Kabla ya Roma ..wagiriki pia walitawala Europe?Sawa??
Ustaarabu wa miji ya Ulaya ulianzishwa na jamii ya Waminoasi wa Zama za Shaba wa Krete na Ugiriki wa Mycenaea, ambao uliisha karibu karne ya 11 BC wakati Ugiriki ilipoingia Enzi za Kigiriki ya nyakati za giza (dark ages).
Kutokana na historia, kabla ya Himaya ya Kirumi, maeneo hayo yalitawaliwa na Waetruria (Etruscans), ambayo ilikuwa jamii ya watu wa hali ya juu na matata kwa wakati huo. Waetruria waliishi kaskazini ya mji wa Roma, huko Toscany.
Baada ya mwaka 650 BC, Waetruria walikuwa wanatawala Italia na kupanuka hadi kaskazini ya kati ya Italia. Kimsingi, Waetruria walitawala Italia, wakifanya biashara na tamaduni nyingine zilizositawi kama vile Ugiriki na Mashariki ya Karibu.
Kwa hivyo basi, himaya zote zilikuwepo wakati huo. Na Himaya ya Ugiriki ilikuja kuangushwa na Alexander the Great, mfalme wa Himaya ya Kirumi ya kale, iliyokuwa inaanza kuimarika katika nyanja zote za maendeleo.
Historia inaonesha kuwa Warumi walifikiri kuwa Wagiriki walikuwa kama watoto kwa kuwa inaaminika walikuwa wakigombana daima, waongo na wasioshirikiana.
Himaya ya Kirumi ndiyo inasemekana kudumu zaidi katika historia. Tarehe rasmi ya kuanza kwa himaya hii bado ni mada ya mjadala, lakini wanahistoria wengi wanakubali kuwa ilianzishwa mwaka 27 BC, wakati mwanasiasa Mroma Octavian alipoipindua Jamhuri ya Kirumi na kujiita Mfalme Augusto