Hivi ingekuaje kama Wilaya au Mikoa ingepewa uwezo wa kusaka wawekezaji toka nje?

Hivi ingekuaje kama Wilaya au Mikoa ingepewa uwezo wa kusaka wawekezaji toka nje?

Red Giant

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2012
Posts
15,657
Reaction score
20,967
Habari wakuu.

Hivi ingekuwaje iwapo halmashauri za wilaya a mikoa ingepewa ruhusa ya kusaka wawekezaji popote duniani, kwa kujitangaza na kuwapa incentives zilizopo katika maeneo yao kama ardhi, kuwapelekea maji na kuwachongea barabara?

Mfano labda wilaya ya Mbinga itangaze kuwa inahitaji muwekezaji wa kiwanda cha kahawa, itampa ardhi bure ya kujenga kiwanda, itampelekea maji, iitachonga barabara, na kupeleka umeme hapo kiwandani. Chato wafanye hivyo kwa kiwanda cha samaki. Huko liwale wafanye hivyo kwa korosho. Singida nao kwa viwanda vya mafuta nk.

linaweza chochea maendeleo?
 
Ndio, maendeleo yatazidi. Changamoto kubwa katika kulifanikisha hili ni serikali kuu kuhodhi madaraka. Hili litawezekana tukigatua madaraka kwenda mikoani na wilayani.

Hivi sasa nafasi ya serikali za wilaya na mikoa kwenye uwekezaji ni ndogo. Turudishe maamuzi mashinani. Serikali za Mitaa -mikoa na wilaya- ziwe na uwezo wa kuweka strategic plans zao. Naamini, watu walio wilayani wanajua hali na mahitaji yao vizuri zaidi kuliko watu wa Wizara ya Fedha na Mipango. Mipango hii iwe aligned na mipango ya taifa.
 
MAENEO Mengine yatakuwa nyuma kimaendeleo kwa kuwa viongozi wao watakosa mbinu za kuwapata wawekezaji katika maeneo yao
 
Lindi mngeongoza kwenye Uwekezaji wa ULOZI
 
MAENEO Mengine yatakuwa nyuma kimaendeleo kwa kuwa viongozi wao watakosa mbinu za kuwapata wawekezaji katika maeneo yao
Obviously, maendeleo hayawezi kuwa sawa. Ila hoja ya kukosa viongozi hapana. Nchi hii ina wasomi wengi tu. Kugatua madaraka hakumaanishi kuwa nafasi za uongozi na watendaji zitakuwa kwa kabila au watu waliozaliwa eneo hilo tu! Nafasi za hawa matechnocrats kwenye kada mbalimbali zitatangazwa na kila Mtanzania atakuwa na haki ya kuomba na kufanya kazi.
 
MAENEO Mengine yatakuwa nyuma kimaendeleo kwa kuwa viongozi wao watakosa mbinu za kuwapata wawekezaji katika maeneo yao
Nilisoma pahala kuhusu Las Vegas Moja ya vitu vilivyo influence ni pamoja na uwekezaji kwenyema-casino
Nadhani kuna kitu cha kujifunza though hilo jiji laweza lisifanane na jiji jingine kimaendeleo
 
Hicho ndicho kilipaswa kuwa kipimo cha madiwani na mabaraza yao, ila kwa hii tabia ya outshining your master si rahisi may be arumeru ya chadema imoutshine kongwa ya ccm in terms of investment attracting strategies 😝😝
 
Kuna baadhi ya mikoa ingepata nguvu kubwa kiuchumi na kuwa na ushawishi kwenye nchi. Hili suala ni jambo la muda tu kwani ugomvi ungekuwa nje nje, unaonewa na Mr.Flani kwakuwa katokea kwenye royal family yaani wengine wangesiginiwa ardhini
 
Nilisoma pahala kuhusu Las Vegas Moja ya vitu vilivyo influence ni pamoja na uwekezaji kwenyema-casino
Nadhani kuna kitu cha kujifunza though hilo jiji laweza lisifanane na jiji jingine kimaendeleo
Jangwa kabisa. meya na baraza lake wakakaa wakawazua. wakaona fursa kwenye kamari. leo hii jiji kubwa na lina uchumi mkubwa balaa. kama mdau alivyosema huko juu. ikifanya ugatuzi watu wataumiza kichwa kutatua shida zao.
 
Kuna baadhi ya mikoa ingepata nguvu kubwa kiuchumi na kuwa na ushawishi kwenye nchi. Hili suala ni jambo la muda tu kwani ugomvi ungekuwa nje nje, unaonewa na Mr.Flani kwakuwa katokea kwenye royal family yaani wengine wangesiginiwa ardhini
Mikoa siyo kitu cha maana wala cha kudumu. inaweza gawanya na kupinduliwa pinduliwa muda wowote. maendeleo ndiyo jambo la msingi.
 
Kuna baadhi ya mikoa ingepata nguvu kubwa kiuchumi na kuwa na ushawishi kwenye nchi. Hili suala ni jambo la muda tu kwani ugomvi ungekuwa nje nje, unaonewa na Mr.Flani kwakuwa katokea kwenye royal family yaani wengine wangesiginiwa ardhini
Devolution "ugatuzi" na federalism "shirikisho" ni vitu tofauti. Tanzania sio shirikisho. Hatuna sababu ya kuwa shirikisho.

Devolution ilishaanza kutekelezwa nchini. Kwenye elimu na afya baadhi ya maamuzi yanafanyika katika halmashauri. Tatizo kubwa ni sera na kasi ya kuzipa serikali za mitaa haya mamlaka. Vitu vingi bado, ambavyo maamuzi yangetoka wilayani ama mkoani yanasubiri serikali kuu.
 
Samahani wajumbe! Labda mimi ntakuwa nimeachwa nyuma na kasi ya nchi.

Kwani ni lini halmashauri za wilaya na serikali za mikoa zilikatazwa kutafuta wawekezaji ndani na je ya nchi, ikiwemo kujitangaza?

Mimi nilikuwa nadhani wanaruhusiwa kufanya hivyo, na wakiishawapata basi wanafuata taratibu za nchi ikiwemo kupitia katika kituo cha uwekezaji (TIC), kwa taratibu zingine.

Nafikiri kinachofanyika hapa Tanzania, ni kwa baadhi ya viongozi wa wilaya na mikoa hawataki kujishughulisha zaidi katika kuwasaka wawekezaji, wa ndani na nje.

Kwa mfano, karibu halmashauri nyingi na mikoa, ina tovuti (website), na kuna mambo mbalimbali yamepostiwa humo. Hivyo, hata hizo website wanaweza kuzitumia kuutangaza mkoa au wilaya na fursa zake. Sidhani kama wakifanya hivyo wataadhibiwa na ngazi za juu.

Miezi ya michache iliyopita kulikuwa na uzinduzi wa kitabu cha mwongozo wa uwekezaji, kwa baadhi ya mikoa ikiwemo Tabora, ambao fursa mbalimbali za mkoa huo zimeainiishwa. Mwongozo huu umeandaliwa na UNDP ikishirikiana na serikali.

Pia, tusisahau wabunge wanatakiwa watafute wawekezaji ndani na nje ya nchi, na kuwapeleka katika majimbo yao, hakuna atakayekasirika.

Hata mwananchi akiingia mtandaoni akapata mwekezaji, ruksa kumpeleka kijijini kwao, ila atafuata taratibu za nchi.
 
Tujaribu kutembelea websites za halmashauri tuone kilichopostiwa. Zipo halmashauri zimepost mambo ya kiuchumi, na zingine zimepost taarifa za kiutawala zaidi. Zingine zina habari za mwaka 2020.

Pi, zipo halmashauri zina social media mfano facebook.

Mtandao wa internet ni njia rahisi ya kujitangaza duniani. Tujiulize, je mikoa na halmashauri haziruhusiwi kutumia tovuti zao kujitangaza na kutafuta wawekezaji? au ni kukosa ubunifu?
 
Kujitangaza na uwezo wa kufanya maamuzi ni vitu tofauti. Devolution bado ni work im progress kwetu.

Mfano, tunaweza decentralise baadhi ya vitu katika mchakato mzima wa kuwekeza. Kuwekeza ni zaidi ya matangazo.
 
Binafsi naona hoja Ina mashiko lakini inatekelezeka kama tungekuwa na serikali za majimbo. Hizi zingekuwa autonomous na zingekuwa na sheria zake ambazo haziingiliani na Sheria za Jamhuri.

Suala la kwamba kuna maeneo yangekuwa hayana maendeleo nadhani halina mashiko sababu hao ambao wanheona hakuna maendeleo wangehamia kwenye maendeleo.

Leo hii watu wanatoka vijijini kuka mjini kwa sababu gani? So wangebaki huko?

Tanzania ni kubwa sana na ndio maana hatuwezi kuendelea, mtu anakaa maporini anaacha kukaa sehemu ambayo kuna mkusanyiko wa jamii ili serikali iwapelekee huduma kirahisi unashangaa mtu kajipeleka milimani halafu anaanza kulaumu serikali haipeleki maji na umeme, hospital etc.

Kiukweli ni ngumu sana, kuna watu wanaishi kwenye mapori huko Katavi aisee mpaka unashangaa kwanini? Serikali itawezaje kuwaletea huduma za kijamii na ingali wapo jamii ndogo tu na hawataki kukaa kwenye vijiji ambavyo itakuwa rahisi kupeleka huduma?

Hoja hii ya msingi sana. As long Tanzania ni moja basi watu wawe huru kuhamia maeneo ambayo yataonekana yameendelea kulingana na mapenzi ya mtu mwenyewe.
 
Imekaa vizuri sana ingeondoa baadhi ya maeneo kufaidika kwa rasilimali za maeneo mengine, pia ingeongeza ushindani na ubunifu kuhakikisha local resources zinatumika kusisimua maendeleo nadhani hata ingechangia kupunguza changamoto za ajira,uchumi na huduma za jamii
 
Samahani wajumbe! Labda mimi ntakuwa nimeachwa nyuma na kasi ya nchi.

Kwani ni lini halmashauri za wilaya na serikali za mikoa zilikatazwa kutafuta wawekezaji ndani na je ya nchi, ikiwemo kujitangaza?

Mimi nilikuwa nadhani wanaruhusiwa kufanya hivyo, na wakiishawapata basi wanafuata taratibu za nchi ikiwemo kupitia katika kituo cha uwekezaji (TIC), kwa taratibu zingine.

Nafikiri kinachofanyika hapa Tanzania, ni kwa baadhi ya viongozi wa wilaya na mikoa hawataki kujishughulisha zaidi katika kuwasaka wawekezaji, wa ndani na nje.

Kwa mfano, karibu halmashauri nyingi na mikoa, ina tovuti (website), na kuna mambo mbalimbali yamepostiwa humo. Hivyo, hata hizo website wanaweza kuzitumia kuutangaza mkoa au wilaya na fursa zake. Sidhani kama wakifanya hivyo wataadhibiwa na ngazi za juu.

Miezi ya michache iliyopita kulikuwa na uzinduzi wa kitabu cha mwongozo wa uwekezaji, kwa baadhi ya mikoa ikiwemo Tabora, ambao fursa mbalimbali za mkoa huo zimeainiishwa. Mwongozo huu umeandaliwa na UNDP ikishirikiana na serikali.

Pia, tusisahau wabunge wanatakiwa watafute wawekezaji ndani na nje ya nchi, na kuwapeleka katika majimbo yao, hakuna atakayekasirika.

Hata mwananchi akiingia mtandaoni akapata mwekezaji, ruksa kumpeleka kijijini kwao, ila atafuata taratibu za nchi.
Alichokiongelea mleta mada ni kwamba huyo muwekezaji awe chini ya wilaya na sio nchi, kwamba makubaliano yataingiwa kati ya muwekezaji na Halmashauri kwa mkataba wa Kupewa masharti ya kutengeneza miundombinu ya wilaya husika na yeye muwekezaji Kupewa Uhuru wa kutumia ardhi bure kwa muda flani
 
Habari wakuu.

Hivi ingekuwaje iwapo halmashauri za wilaya a mikoa ingepewa ruhusa ya kusaka wawekezaji popote duniani, kwa kujitangaza na kuwapa incentives zilizopo katika maeneo yao kama ardhi, kuwapelekea maji na kuwachongea barabara?

Mfano labda wilaya ya Mbinga itangaze kuwa inahitaji muwekezaji wa kiwanda cha kahawa, itampa ardhi bure ya kujenga kiwanda, itampelekea maji, iitachonga barabara, na kupeleka umeme hapo kiwandani. Chato wafanye hivyo kwa kiwanda cha samaki. Huko liwale wafanye hivyo kwa korosho. Singida nao kwa viwanda vya mafuta nk.

linaweza chochea maendeleo?

Kikubwa ni uchumi utakufa na nchi itakua flooded na foreign reserves! hakutakua na uwiano kati ya uchumi wa nchi na wananchi wenyewe japokua kwenye karatasi kutaonekana mambo yanaenda vizuri, yule mkulima wa kawaida itambidi afanye juu chini kulevel
 
Back
Top Bottom