Hivi inawezekana ukamkopesha ex wako pesa na akakulipa kweli?

Hivi inawezekana ukamkopesha ex wako pesa na akakulipa kweli?

Mkuu kama unastaajabu kuona kichuguu,,,basi jua utazimia siku ukiuona mlima...

Sio Ex tu,,,kukopesha ni Risk,, labda kama mtu ameweka Bond.
 
Hivi mnawezaje wezaje kuwa na mawasiliano na ex mpaka mnafikia hatua ya kutaka kukopeshana hela

Ila kama unamkopesha fanya kama umetoa sadaka
 
Habari zenu wazee wenzangu?

Iko hivi, kuna binti mmoja alikuwa mtu wangu back then. Sasa kutokana na harakati za maisha tukajikuta tumeachana, sema toka tuachane hatukuwa na ukaribu kivile.

So toka last week ananitafuta ananiomba nimkopeshe 800k ya ada ya mwanae kakwama then mwisho wa mwezi atanirudishia.

Kiasi hicho cha pesa naweza kupambana nikakipata ila wasiwasi wangu huyu mtu atanirudishia kweli hiyo pesa au ndio itakua bad debt?

Wenye uzoefu wa kuwakopesha ma ex wenu nipeni ushauri please!

Inategemea, kama ni mstaarabu atakulipa ila kama ni mpuuzi hawezi kukulipa.

Niliwahi kumkopesha mwanamke wangu mmoja wa zamani hela, akaishia kuingia mitini na kiasi cha 1.5m.

Mimi wiki iliyopita ex wangu aliniazima 2.4m kwa makubaliano kwamba nitamlipa kwa awamu. Wiki hii nishamlipa 1.2m napanga kumalizana naye wiki ijayo.

Kwa kifupi, inategemea na mtu.
 
Back
Top Bottom