Hivi January Makamba na Nape wamechukua form za ubunge kweli?

Hivi January Makamba na Nape wamechukua form za ubunge kweli?

Ubunge sio kazi ya heshima tena , na hii ni kutokana na kuwapeleka Dodoma wasanii kila mara , wamepazoea Sana Dodoma na wanapaona rahisi kuishi
Baada ya ccm kupoteza mvuto hasa kwa vijana, imebidi wajishikize kwa wasanii, wakiamini wakiwa na wasanii wengi watawasaidia kupata uungwaji mkono na kundi la vijana.
 
Wasanii wanaitwa kuhamasisha katika shughuli za serikali kutokana na wananchi kukosa mvuto na uongozi sasa wasanii wameamua kuwa sehemu ya serikali.
Hivyo Unaniaminisha Kuwa Nitarajie Kuona Maigizo na Vichekesho zaidi Serikal Ijayo?
 
Hawa watu wawili sijaona wala kusikia kama wametia nia ya kutetea nafasi zao za ubunge kwa kuchukua form.
Kuna mwenye kujua lolote?
Wazee wa kuchungulia wale- upepo haupo sawa huu, ishi kwa akili za kuzaliwa.
 
Hawa watu wawili sijaona wala kusikia kama wametia nia ya kutetea nafasi zao za ubunge kwa kuchukua form.
Kuna mwenye kujua lolote?
January kachukua na akamzingua mpinzani wake eti asiongee na vyombo vya habari na wala asikusanyike maeneo Yale ya ofisi maana si Kilindi cha kampeni,naye akazinguliwa
 
Wanaweza kkushinda maana tabia ya wananchi kuchagua wabunge kwa msingi wa umaarufu badala ya sifa stahiki.”
Ni wazi kuwa katika historia ya siasa yetu, tumeona wabunge wasiokuwa na sifa au uwezo wa kutosha kushinda chaguzi si kwa sababu ya sera au uwezo wao, bali kutokana na umaarufu wao au mtandao wa chama. Hii ni hatari kwa ustawi wa taifa.
Kipimo halisi cha welevu wa wapiga kura ni aina ya viongozi wanaowachagua kuwa wawakilishi wao. Kama wapiga kura wataendelea kuchagua viongozi kwa misingi ya kijinafsi, kijamii au kisiasa badala ya sifa, maadili, na uwezo wa kuleta maendeleo basi hatuwezi kulalamikia ubora mdogo wa Bunge letu.
Tatizo hili lina mizizi ya kisaikolojia pia. Wapiga kura wengi hujihisi hawana nguvu ya mabadiliko, hasa pale wanapodhani kuwa chama fulani kikimpitisha mgombea wake, basi huyo lazima ashinde. Hali hii ya kutojitokeza kupiga kura kwa kutoamini kura zao zina nguvu ni mojawapo ya matatizo yanayowezesha viongozi wasiostahili kushinda.
Lakini historia imetuonyesha kuwa wakati wananchi wanaposimama kidete na kujitokeza kwa wingi kupiga kura, na kuchagua kwa uelewa si kwa utashi wa chama viongozi wenye maono na weledi waliweza kushinda. Hii ndiyo ilivyokuwa nyakati zile ambapo watu walilinda na kulinda kura zao kwa dhati. Ndipo ilipowezekana kuingiza bungeni wabunge wenye nia ya dhati ya kuwatumikia wananchi.
Hivyo basi, suluhisho liko mikononi mwa wapiga kura wenyewe: waondoe woga, waachane na fikra za "lazima chama fulani washinde," wajitokeze kwa wingi, waamue kwa akili na si kwa mazoea.
Unaongea nadharia mkuu. Kwa sasa toka ccm ikutane na dhoruba la 2015, haiko tayari tena kuheshimu matokeo katika box la kura. Hivyo washindi wanapatikana kwa maagizo toka juu. Na hakuna popote utakwenda, kwani hata mahakamani tayari wameshaagizwa nini wafanye. Na tatizo hili kwa sehemu kubwa lilipandikizwa chini ya utawala wa Magufuli. Na hakuna uwezekano hali hiyo kubadilika bila machafuko ama mapinduzi ya kijeshi.
 
Unaongea nadharia mkuu. Kwa sasa toka ccm ikutane na dhoruba la 2015, haiko tayari tena kuheshimu matokeo katika box la kura. Hivyo washindi wanapatikana kwa maagizo toka juu. Na hakuna popote utakwenda, kwani hata mahakamani tayari wameshaagizwa nini wafanye. Na tatizo hili kwa sehemu kubwa lilipandikizwa chini ya utawala wa Magufuli. Na hakuna uwezekano hali hiyo kubadilika bila machafuko ama mapinduzi ya kijeshi.
Ni kweli kabisa niliyosema yaweza kuonekana kama nadharia, hasa tukitazama hali halisi ya kisiasa ilivyo sasa, ambapo ushindani wa kweli kwenye sanduku la kura unaonekana kufifia kutokana na muingiliano wa mamlaka na mfumo usio huru. Hata hivyo, hoja yangu inalenga mizizi ya tatizo: utamaduni wa kupima wagombea kwa umaarufu badala ya sifa.
Hata kama ushindi hautolewi kwa haki, bado mwelekeo wa fikra za wananchi una athari kubwa kwenye mchakato wa kisiasa wa muda mrefu. Ni kupitia mabadiliko ya mitazamo ya wapiga kura ndipo hata tawala kandamizi huanza kuyumba si lazima kwa mapinduzi ya kijeshi, ambayo kwa Tanzania ni magumu sana kutokana na historia, muundo wa kijeshi na utamaduni wa heshima kwa mamlaka.
Kilicho na nafasi zaidi ni mapinduzi ya kiraia yaani mabadiliko ya kifikra, uelewa, na mwamko wa wananchi katika kushiriki mchakato wa kura na kuwawajibisha viongozi kwa njia za amani na sheria.
Kwa hiyo hoja yangu inasimama pale ambapo tunahitaji kuwekeza kwenye fikra za wananchi, maana ndiko kwenye chanzo cha mabadiliko ya kweli hata katika mazingira yasiyokuwa huru kabisa.
 
CCM kutoheshimu sanduku la kura wameanza Zanzibar 1995 na wamekuwa wakifanya hivyo kwa chaguzi zote zilizofuatia.
Tanganyika yamechelewa kufika kwa sababu upinzani ulikuwa dhaifu. Uchaguzi wa 2015 uliwaonesha kuna uwezekano wa kutolewa madarakani. Kuanzia hapo yote yaliyofanywa Zanzibar yanatendeka Tanganyika.
 
Unawatakia nini vilaza hawa, si bora hata hizo form zingechukuliwa na Lulu Diva au Wema maana wao japo hawatachangia chochote lakini watagawa uroda tu kwa wabunge wenzao na kuambukizana kale kagonjwa ketu.
UTI au kisonono/kaswende/gono/klamidia/panguso?
 
Back
Top Bottom