Ngoheranga
Member
- Oct 13, 2012
- 29
- 35
Labda suala la chanjo limetufanya wengine kutaka kumwelewa zaidi Gwajima. Kwangu binafsi nimeona ni mtu anaependa kusikika, kuonekana wa tofauti, mjuvi na hivyo yuko tayari abishane hata na dunia nzima ili mradi afanikishe "agenda" yake. Siamini kwamba hapa "agenda" yake ni madhara yatakayoletwa na chanjo. Hivi hatuoni kwamba ile kauli ya kuwa "tangu (fulani) afariki mambo yanaenda ovyo" ina ujumbe mkubwa kuliko hata hilo suala la chanjo yenyewe? Nikitafakari kwa kina naiona chanjo ikitumika kama kivuli tu. Tafakarini, "linalojamba ni tumbo, matako ni spika tu".