Hivi inawezekana tukafanya uchaguzi bila dosari? Wakenya je tupo tayari kweli kwa demokrasia ya kihivyo

Hapa nawaza na kuwasilisha, mahakama ya Kenya imebatilisha matokeo ya uchaguzi kwa kile ilichokitaja kuwa ukiukwaji wa katiba na tume huru ya uchaguzi. Japo mahakama iliomba muda ili itoe maelezo kamili kuhusu ilivyofikia kwenye hayo maaamuzi, hivyo kwa kifupi hadi hapo hakuna anayejua nini sababu haswa za kufutwa kwa matokeo, sote tunasubiri kwa hamu taarifa kamili.

Ninachojiuliza, hivi inawezekana tukarudia uchaguzi na ufanyike mwanzo hadi mwisho bila dosari? Ama ndio tena tutajikuta kwenye hali hii hii baada ya siku sitini zijazo. Kama Wakenya tumejiandaa vipi, maana kampeni zimeanza, hivyo inamaana tutaburuzana kwa miezi miwili ijayo, ikumbukwe pia Raila naye ameanzisha mtiti dhidi ya tume, hivyo lazima patachimbika hadi awatolee nje viongozi wa tume kama alivyofanya kwa wale wa awali.

Vipi katiba inasema nini, ama inawezekana tukarudia chaguzi mpaka basi, maana kila ikitokea dosari tutarudi hapa. Binafsi nina furaha kwa kuona mahakama zetu zimedhihirisha kuwa huru, lakini nahisi sisi wenyewe hatupo tayari kwa demokrasia ya kiwango hicho.
Hakuna nchi yenye kufanya uchaguzi bila dosari tumeona uchaguzi wa marekani ndio wameendelea kwenye kila kitu na mie nimeona muraga na wenzie wamekosewa sababu hoja bishaniwa ilikuwa ni namna kura zilivyosafirishwa kutoka kwenye vituo vya kura kwenda kwenye kituo kikuu Cha majumuisho kisha nikajiuliza kwakuwa odinga ajapinga mahesabu ya kura kutoka kwenye vituo vya kura kwanini hakutoa order ili IEBC warudie upya kuhesabu kura au kusafirisha kura kwa usahihi na Sio kubatilisha uchaguzi wote sasa kama uchaguzi wa uraisi una dosari maana yake hata ule wa magavana, maseneta, wabunge nao ulikuwa batili..... Mahakama imetaka kuweka historia Lakini naamini mwisho wao haukuwa sahihi....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cha msingi sasa hivi ni kusubiri hukumu yenyewe ili tuichambue neno kwa neno na kujua kipi kilisababisha mahakama kubatilisha uchaguzi wote. Binafsi pia nahisi ingekua busara kuzihesabu upya, anyway kwa vyovyote vile tutarudi uwanjani tena kwenye mafoleni na kupiga kura kwa mamilioni.
Wabunge, magava,na maseneta, na MCA wote watatiririka mashinani kuwafanyia kampeni akina Raila na Uhuru, hapo mchezo utakua wa kuvutia.
 
Chapaneni tu tujue moja. Mnachosha.
 
Hapa nawaza na kuwasilisha, mahakama ya Kenya imebatilisha matokeo ya uchaguzi kwa kile ilichokitaja kuwa ukiukwaji wa katiba na tume huru ya uchaguzi. Japo mahakama iliomba muda ili itoe maelezo kamili kuhusu ilivyofikia kwenye hayo maaamuzi, hivyo kwa kifupi hadi hapo hakuna anayejua nini sababu haswa za kufutwa kwa matokeo, sote tunasubiri kwa hamu taarifa kamili.

Ninachojiuliza, hivi inawezekana tukarudia uchaguzi na ufanyike mwanzo hadi mwisho bila dosari? Ama ndio tena tutajikuta kwenye hali hii hii baada ya siku sitini zijazo. Kama Wakenya tumejiandaa vipi, maana kampeni zimeanza, hivyo inamaana tutaburuzana kwa miezi miwili ijayo, ikumbukwe pia Raila naye ameanzisha mtiti dhidi ya tume, hivyo lazima patachimbika hadi awatolee nje viongozi wa tume kama alivyofanya kwa wale wa awali.

Vipi katiba inasema nini, ama inawezekana tukarudia chaguzi mpaka basi, maana kila ikitokea dosari tutarudi hapa. Binafsi nina furaha kwa kuona mahakama zetu zimedhihirisha kuwa huru, lakini nahisi sisi wenyewe hatupo tayari kwa demokrasia ya kiwango hicho.
Tumia akili kuwaza na kujadili maada ambazo zinatakiwa kuwa kioo kwa mataifa yaliyoendelea yaliyoendelea. Hatutarajii kuwa na uchaguzi wenye dosari kwani hiyo inaminya demokrasia kwa kiasi kikubwa. Angalia mataifa mengi duniani yanaiangazia Kenya km nchi yenye katiba huru, thabiti na mihimili yake inaheshimiana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapa nawaza na kuwasilisha, mahakama ya Kenya imebatilisha matokeo ya uchaguzi kwa kile ilichokitaja kuwa ukiukwaji wa katiba na tume huru ya uchaguzi. Japo mahakama iliomba muda ili itoe maelezo kamili kuhusu ilivyofikia kwenye hayo maaamuzi, hivyo kwa kifupi hadi hapo hakuna anayejua nini sababu haswa za kufutwa kwa matokeo, sote tunasubiri kwa hamu taarifa kamili.

Ninachojiuliza, hivi inawezekana tukarudia uchaguzi na ufanyike mwanzo hadi mwisho bila dosari? Ama ndio tena tutajikuta kwenye hali hii hii baada ya siku sitini zijazo. Kama Wakenya tumejiandaa vipi, maana kampeni zimeanza, hivyo inamaana tutaburuzana kwa miezi miwili ijayo, ikumbukwe pia Raila naye ameanzisha mtiti dhidi ya tume, hivyo lazima patachimbika hadi awatolee nje viongozi wa tume kama alivyofanya kwa wale wa awali.

Vipi katiba inasema nini, ama inawezekana tukarudia chaguzi mpaka basi, maana kila ikitokea dosari tutarudi hapa. Binafsi nina furaha kwa kuona mahakama zetu zimedhihirisha kuwa huru, lakini nahisi sisi wenyewe hatupo tayari kwa demokrasia ya kiwango hicho.
Mzee hebu nisaidie kitu kodogo halafu ntakuja kuchangia baadae!

Wafanya kazi wa tume huru ya uchaguzi na mipaka wanapatikana kwa utaratibu upi? Wanawajibika kwa nani? Nini nafasi ya vyama vya siasa dhidi ya tume hii? Utaratibu wa kuwaondoa madarakani ukoje?
 
Muundo wa tume ni makamishna tisa wakiwa na mwenyekiti na naibu wake, halafu pembeni kuna katibu na watendaji wengine.
Huwa lazima bunge iridhie kuajiriwa au kufutwa kwao kazi, rais hana mamalaka juu yao kikatiba. Na kuwafuta huwa ni mchakato unaohusu kuburuzana bungeni, hivyo sio kitu cha kutegemea ndani ya siku sitini zijazo.
Lakini watendaji wanawajibika kwa mwenyekiti na ana uwezo wa kuwatolea nje.
 
Akhsante sana! Niliuliza hili suala kwa kuwa hapa kwenye tume ndo kuna kiini kizima na pengine sura ya nini kinaweza kutokea!

Kwanza ifahamike kuwa wakenya (nikimaanisha wananchi wa kawaida) hawana shida na kuhusiana na haya matokeo. Hata wale tunaowaona wakifanya fujo baada ya uchaguzi kama hakuna neno kutoka kwa hawa wanaotafuta madaraka hawawezi kuonekana wakifanya lolote.

Nikirudi kwenye hoja ya kuwa nabuchaguzi salama hadi mshindi akapatikana, hilo ni suala la kuombea kila mtu kwa imani yake, tena kuomba kweli kweli!

Tayari pande mbili hizi zimeshahitilafiana kimtazamo kuhusu hii tume ya uchaguzi na mipaka! Kama tume hii haitabadilishwa, kama nasa wanavyotaka, ni dhahili matokeo yasipokuwa upande wa nasa wataendelea kulalamikia tume hii na!

Halafu kitu kingine ambacho UK alikosea ni maamuzi ya kutangaza hadharani kuwa hawataibadilisha tume kama nasa wanavyotaka! Kwa jicho la pembeni unaweza kuhisi kuna kitu hapo hata kama hicho kitu hakipo. Nahisi UK angetumia vyombo husika vinavyohusika na kuiweka tume hii madarakani kuonyesha ugumu wa suala hilo kufanyika ndani ya kipindi kifupi hicho!

Lakini kitendo cha UK ambaye ni mgombea na rais kupinga kata kata kubadili tume, tena bila kutoa sababu yoyote ya kitaalamu zaidi ya kusema tu kuwa nasa wamekuwa wakiomba kufanya mambo mengi hivyo kwa hili hawatakubali, inaweza kuonekana kama kuna kitu cha ziada!

Kingine ambacho kwa mtazamo wangu hakikuwa kitu cha kuongea sa hizi ni masuala ya NUSU MKATE. Hayakuwa mambo ya kuongea sa hz maana yanaanza kupanda mbegu mbaya mapema!

Wito wangu kwa hawa wanasiasa wanaoomba madaraka ni kuwa waangalie maslahi ya wakenya! Wapambane tu kwa hoja na mshindi apatikane kihalali ili mambo mengine yaendelee!

Unaona hata hapa jukwaani mijadala ya maendeleo imesimama sababu ya hizi siasa!.
 
Hapa nawaza na kuwasilisha, mahakama ya Kenya imebatilisha matokeo ya uchaguzi kwa kile ilichokitaja kuwa ukiukwaji wa katiba na tume huru ya uchaguzi. Japo mahakama iliomba muda ili itoe maelezo kamili kuhusu ilivyofikia kwenye hayo maaamuzi, hivyo kwa kifupi hadi hapo hakuna anayejua nini sababu haswa za kufutwa kwa matokeo, sote tunasubiri kwa hamu taarifa kamili.

Ninachojiuliza, hivi inawezekana tukarudia uchaguzi na ufanyike mwanzo hadi mwisho bila dosari? Ama ndio tena tutajikuta kwenye hali hii hii baada ya siku sitini zijazo. Kama Wakenya tumejiandaa vipi, maana kampeni zimeanza, hivyo inamaana tutaburuzana kwa miezi miwili ijayo, ikumbukwe pia Raila naye ameanzisha mtiti dhidi ya tume, hivyo lazima patachimbika hadi awatolee nje viongozi wa tume kama alivyofanya kwa wale wa awali.

Vipi katiba inasema nini, ama inawezekana tukarudia chaguzi mpaka basi, maana kila ikitokea dosari tutarudi hapa. Binafsi nina furaha kwa kuona mahakama zetu zimedhihirisha kuwa huru, lakini nahisi sisi wenyewe hatupo tayari kwa demokrasia ya kiwango hicho.

Si mnataka kusifiwa na Muzungu, kwamba Kenya is a democratic country in Afrika, haya sasa, mlishalikoroga itabidi tu mlinywe, na huo uchaguzi hautaisha labda Raila Odinga atangazwe mshindi vinginevyo utaendelea mpaka 2020, mpaka mpate election fatigue halafu Wakikuyu wakubali kumuachia Jaluo nchi, na hiyo itakuwa ni suicide kwa Kikuyu people, Mimi demu wangu ameshahamia Bongo kitaambo, hivyo shauri yenu!
 
Rahisi, kama ilivyo wasimamizi kwenye vituo vya kupigia kura.
Vyama viruhusiwe pia mfano NASA watoe ICT experts na Jubilee watoe ICT experts. Harafu nafasi ya chiloba wawe watu wawili mmoja awe Kalonzo na mwingine William Ruto. Hivyo ndo katiba yenu inatakiwa muidraft ili mpate uwazi mnaotaka, vinginevyo mtafilisi hiyo nchi. Methinks.
 
Si mnataka kusifiwa na Muzungu, kwamba Kenya is a democratic country in Afrika, haya sasa, mlishalikoroga itabidi tu mlinywe, na huo uchaguzi hautaisha labda Raila Odinga atangazwe mshindi vinginevyo utaendelea mpaka 2020, mpaka mpate election fatigue halafu Wakikuyu wakubali kumuachia Jaluo nchi, na hiyo itakuwa ni suicide kwa Kikuyu people, Mimi demu wangu ameshahamia Bongo kitaambo, hivyo shauri yenu!
Pumbavu zako, huelewi nchi yetu ya Kenya wewe! Sisi tunafanya yetu hatuangalii mzungu wala nini! Kwani watatoka kwao waje kupiga kura? Nyinyi tz mnang'ang'ania katiba yenyu ya jadi na dikteta wenyu ili muwafurahishe nani? Babu Zenyu, Mugabe, Museveni au nani?
 
Hapa nawaza na kuwasilisha, mahakama ya Kenya imebatilisha matokeo ya uchaguzi kwa kile ilichokitaja kuwa ukiukwaji wa katiba na tume huru ya uchaguzi. Japo mahakama iliomba muda ili itoe maelezo kamili kuhusu ilivyofikia kwenye hayo maaamuzi, hivyo kwa kifupi hadi hapo hakuna anayejua nini sababu haswa za kufutwa kwa matokeo, sote tunasubiri kwa hamu taarifa kamili.

Ninachojiuliza, hivi inawezekana tukarudia uchaguzi na ufanyike mwanzo hadi mwisho bila dosari? Ama ndio tena tutajikuta kwenye hali hii hii baada ya siku sitini zijazo. Kama Wakenya tumejiandaa vipi, maana kampeni zimeanza, hivyo inamaana tutaburuzana kwa miezi miwili ijayo, ikumbukwe pia Raila naye ameanzisha mtiti dhidi ya tume, hivyo lazima patachimbika hadi awatolee nje viongozi wa tume kama alivyofanya kwa wale wa awali.

Vipi katiba inasema nini, ama inawezekana tukarudia chaguzi mpaka basi, maana kila ikitokea dosari tutarudi hapa. Binafsi nina furaha kwa kuona mahakama zetu zimedhihirisha kuwa huru, lakini nahisi sisi wenyewe hatupo tayari kwa demokrasia ya kiwango hicho.

IEBC waachane na mambo ya electronic transmission of votes from the poling station. Turudi Manual 95%. Voter identification na transmission from the constituency tallying center ndio yafaa tu iwe electronic.
 
Akhsante sana! Niliuliza hili suala kwa kuwa hapa kwenye tume ndo kuna kiini kizima na pengine sura ya nini kinaweza kutokea!

Kwanza ifahamike kuwa wakenya (nikimaanisha wananchi wa kawaida) hawana shida na kuhusiana na haya matokeo. Hata wale tunaowaona wakifanya fujo baada ya uchaguzi kama hakuna neno kutoka kwa hawa wanaotafuta madaraka hawawezi kuonekana wakifanya lolote.

Nikirudi kwenye hoja ya kuwa nabuchaguzi salama hadi mshindi akapatikana, hilo ni suala la kuombea kila mtu kwa imani yake, tena kuomba kweli kweli!

Tayari pande mbili hizi zimeshahitilafiana kimtazamo kuhusu hii tume ya uchaguzi na mipaka! Kama tume hii haitabadilishwa, kama nasa wanavyotaka, ni dhahili matokeo yasipokuwa upande wa nasa wataendelea kulalamikia tume hii na!

Halafu kitu kingine ambacho UK alikosea ni maamuzi ya kutangaza hadharani kuwa hawataibadilisha tume kama nasa wanavyotaka! Kwa jicho la pembeni unaweza kuhisi kuna kitu hapo hata kama hicho kitu hakipo. Nahisi UK angetumia vyombo husika vinavyohusika na kuiweka tume hii madarakani kuonyesha ugumu wa suala hilo kufanyika ndani ya kipindi kifupi hicho!

Lakini kitendo cha UK ambaye ni mgombea na rais kupinga kata kata kubadili tume, tena bila kutoa sababu yoyote ya kitaalamu zaidi ya kusema tu kuwa nasa wamekuwa wakiomba kufanya mambo mengi hivyo kwa hili hawatakubali, inaweza kuonekana kama kuna kitu cha ziada!

Kingine ambacho kwa mtazamo wangu hakikuwa kitu cha kuongea sa hizi ni masuala ya NUSU MKATE. Hayakuwa mambo ya kuongea sa hz maana yanaanza kupanda mbegu mbaya mapema!

Wito wangu kwa hawa wanasiasa wanaoomba madaraka ni kuwa waangalie maslahi ya wakenya! Wapambane tu kwa hoja na mshindi apatikane kihalali ili mambo mengine yaendelee!

Unaona hata hapa jukwaani mijadala ya maendeleo imesimama sababu ya hizi siasa!.

Asante kwa mchango wako uliotulia, ni kweli kama taifa tunahitaji kuomba kwa bidii maana tupo kwenye giza na hatujui kipi kinasukwa wapi na nani.
Kikubwa ni kwamba hadi tupate taarifa kamili kutoka kwa mahakama, tutaishia kukisia na kulaumiana na kutukanana hadi mwisho.
Hadi hapo, hakuna mwenye uelewa wa ndani kuhusu vigezo vipi au nini kilipelekea mahakama kufikia hatua ya kubatilisha matokeo ya uchaguzi. Hivyo haya yote unayoyaona ni speculations tu, na kadiri mahakama inavyozidi kuchukua muda wake ndivyo Wakenya wanaendelea kugawanyika. Jazba na hasira zinaongezeka, maana upinzani umejitokeza bila kuremba maneno na kuwatukana mlengo wa serikali kwamba wao wezi, ilhali mahakama haikulaumu upande wa serikali, ilisema tu kuna kanuni za kikatiba hazikuzingatiwa na tume ya IEBC, hata bado hawajasema kwamba kuna wizi wowote ulitendeka.

Sasa nafikiri hii inapelekea mlengo wa Uhuru kujibu mapigo kwa hasira maana kumbuka anaposimama kuhutubia umati, rais Uhuru hapo anakua mwanasiasa na urais anauweka pembeni.

Tunasubiri kwa hamu taarifa ya mahakama, kumbuka jaji wawili waliokinzana na uamuzi wa hiyo mahakama walishatoa taarifa zao tena kwa kina. Wao walieleza
- Hakuna aliyewasilisha matatizo ya usajili, tofauti na ilivykua 2013
- Wapiga kura wote walitambuliwa bila matatizo wakati wa kupiga kura tofauti na ilivykua 2013
- Upigaji kura ulifanyika ndani ya muda bila dosari tena tofauti na ilivykua 2013
- Kura zilihesabiwa, kutangazwa na kuhakikiwa majimboni bila tatizo lolote tena tofauti na ilivykua 2013

Mahakama ya rufaa hapo awali ilitoa maagizo kwamba ushindi wa urais utakua kwa mujibu wa kura zinazohesabiwa majimboni, haya mengine ya upeperushaji ni ya kuremba tu na hayana uzito wowote katika kubaini mshindi.

Teknolojia ya uchaguzi bado haijafikia kiwango cha kuaminika, binafsi mimi kama mhandisi wa software, nikiri kwamba hilo haliwezi kutendeka hivi karibuni. Mifumo itadukuliwa tu, ikumbukwe hapa tunaongea kuhusu tukio la siku mbili, sio kama kwenye benki ambapo wana matawi kote na wamewekeza kwenye usalama wa mifumo yao. Kwenye uchaguzi tunazungumzia kuhusu mtumiaji wa mfumo anyeitwa Shirandula akiwa anaingiza taarifa kwenye mfumo katika kituo kinachoitwa Longiyapun kule kijijini in the middle of nowhere.

Wengi mtasema kwamba walipata darasa jinsi ya kutumia au kupeperusha taarifa, kwa mtu asiyekua na ujuzi wa jinsi ya kufanikisha mfumo ndani ya jamii anaweza kusema chochote. Mimi hapa nimezunguka EAC yote nikitoa mafunzo ya mifumo, lakini kuna maeneo mengi huwa inabidi nirudi mara zaidi ya kumi maana wanajamii pale wanachukua muda sana kuelewa.

Kumbuka pia, humo ndan ya IEBC kuna wafuasi wa NASA na wanauwezo wa kuhujumu mfumo ili uonekane una mapungufu au umedukuliwa pindi wakiona kama wanashindwa kwenye uchaguzi. Wengi mtabishia hili lakini nawaambia inawezekana tena sana.
 
Hapa nawaza na kuwasilisha, mahakama ya Kenya imebatilisha matokeo ya uchaguzi kwa kile ilichokitaja kuwa ukiukwaji wa katiba na tume huru ya uchaguzi. Japo mahakama iliomba muda ili itoe maelezo kamili kuhusu ilivyofikia kwenye hayo maaamuzi, hivyo kwa kifupi hadi hapo hakuna anayejua nini sababu haswa za kufutwa kwa matokeo, sote tunasubiri kwa hamu taarifa kamili.

Ninachojiuliza, hivi inawezekana tukarudia uchaguzi na ufanyike mwanzo hadi mwisho bila dosari? Ama ndio tena tutajikuta kwenye hali hii hii baada ya siku sitini zijazo. Kama Wakenya tumejiandaa vipi, maana kampeni zimeanza, hivyo inamaana tutaburuzana kwa miezi miwili ijayo, ikumbukwe pia Raila naye ameanzisha mtiti dhidi ya tume, hivyo lazima patachimbika hadi awatolee nje viongozi wa tume kama alivyofanya kwa wale wa awali.

Vipi katiba inasema nini, ama inawezekana tukarudia chaguzi mpaka basi, maana kila ikitokea dosari tutarudi hapa. Binafsi nina furaha kwa kuona mahakama zetu zimedhihirisha kuwa huru, lakini nahisi sisi wenyewe hatupo tayari kwa demokrasia ya kiwango hicho.
There will never be a perfect election and that's where i fault Judge Maraga's ruling.With 41000 polling stations and thousands of officials things will not go smoothly again.So are we gonna use the same excuse to nullify this and the next and the next repeat elections?
 
Back
Top Bottom