Kwanza lazima ujue mafundisho Yote ya Uisilamu yanapatikana katika Qur'an na Hadithi za mtume Muhammad (saw), hivyo ili waisilamu waungane ni lazima waunganishwe chini ya Imam Mahd (kiongozi anayeongozwa ) na sio chini ya Empire yoyote, hakuna kitu kama hicho kwamba Empire ndiyo itawaleta pamoja waisilamu, kama unaoushahidi kutoka katika hizo Sources mbili yaani Qur'an na Hadithi lete hapa. Imam Mahd ndiye Muanzilishi mtukufu wa Jumuiyya ya waislamu wa Ahmadiyya.
Umesema kweli kwamba dhehebu la Sunni wanawaita Mashia Makafiri na Mashia hivyo hivyo huwaita Masunni makafiri, Answar sunna pia huwaita Mashia makafiri na hivyohivyo mashia huwaita Answar makafiri ilmuradi wote wanaitana makafiri, lakini jifunze jambo hili; wanapotokea Ahmadiyya mbele ya hayo madhehebu mengine hayo madhehebu huungana na huweka tofauti zao pembeni na kuwa kitu kimoja dhidi ya Ahmadiyya, mfano wake ni huu Simba na Swala ni maadui lakini ukiwaweka katika chumba kimoja na ukawasha moto hapo uadui wao huisha na kuanza kupambana na moto kwanza, hapo Ahmadiyya ni kama moto na hayo madhehebu mengine ni kama simba na swala, hapo ndipo ile hadithi ya mtume (saw) inapofanya kazi pale aliposema kwamba; "Umati wake utagawanyika makundi 73 yote yataingia motoni isipokuwa kundi moja".
Umesema kweli kwamba waisilamu wa Waahmadiyya ni watu wa amani lakini hujasema kweli unaposema kwamba waisilamu -Waahmadiyya huswali kanisani, karibu kila nchi duniani kuna Waahmadiyya na kuna Misikiti ya Ahmadiyya imejengwa sasa inakuaje unadanganya kwamba Waahmadiyya huswali kanisani??.
Of all religions sects, Ahmadiyya sect is in Islam is the fastest growing sect of all sects , Chukua madhehebu ya dini zote duniani Ahmadiyya ndiyo dhehebu linalokuwa kwa kasi kubwa kupita madhehebu ya dini zote na hii ni moja ya sababu ya Ahmadiyya kuchukiwa na madhebu mengine ya Waisilamu, licha ya juhudi za hali na mali zinazofanywa na hao waisilamu wengine kuzuia Jumuiyya ya Waisilamu wa Ahmadiyya lakini wao wenyewe wanakiri; Ahmadiyya is unstopable.