Hivi kabla ya kugunduliwa kwa ma- ‘speaker’ makubwa yenye mshindo, makanisa ya kilokole yalijiendeshaje?

Wewe hutaki injili ihubiriwe kwa mataifa..uko tayari kuskiliza mziki wa baa..siku nzima ila ibada na mafundisho hutaki..itakua na pepo wewe sio bure.

Tubu na uende ukaombewe

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na wale wa usiku wasaa 10 wanao ita amukaaa amukaaa swalaaa swalaaa kumekuchaaaa kumekuchaàaa,walikuwa nafanyaje kabla ya hivyo vipaza sauti!
Tena hawa huwa wana vitisho muda mwingine,unakuta wanaitana kwa kutishanaaa
 
Mimi nadhani ifikie wakati nyumba zote za ibada ziache kutumia vipaza sauti vyao nyakati za usiku. Na badala yake ziendeshwe ibada zisizo tumia hivyo vipaza sauti ili watu waishio jirani na hizo nyumba za ibada kupata utuliu wa kutosha baada ya miahanhaiko ya kutwa nzima.

Yaani hapa namaanisha hayo makanisa ya kilokole, lakini pia zile nyumba za ibada za wale ndugu zetu wa upande wa pili. Tusisikie visingizio vya kufukuza mapepo usiku, au kuamshana sijui kuswal!
Maana sala/swala kwa upande mmoja, zinaweza kutafsiriwa kama kelele kwa upande mwingine!

Na kuhusu baa na kumbi za starehe, nazo zifunge vifaa maalum vya kuzuia sauti kutoka nje na kukera wasio husika.
 
Wewe hutaki injili ihubiriwe kwa mataifa..uko tayari kuskiliza mziki wa baa..siku nzima ila ibada na mafundisho hutaki..itakua na pepo wewe sio bure.

Tubu na uende ukaombewe

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
Mataifa ni akina nani?
Maeneo yetu yamejaa waumini wa madhehebu mengine tofauti na pentekosti,kwanini wasiheshimiwe imani zao?
 
Nikuulize swali dogo tuu

We ushawahi kuona wapi anoamka alfajiri akakimbiwa na basi

kila mtu ana dini yake afuate mafundisho ya dini yake
 
Dawa huwa ni ndogo tu, nunua mispika na wewe hata mispika mwili tu na mbase moja, au kodi mziki tu si huwa ni 50 elfu [emoji28][emoji28][emoji28]


Sasa kuna muda huwa wanayazima na kuanza kuanza maombi.....

Sasa we ndo washa wakwako yaani [emoji1787] afu una piga ule wimbo wa wozu wa ahh wapi......


Yaani Ukifanya hivyo wiki tu wataelewa somo [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 

Acha uongo mkuu saa kumi na moja huwa husikii kitu?
 
Yaani walikuwa wanaendeshaje endeshaje shughuli zao za ibada?

Kwamba wanaemuabudu alianza kupoteza uwezo wake wa kusikia au ilianzaje anzaje hii hali?

walokole wamekuja juzi juzi miaka ya 90
 
Kuna mchungaji mwingine anaweka mziki wa injili halafu anaenda kulala maana unakuta anaishi mtaa wa mwingine. Sasa mtajuwa wenyewe mlio karibu na kanisa lake.😁😁 yeye anapiga usingizi Mzuri kabisa huko kwake.
 
Haya mambo ya makanisa kupiga mziki nilikua sijawai kuona kwetu kuna msikiti na kanisa la wakatoliki, kwa wakatoliki utakachosikia ni kengele tu na waislamu utakachosikia ni adhana tu kwaiy haikuwa kero kabisa,
Lakini nlivofika mkoa flani nlikuta haya makanisa ya kupiga mziki ule mzito kabisa yan mziki mkubwa tena usiku ila nashukuru mimi huwa nikiamua kulala nalala sehemu yoyote tena bila shida kwaiy ata huw sihangaiki kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…