Hivi kama vijana wanaambiwa wafanye kazi yoyote kwanini wanaenda chuo?

Hivi kama vijana wanaambiwa wafanye kazi yoyote kwanini wanaenda chuo?

Liverpool_Jr

JF-Expert Member
Joined
Sep 7, 2019
Posts
1,220
Reaction score
1,415
Ni siku nyengine tuseme asante Mungu kwa kutuamsha tena.

Naomba niende kwenye mada.

Leo alfajiri nimepigiwa simu na mshakaji wangu wa kipindi Fulani hivi tuliendana sanaa ila ndio harakati za maisha zilitutenga.

Yeye kwasasa ni muuza mayai na alisoma engineering. Jamaa anasema biashara inamuendea poa sanaa maana anauza mayai mpaka ofisi kubwaa posta (DSM).

Alivyokata simu nikabaki najiuliza "Kama ishu ni kuuza mayai, alienda kusoma Geology, kumeza ma physics na ma science ya nini?""

Muhasibu analima hoho...
IT kajiajiri kwenye batiki...
Bachelor ya Education ipo sokoni inauza machungwa..!!!

Hivi kweli HAYA NDIO MATUMIZI SAHIHI YA TAALUMA YETU?

Kuna mwanauchumi mmoja (jina nimelisahau) alishawahi sema "" There are two types of unemployment; 1. Doing nothing while you have power and skills. 2. Doing different thing from what you have learnt"

Kwa mwanauchumi Huyu alimaanisha...
Mwenye degree ya utumishi
1. Akikaa tu kijiweni hiyo ni unemployment.
2. Tukimkuta anafuga nguruwe nayo ni unemployment.
Were are the Human resource management skills in ufugaji wa nguruwe??

Sasa kama jamii na wale wenye ajira wanawaambia vijana "fanyeni kazi yoyote..!"" Kuna haja kweli ya kwenda chuo kuchukua skills halafu tuje mtaani kufanya kazi yoyote?

Nimesoma PCM naenda UD kuchukua Bachelor ya Engineering then naishia kulima bamia...

Hivi ile ada niliyolipa UD kama ningelimia bamia yoote nikiwa na PCM yangu si baada ya miaka 4 ambayo nimeipotezea UD si ningekua na export kabisa..!!!

Halafu cha ajabu asilimia kubwaa wanaowaambia vijana KAJIAJIRINI wao WAMEAJIRIWA na hawafikirii kabisa kuacha kazi.

Mwanasiasa anasisima jukwaani "Vijana jiajirini" kasahau akitoka pale analipwa kwa kodi za wananchi kwasababu ni kiongozi mwanasiasa wa nchi..!!!

Hivi jiulize wewe unaesoma hii post unasema kila siku "vijana jiajirini" bila hiyo kazi uliyo nayo sasa "UNGEWEZA KUJIAJIRI KWELI?"""

VIJANA JIAJIRINI KWENYE LOLOTE
KIJANA FANYA KAZI YOYOTE.
WHAT IS THIS?

Kwasababu sikuenda chuo kusoma chochote nilichagua cha kusoma ili kinitoe maishani ila nikirudi mtaani naambiwa Fanya LOLOTE.

Sasa kama maisha ni chochote basi vyuo vingekuwa vinatufundisha chochote.
 
Serikali iweke somo la LIFESKILLS liwe compulsory kwa kila mtu anayepita chuo kwa kipindi chote anachokua chuo ili waweze kujifunza

Focus and Self-Control. Children need this skill to achieve goals

Perspective Taking

Communicating

Making Connections

Critical Thinking.

Taking on Challenges.

Self-Directed, Engaged Learning.

+Money savings
+Time management
+Entrepreneurial skills
+selling

Pamoja na mtu kuwa na profession yake ili aweze kuwa na plan B ni lazima awe na ujuzi huo ambao wengi wanaukosa.
 
Ndo ujue kusoma ni kupanua mawazo tu na si kupata pesa,tambua ya kwamba kazi si lazima iendane na ulichosoma,wanaofanya kazi inayoendana na elimu yao ni wachache na hazipo office za kuajilii wote hao,serikali na nchi zote duniani watu wamesoma lakini wanaendesha mambo yao mengine kabisa,na haipi serikali yoyote itakayo ingilia mamlaka ya MUNGU aliyo mpa mwanadamu kua kwa jasho la uso wake atakula,then ije serikali ikulishe au ikuoe kirahisi eti kwa sababu mlisoma,ondoeni fikra mfu za kua ulisoma unapaswa kuishi vzr,waingereza mliwasikiliza sana na hii elimu iliyo jaa misingi ya kigeni na sasa mnahangaika huku mkiwa mmepoteza pesa na kupewa karatasi na fikra za kujiita boss.
 
yani umeandika pumba pumba
 
Maisha mtaani ni magumu vijana sio kwamba wanapenda kufanya hivyo sasa utafanyaje?? Kazi uliosomea huna na pesa huna?
 
Hakuna shida,tumia akili unayoiamini tuone inakusaidiaje..ungekua na akili kulalamika kusingekuwepo maana mwenye akili anasonga mbele na maisha yake hayamtegemei mtu wala serikali
yani umeandika pumba pumba
 
Utasikia:-

- Wasomi wanafeli maishani kwasababu wanachagua kazi

- Kazi ni kazi, vijana msichague kazi

- Au utasikia Hawa vijana wa sikuhizi hawapendi kazi

Ukimkuta Kigwangala hapo sasa, anasema vijana msitegemee kuajiriwa, jiajirini wenyewe, wakati yeye ameajiriwa na anachunga ajira yake kama roho.

Kifupi ni kuwa Wasomi wanatafuta namna ya kujiongeza kwasababu hali ni ngumu na Ajira hazipo.
 
Ndo ujue kusoma ni kupanua mawazo tu na si kupata pesa,tambua ya kwamba kazi si lazima iendane na ulichosoma,wanaofanya kazi inayoendana na elimu yao ni wachache na hazipo office za kuajilii wote hao,serikali na nchi zote duniani watu wamesoma lakini wanaendesha mambo yao mengine kabisa,na haipi serikali yoyote itakayo ingilia mamlaka ya MUNGU aliyo mpa mwanadamu kua kwa jasho la uso wake atakula,then ije serikali ikulishe au ikuoe kirahisi eti kwa sababu mlisoma,ondoeni fikra mfu za kua ulisoma unapaswa kuishi vzr,waingereza mliwasikiliza sana na hii elimu iliyo jaa misingi ya kigeni na sasa mnahangaika huku mkiwa mmepoteza pesa na kupewa karatasi na fikra za kujiita boss.
Ishu ni kwamba, basi elimu inayotolewa iendane na kujiajiri. Kama najiajir kufunga nguruwe basi nifundishwe kufuga kitaalamu, kama biashara basi shule yawepo masomo ya biashara ili nilitoka inisaidie sio nisomee kufundisha kingereza halafu nikafuge ng'ombe maana ake nitahitaji elimu nyingine ya ufugaji ile ya elimu ya kwanza ni useless.
 
Sasa hiyo si akili yako wewe unamlaumj nani?wewe na wazazi wako ndo mnaochagua usome nini,sasa unachaguliwa na mwingine au unalazimishwa? Hv waTanzania mna shida gani kichwani? Toka unasoma wewe na washauli wako hasa wazazi ndo wanakuchagulia na wewe unakubali,sasa shida na lawama ni kwa nani

Una akili fupi Sana
 
hoja zako za kitotoooo
 
Hakuna shida,tumia akili unayoiamini tuone inakusaidiaje..ungekua na akili kulalamika kusingekuwepo maana mwenye akili anasonga mbele na maisha yake hayamtegemei mtu wala serikali
Mkuu jifunze angalau matumizi sahihi ya alama za uandishi.

Wapi zikae na kwanini

Then wewe unajinasibu ulienda shule while hujui hata kuandika
 
Miaka ya nyuma watu walikuwa wakisoma na kupata ajira moja kwa moja, sidhani kama kuna aliyeona kusoma ni kupoteza muda kwa wakati huo.

Lakini hivi sasa mambo yamebadilika unaweza ukamaliza kusoma na usipate ajira, lakini pia sidhani kama kuna haja ya kumlaumu aliyekosa ajira baada ya kusomea kitu fulani na kumuona alikuwa akipoteza muda.

Kwa sababu kusomea taaluma fulani sio kujifunga, kuwa hunajingine la kufanya ila ulilosomea tu.

Hivyo watu tupohuru kupambana na maisha kivyovyote, sawasawa kama ulisoma hadi elimu ya juu au uliishia kati au hukubahatika kusoma kabisa.
 
VIJANA JIAJIRINI KWENYE LOLOTE
KIJANA FANYA KAZI YOYOTE.
WHAT IS THIS?
Hii ndiyo hali halisi, na niDo ukweli,
kuna Mheshimiwa Mbunge fulani aliwahi kulisemea bungeni suala hili la Elimu ya Tanzania kuwa ni Kitanzi cha misha na siao ufunguo wa maisha kama ilivyo zoeleka.
Degree ,zimekuwa majanga Tanzania.
 
Back
Top Bottom