Hivi inawezekana ukamkopesha ex wako pesa na akakulipa kweli?

Mkuu kama unastaajabu kuona kichuguu,,,basi jua utazimia siku ukiuona mlima...

Sio Ex tu,,,kukopesha ni Risk,, labda kama mtu ameweka Bond.
 
Hivi mnawezaje wezaje kuwa na mawasiliano na ex mpaka mnafikia hatua ya kutaka kukopeshana hela

Ila kama unamkopesha fanya kama umetoa sadaka
 

Inategemea, kama ni mstaarabu atakulipa ila kama ni mpuuzi hawezi kukulipa.

Niliwahi kumkopesha mwanamke wangu mmoja wa zamani hela, akaishia kuingia mitini na kiasi cha 1.5m.

Mimi wiki iliyopita ex wangu aliniazima 2.4m kwa makubaliano kwamba nitamlipa kwa awamu. Wiki hii nishamlipa 1.2m napanga kumalizana naye wiki ijayo.

Kwa kifupi, inategemea na mtu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…