Obviously, maendeleo hayawezi kuwa sawa. Ila hoja ya kukosa viongozi hapana. Nchi hii ina wasomi wengi tu. Kugatua madaraka hakumaanishi kuwa nafasi za uongozi na watendaji zitakuwa kwa kabila au watu waliozaliwa eneo hilo tu! Nafasi za hawa matechnocrats kwenye kada mbalimbali zitatangazwa na kila Mtanzania atakuwa na haki ya kuomba na kufanya kazi.MAENEO Mengine yatakuwa nyuma kimaendeleo kwa kuwa viongozi wao watakosa mbinu za kuwapata wawekezaji katika maeneo yao
Nilisoma pahala kuhusu Las Vegas Moja ya vitu vilivyo influence ni pamoja na uwekezaji kwenyema-casinoMAENEO Mengine yatakuwa nyuma kimaendeleo kwa kuwa viongozi wao watakosa mbinu za kuwapata wawekezaji katika maeneo yao
Jangwa kabisa. meya na baraza lake wakakaa wakawazua. wakaona fursa kwenye kamari. leo hii jiji kubwa na lina uchumi mkubwa balaa. kama mdau alivyosema huko juu. ikifanya ugatuzi watu wataumiza kichwa kutatua shida zao.Nilisoma pahala kuhusu Las Vegas Moja ya vitu vilivyo influence ni pamoja na uwekezaji kwenyema-casino
Nadhani kuna kitu cha kujifunza though hilo jiji laweza lisifanane na jiji jingine kimaendeleo
Mikoa siyo kitu cha maana wala cha kudumu. inaweza gawanya na kupinduliwa pinduliwa muda wowote. maendeleo ndiyo jambo la msingi.Kuna baadhi ya mikoa ingepata nguvu kubwa kiuchumi na kuwa na ushawishi kwenye nchi. Hili suala ni jambo la muda tu kwani ugomvi ungekuwa nje nje, unaonewa na Mr.Flani kwakuwa katokea kwenye royal family yaani wengine wangesiginiwa ardhini
Devolution "ugatuzi" na federalism "shirikisho" ni vitu tofauti. Tanzania sio shirikisho. Hatuna sababu ya kuwa shirikisho.Kuna baadhi ya mikoa ingepata nguvu kubwa kiuchumi na kuwa na ushawishi kwenye nchi. Hili suala ni jambo la muda tu kwani ugomvi ungekuwa nje nje, unaonewa na Mr.Flani kwakuwa katokea kwenye royal family yaani wengine wangesiginiwa ardhini
Alichokiongelea mleta mada ni kwamba huyo muwekezaji awe chini ya wilaya na sio nchi, kwamba makubaliano yataingiwa kati ya muwekezaji na Halmashauri kwa mkataba wa Kupewa masharti ya kutengeneza miundombinu ya wilaya husika na yeye muwekezaji Kupewa Uhuru wa kutumia ardhi bure kwa muda flaniSamahani wajumbe! Labda mimi ntakuwa nimeachwa nyuma na kasi ya nchi.
Kwani ni lini halmashauri za wilaya na serikali za mikoa zilikatazwa kutafuta wawekezaji ndani na je ya nchi, ikiwemo kujitangaza?
Mimi nilikuwa nadhani wanaruhusiwa kufanya hivyo, na wakiishawapata basi wanafuata taratibu za nchi ikiwemo kupitia katika kituo cha uwekezaji (TIC), kwa taratibu zingine.
Nafikiri kinachofanyika hapa Tanzania, ni kwa baadhi ya viongozi wa wilaya na mikoa hawataki kujishughulisha zaidi katika kuwasaka wawekezaji, wa ndani na nje.
Kwa mfano, karibu halmashauri nyingi na mikoa, ina tovuti (website), na kuna mambo mbalimbali yamepostiwa humo. Hivyo, hata hizo website wanaweza kuzitumia kuutangaza mkoa au wilaya na fursa zake. Sidhani kama wakifanya hivyo wataadhibiwa na ngazi za juu.
Miezi ya michache iliyopita kulikuwa na uzinduzi wa kitabu cha mwongozo wa uwekezaji, kwa baadhi ya mikoa ikiwemo Tabora, ambao fursa mbalimbali za mkoa huo zimeainiishwa. Mwongozo huu umeandaliwa na UNDP ikishirikiana na serikali.
Pia, tusisahau wabunge wanatakiwa watafute wawekezaji ndani na nje ya nchi, na kuwapeleka katika majimbo yao, hakuna atakayekasirika.
Hata mwananchi akiingia mtandaoni akapata mwekezaji, ruksa kumpeleka kijijini kwao, ila atafuata taratibu za nchi.
Habari wakuu.
Hivi ingekuwaje iwapo halmashauri za wilaya a mikoa ingepewa ruhusa ya kusaka wawekezaji popote duniani, kwa kujitangaza na kuwapa incentives zilizopo katika maeneo yao kama ardhi, kuwapelekea maji na kuwachongea barabara?
Mfano labda wilaya ya Mbinga itangaze kuwa inahitaji muwekezaji wa kiwanda cha kahawa, itampa ardhi bure ya kujenga kiwanda, itampelekea maji, iitachonga barabara, na kupeleka umeme hapo kiwandani. Chato wafanye hivyo kwa kiwanda cha samaki. Huko liwale wafanye hivyo kwa korosho. Singida nao kwa viwanda vya mafuta nk.
linaweza chochea maendeleo?