nini jambo hili lihusianishwe na kuonekana au kutoonekana kwa mwezi? Kwa nini isijulikane kwamba ukianza kufunga leo, basi utakuwa katika mfungo kwa siku 30, na zikiisha basi, mwezi uwepo au usiwepo, unakuwa umemaliza kipindi chako cha utafakari, kwa kuwa kutoonekana au kuonekana kwa mwezi katika siku fulani ni jambo tu la kijiografia katika mizunguko ya sayari.
Najua kwa Waislamu mwezi na alama yake ni muhimu kama ilivyo msalaba kwa Wakristo, ambapo kwa Waislamu mwezi huwakilisha mwongozo wa Mwenyezi Mungu katika njia ya maisha, wakati Wakristo huuona msalaba kama ishara ya ukombozi wa dhambi kupitia Yesu, na ndio maana alama ya mwezi na msalaba vina sehemu kubwa katika dini hizi mbili.