Kwa makadirio ni kama ifuatavyo:
1. Pc yenye uwezo kwa bei za kariakoo ni 2m
2. Monitor speakers za yamaha (hs 8) ni 2.4m na mkononi ni 1.8m
3. Sound card /audio interface ya njia mbili ndani na nne nje ni laki saba hadi tisa kulingana na brand kama focusrite, avid, m audio, presonus, behringer na kadhalika.
4. Microphone: kwa hapa dar nisikudanganye tu mkuu ukienda kariakoo utakuta hizi mic za mchina kama turkstar zimejaa kuanzia laki tatu ila sikushauri ununue. Mic nzuri ni ile ambayo bei zake zipo kuanzia laki nane au uipate kutoka kwa mtu. Kama utapata audio technica at 2020 itafaa sana na kuna siku niliwahi kuiona huko kariakoo duka la congo music shop
5. Midi keyboard controller huanzia laki tano na nusu kulingana na aina ya midi controller unayoitaka, kuna za keys 49, 61 hadi 88 na pia huwa zinakuwa semi weighted au full velocity.
6. Software kwa ajili ya productions pamoja na audio samples. Hizi ndio silaha za maangamizi kwenye production na sio rahisi sana kuzipata. Huwa mtu anakufanyia installation kwa package ya laki tatu kwa plugin za kawaida au laki 8 kwa full package ya world class samplers, synthesizers na plugins za mixing na Mastering.
7. Cables, stands na accessories: hizi mara nyingi huwa bei rahisi na huweza kufika laki sita kulingana na quality yake.
8. DIY Acoustics treatment: hii mara nyingi hutegemea na aina ya chumba utakachofanya kuwa studio na mimi binafsi nashauri uwekeze kwenye zile movable panels ambazo ukutaka kuhama ni rahisi kuzitoa na gharama zake ni approximately laki sita kwa chumba cha wastani.
9. Furniture: utahitaji kiti na meza kwa ajili ya prodicer, sofa set kwa ajili ya wageni na wateja na carpet
10. Air conditioner; kwa kawaida unahitaji a/c ya 9,000 btu/hr au 12,000 btu/hr kama chumba kitakuwa kikubwa kiasi