(not debating just leaving this here)
1) Kama kawaida katika changamoto za Biblia,
mambo hayako rahisi kama yanavyoweza kuonekana mwanzoni.
Badala ya kudhani kwamba Maandiko yamekosea, watafsiri makini zaidi (na wenye uzoefu) watasita kutoa hukumu na kutafuta suluhisho.
Hii si kupinga kwamba kuna makosa / tofauti za kunakili katika nakala za maandiko, bali kwamba baadhi ya tofauti kati ya mistari inaweza kuwa na
ufahamu mkubwa zaidi ikiwa tutakabiliana nazo kwa makini badala ya
kudhani kwamba ni tu
kosa la kunakili ndilo chanzo cha tofauti hiyo.
"Ahazia alianza kutawala akiwa na umri wa miaka ishirini na miwili, akatawala kutoka Yerusalemu kwa muda wa mwaka mmoja. Mama yake aliitwa Athalia, mjukuu wa mfalme Omri mfalme wa Israeli."
2Wafalme.8.26.BHN
"Ahazia, alianza kutawala akiwa mwenye umri wa miaka arubaini na miwili, akatawala kutoka Yerusalemu kwa muda wa mwaka mmoja. Mama yake aliitwa Athalia, mjukuu wa Omri."
2Nyakati.22.2.BHN
2) Wengi wamegundua jinsi herufi za 22 na 42 zinavyofanana hivyo kupendekeza kwamba mwandishi anaweza kuwa amesoma na kuikopi vibaya.
Hii inaweza kuwa ndiyo tafsiri, lakini inakutana na tatizo: Nakala za
Kiebrania katika mistari hii miwili hazitumii
herufi kuwakilisha umri, bali zinatoa umri kwa
maneno.
[ḇen–ʾarbāʿîm wšettayim šānâ] : [a] son of forty and two years :
Mwana wa miaka arobaini na miwili
[ḇen–ʿeśrîm wšettayim šānâ] : [a] son of twenty and two years :
Mwana wa miaka ishirini na miwili
Maneno ya
arobaini na
ishirini si rahisi kuchanganywa.
Hili limewafanya baadhi ya chronologists kufikia maelezo mengine ambayo ndani yake kauli zote mbili zinaweza kuwa za
kweli.
3) Ufunguo wa kuelewa jambo hili unapatikana kwa kutambua kwamba kwa Kiebrania
hapasemi “mwenye umri wa miaka arobaini na miwili.” Badala yake anatumia msemo wa Kiebrania “
mwana wa miaka 42.”
Swali linakuwa: mwana wa nani?
4) Ingawa inaweza kumaanisha “mwana aliyezaliwa na baba yake wa karibu miaka 42 iliyopita,” neno mwana lina maana pana sana katika Kiebrania, na mara nyingi hutumiwa kuhusiana na
babu au
mtangulizi mwingine, si lazima baba wa moja kwa moja.
Hili ndilo wazo
linalopendekezwa na wachambuzi wengi wa Biblia.
5) Kitu kimoja ambacho mistari yote miwili inasisitiza ni kwamba jina la
mama yake lilikuwa Ataliah, mjukuu wa Omri ambaye alikuwa mfalme wa Israeli (Ufalme wa Kaskazini).
Kwahiyo Hapa kuna mfalme ameketi kwenye kiti cha enzi cha Yuda (
Ufalme wa Kusini), ambaye ni mzaliwa wa ukoo uliomuasi MUNGU kutoka
Ufalme wa Kaskazini.
Omri ni baba wa
Ahabu, mfalme muovu aliyemuoa malkia muovu
Yezebeli. Kwahiyo huyu mama
Athaliah ni mjukuu wa Yezebeli.
"Omri alitenda maovu mbele ya Mwenyezi-Mungu; alifanya maovu zaidi ya wale wote waliomtangulia."
1Wafalme.16.25.BHN
"Nyinyi mnafuata mfano mbaya wa mfalme Omri na mfano wa jamaa ya mfalme Ahabu na mfano mbaya wa jamaa ya mwanawe, Ahabu, na mmefuata mashauri yao. Kwa hiyo nitawaleteeni maangamizi, na kila mtu atawadharau. Watu watawadhihaki kila mahali.”
mika.6.16.BHN
MUNGU anakataa kumtambua Ahazi kama mwana wa Daudi, badala yake anamtambulisha kupitia mama yake, mjukuu wa Yezebeli muovu.
Yeye ni
mzao wa nyumba ya
Ahabu, mwana wa nyumba ya
Omri, na kwa maana hiyo ni “mwana wa miaka 42,” kwa kuwa nasaba (
dynasty) ya nyumba ya Omri ilikuwa na umri wa miaka 42 kamili.
Hiyo
si njia ya “kisasa” ya kuandika historia, bali ni njia ya waandishi wa Agano la Kale na wa Agano Jipya.
Huo ulikuwa mwaka wa 42 kamili wa nasaba (dynasty) ya Israeli aliyoiunda Omri mwaka
929 BC alipomuua Zimri.
Miaka hii 42
si umri wa Ahazia, bali ni umri wa
utawala wa familia ya Omri, mfalme wa Israeli.
Umri wa Ahazia unakuja kutajwa kuwa ni 22.
6) Wengine hufasiri hiyo miaka 42 kuwa ni
umri wa mama yake Athalia, yaani mwana wa mama aliyekuwa na umri huo; na kwa haki kabisa umri wake ukawekwa badala ya wake, ili
kumlaumu, kwa sababu yeye ndiye
aliyemwelekeza na kufanya apendavyo—kwa hakika, yeye ndiye aliyekuwa akitawala, naye hakuwa na zaidi ya cheo cha mfalme tu.