Hivi inawezekana ukaondoa FUSE kwenye stabilizer na bado ikandelea kuwaka na kufanya kazi?

Hivi inawezekana ukaondoa FUSE kwenye stabilizer na bado ikandelea kuwaka na kufanya kazi?

BANDOKITITA

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2022
Posts
1,484
Reaction score
2,852
Wataalamu na wafundi wa electronics, Nina stabilizer ambayo leo sijaielewa.

Hivi inawezekana ukaondoa FUSE kwenye stabilizer na bado ikandelea kuwaka na kufanya kazi au kuna tatizo. Na km ni tatizo, litakuwa tatizo gani.
 
Fuse umeiondoa wapi? kwenye circuit ya stabilizer au kwenye wire unaoenda kwenye kuingia kwenye wall/switch socket.
 
Fuse umeiondoa wapi? kwenye circuit ya stabilizer au kwenye wire unaoenda kwenye kuingia kwenye wall/switch socket.
Kwenye circuit ya stabilizer
Hcb6002629d1248b180912932cad6fceek.jpg_720x720q50.jpg
 
Maana Kuna stabilizer huwa zinafanya kazi kama UPS,inatunza umeme ambao unaweza kuwasha computer desktop, laptop na TV au ata kucharge simu
 
Kwanini uitoe?inakuzuia kufanya nini hata unataka kuitoa unahisi walioiweka walikosea na wewe ndiye mwenye akili sana au?
 
Duuuh hatari
Je kazi ya fuse unaijua??

Kwa ufupi fuse inatoa kinga , ikitokea kuna mzigo mkubwa wa umeme au hitilafu ya umeme (kwa mantiki hiyo ni hatari sana kuondoa fuse kwenye stabiliser yako)

Mwisho wa siku ukishaitoa fuse , umeme unaoingia hauwezi ukadhibitiwa , kitu ambacho kinaweza kusababisha uharibifu mkubwa wa vifaa vyako vya umeme.
 
Yaani anataka kuvuka mto bila kutumia daraja manaake anataka kupaa!!!!!
Wakati daraja Lina vipimo vyake vya kubeba mizigo ili ikitokea mzigo umekua mkubwa daraja lazima livunjike/likatike ili kupunguza madhara makubwa
 
Hivi inawezekana ukaondoa FUSE kwenye stabilizer na bado ikandelea kuwaka na kufanya kazi au kuna tatizo

Voltage stabilizer safety device​

The voltage stabilizer below 3KVA (such as ATO 500VA stabilizer for home) uses a fuse for overload or short circuit protection, and the AC voltage stabilizer above 5KVA uses a small circuit breaker or a small air switch for overload or short circuit protection.

Wataalamu na wafundi wa electronics, Nina stabilizer ambayo leo sijaielewa.

Hivi inawezekana ukaondoa FUSE kwenye stabilizer na bado ikandelea kuwaka na kufanya kazi au kuna tatizo. Na km ni tatizo, litakuwa tatizo gani.
Hiyo stabiliser umeiona ina viashiria gani vya tatizo, usaidiwe.

Na kama fuse imeungua unaweza kubadilisha, lakini kama tatizo linaendelea kuwepo huenda kuna malfunction ya baadhi ya components za circuit ya stabiliser yako.

Unaweza kumpelekea fundi kwa usaidizi wa ziada , kuepuka madhara yanayoweza kutokea kama vile moto.
 
Asante, ila fuse ni nzima na ndiyo maan hata mimi nashagaa kwa nini inawaka direct bila kupita kwenye fuse
 
Kwanini uitoe?inakuzuia kufanya nini hata unataka kuitoa unahisi walioiweka walikosea na wewe ndiye mwenye akili sana au?
Nilitoa baada ya kuhisi imeungua baada ya kuona umeme unapungua nguvu lakini stabilizer haitoi sauti yoyote kuashiria kustabilize voltage ya umeme km ilivyo kawaida. Ndipo nikaona ikiendelea kuwaka hata baada ya kuchomoa FUSE.
 
Back
Top Bottom