Hivi January Makamba na Nape wamechukua form za ubunge kweli?

Nape alichukua na anagombea kwa mujibu wa post yake Twitter ya tarehe 1/07/25
Screenshot_20250703_050217_X.jpg
 
Mwenye busara hawezi kujihusisha kugombania ubunge kwa Mfumo uliopo

MFUMO hauna ulinzi wa haki

Maamuzi ya mtu ndiyo yenye haki rejea kauli aliopewa Mbunge wa Taifa Mpina Mwanza ndiyo utanielewa
Lakini na yeye wanachama wamemuonyesha kama mpina anafaa kuwa mbunge wao maana sijaona mwanachama mwingine kisesa kachukuwa fomu zaidi yake kama sijakosea
 
Hawa watu wawili sijaona wala kusikia kama wametia nia ya kutetea nafasi zao za ubunge kwa kuchukua form.
Kuna mwenye kujua lolote?
Kwani hawa wapuuzi bado wanaishi, mi nilifikiri walishatekwa na kupotezwa na chama chao. Wapotee tu, hatuwataki hata kuwasikia na kuwaona.
 
kwani watashinda?
Wanaweza kkushinda maana tabia ya wananchi kuchagua wabunge kwa msingi wa umaarufu badala ya sifa stahiki.”
Ni wazi kuwa katika historia ya siasa yetu, tumeona wabunge wasiokuwa na sifa au uwezo wa kutosha kushinda chaguzi si kwa sababu ya sera au uwezo wao, bali kutokana na umaarufu wao au mtandao wa chama. Hii ni hatari kwa ustawi wa taifa.
Kipimo halisi cha welevu wa wapiga kura ni aina ya viongozi wanaowachagua kuwa wawakilishi wao. Kama wapiga kura wataendelea kuchagua viongozi kwa misingi ya kijinafsi, kijamii au kisiasa badala ya sifa, maadili, na uwezo wa kuleta maendeleo basi hatuwezi kulalamikia ubora mdogo wa Bunge letu.
Tatizo hili lina mizizi ya kisaikolojia pia. Wapiga kura wengi hujihisi hawana nguvu ya mabadiliko, hasa pale wanapodhani kuwa chama fulani kikimpitisha mgombea wake, basi huyo lazima ashinde. Hali hii ya kutojitokeza kupiga kura kwa kutoamini kura zao zina nguvu ni mojawapo ya matatizo yanayowezesha viongozi wasiostahili kushinda.
Lakini historia imetuonyesha kuwa wakati wananchi wanaposimama kidete na kujitokeza kwa wingi kupiga kura, na kuchagua kwa uelewa si kwa utashi wa chama viongozi wenye maono na weledi waliweza kushinda. Hii ndiyo ilivyokuwa nyakati zile ambapo watu walilinda na kulinda kura zao kwa dhati. Ndipo ilipowezekana kuingiza bungeni wabunge wenye nia ya dhati ya kuwatumikia wananchi.
Hivyo basi, suluhisho liko mikononi mwa wapiga kura wenyewe: waondoe woga, waachane na fikra za "lazima chama fulani washinde," wajitokeze kwa wingi, waamue kwa akili na si kwa mazoea.
 
Angalau nyakati zile Kura zilikuwa na chembechembe za nguvu ya kuamua Nani awe kiongozi, lakini alipoingia Yule Mzee,aliyesema hadharani kwamba "...haiwezekani mkurugenzi,nimekuteua,nakulipa mshahara, halafu umtangaze mpinzani kuwa mshindi, hiiiiiii, nitarara nawewe mbere..."
Ukiichukua kauli hii, na Kasi ya watu KUPOTEZWA au KUUAWA, iliwaachia wananchi haki ya kupiga Kura pekee,lakini haki ya kuamua nani awe kiongozi ilizikwa rasmi.

Na CCM walipoona kumbe inawezekana kuwaachia wananchi haki ya kupiga Kura,lakini si kuchagua kiongozi, fursa hiyo wanaendelea kuitumia hata baada ya mwasisi kurudi mavumbini.

Na ili kuondokana na haya ya sasa, ni mpaka wananchi watakapoacha kuogopa RISASI NA MAGEREZA,na watawala Kilosa nyenzo ya kuwatishia wenye nchi,hapo watakua wenye nidhami kwa wananchi wanaowaongoza.

Japo, watawala nasikia Raha Sana kuogopwa na wapiga kura, badala ya wao kuwaogopa wapiga Kura wao!
 
Hawa watu wawili sijaona wala kusikia kama wametia nia ya kutetea nafasi zao za ubunge kwa kuchukua form.
Kuna mwenye kujua lolote?
Wataacha ili wafanye kazi gani mtaani?
 
Bila shaka wamechukua labda camera walizikwepa , mfumo uliwakataa hapo awali .

Namuona January Makamba akiwa siti ya mbele kuwa PM.

Now amepikwa na kuwa kimyaa na vumbi lake litaanza rasmi kwenye mbio za kampeni akiwa mstari wa mbele katika muungano wa ushindi kuelekea Oktoba 2025.
 
Mwenye busara hawezi kujihusisha kugombania ubunge kwa Mfumo uliopo

MFUMO hauna ulinzi wa haki

Maamuzi ya mtu ndiyo yenye haki rejea kauli aliopewa Mbunge wa Taifa Mpina Mwanza ndiyo utanielewa
Kila mtu ana haki sawa wewe umekata tamaa unajua hata ukiwelkwa n mende utashindwa
 
Hilo bunge la kina Mwijaku, Baba Levo, DJ Rommy Jones, Tale-Tale, Mkojani, Gabo nk. Hili ni bunge la Kizimkazi.
Kwani hao kina Mwijaku wamevunja sheria gani kutaka kuwa wabunge? Naona tunawananga sana ila wanatekeleza haki yao ya kikatiba. Hata wakishinda pia ni sawa.
Kama tunataka demokrasia ya kweli lazima tukubaliane na side effects zake.
Changamoto pekee inaweza kuwa mfumo wa uchaguzi na sio wagombea.
Maana hata wewe mwenye akili una haki ya kutangaza nia, kugombea na kuchaguliwa.
 
Ummy Mwalimu a.k.a Odo naye vipi huko Tanga?

Prof. Palamagamba Kabudi a.k.a Jalala kachukua fomu huko Kilosa?

N.B. Huyu mgeni mbona anawanyanyasa wenyeji?
 
Unawatakia nini vilaza hawa, si bora hata hizo form zingechukuliwa na Lulu Diva au Wema maana wao japo hawatachangia chochote lakini watagawa uroda tu kwa wabunge wenzao na kuambukizana kale kagonjwa ketu.
🤣😂😂
 
Ummy Mwalimu a.k.a Odo naye vipi huko Tanga?

Prof. Palamagamba Kabudi a.k.a Jalala kachukua fomu huko Kilosa?

N.B. Huyu mgeni mbona anawanyanyasa wenyeji?
Ummy mwalimu amechukua fomu.
 
Back
Top Bottom