Hivi inawezekana wananchi tukajulishwa vyanzo vyote vya mapato na kiasi gani tunapata kwa mwezi?

Pantosha

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2022
Posts
640
Reaction score
958
Tumekuwa tukisomewa budget za wizara zote ila sina kumbukumbu kama wananchi tuliwahi kujulishwa vyanzo vyote vya mapato na kiasi kinachopatikana kwenye kila chanzo kwa mwezi au mwaka.

Usikute tunaenda kuomba misaada au kuingia madeni na wakati tunajitosheleza.

Hizi taarifa zinapatikana wapi wadau? Hii itatusaidia kupanga pia matumizi.

Ninachokiwa jamani! Nimechoka kukosa miundombinu mizuri. Hadi naanza kuwaza hivi.
 
Tumekuwa tukisomewa budget za wizara zote ila sina kumbukumbu kama wananchi tuliwahi kujulishwa vyanzo vyote vya mapato na kiasi kinachopatikana kwenye kila chanzo kwa mwezi au mwaka...
Hakuna haja nilitegemea Wananchi mngeandamana kudai MAFISADI wa MAPATO yenu WANAUAWA
 
Tumekuwa tukisomewa budget za wizara zote ila sina kumbukumbu kama wananchi tuliwahi kujulishwa vyanzo vyote vya mapato na kiasi kinachopatikana kwenye kila chanzo kwa mwezi au mwaka...
TRA Huwa inawatoa zile taarifa za robo zikiwakilisha Mapato ya Kila mwezi.

Pili Kuna ishu ya Halmashauri,zamani walikuwa wanasoma Mapato ila saizi Wizara haitoi hizo taarifa tena.

Tatu, Serikali Ina taasisi nyingi sana zinazokusanya Mapato , wengine wanatoa wengine hawatoi.

Mwisho saizi Bunge la Bajeti linaendelea ,ndio pale Kuna Mapato na matumizi ya Nchi yote Utajua vyanzo na matumizi yake.
 
Labda nifuatilie Bunge nipate taarifa. Ila point tatu za kwanza hazijitoshelezi.
 
Hazijajitosheleza kivipi? Hata huko kwenye Bunge hutojua maana utaoewa gross revenues na expenditures tuu.
Si umesema kuna wanaotoa taarifa na wengine hawatoi. Sasa hapo imejitosheleza hiyo?
Hizi taarifa ni muhimu sana.
 
Labda nifuatilie Bunge nipate taarifa. Ila point tatu za kwanza hazijitoshelezi.
Mkuu umejuaje hazijitoshelezi wakati umeuliza kujua, unajuzwa unasema hazijitoshelezi, unasanifu watu au??
 
Si umesema kuna wanaotoa taarifa na wengine hawatoi. Sasa hapo imejitosheleza hiyo?
Hizi taarifa ni muhimu sana.
Taarifa karibu wote wanatoa ila hawatoi Kwa utaratibu sawa wa monthly au robo mwaka.
 
Chanzo kikubwa cha mapato ni kunyonya wananchi na mikopo kausha damu,na 90% ya mapato yanaishia kuhudumia mafisadi.
 
Back
Top Bottom