Hivi katika maisha yako umewahi kuzika ndg yako asiye na kichwa ?

Hivi katika maisha yako umewahi kuzika ndg yako asiye na kichwa ?

Nikifa MkeWangu Asiolewe

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2024
Posts
12,463
Reaction score
27,556
Ni hii ya dogo aliyeuawa kikatili na kukutwa mtoni akiwa hana kichwa. Isikie tu maana si kawaida.

Mimi hadi hapa nimewahi sikia ni kijijini kwetu Kaya kama 6 kutoka kwetu bibi alikatwa katwa mapanga kwa imani zetu Kanda ya ziwa na kisha kichwa chake wakaenda nacho hao wakataji.

Hatukwenda kwenye tukio maana tulikuwa watoto bado.

Hii tena imetokea asee sio poa.
 
Ndo maana mimi sipendi ugomvi na watu
Kuna watu ni makatili kitu kidogo tu anakuharibia maisha.
Kuna jamaa miaka ya nyuma tulikua kwenye banda la mpira mechi ya simba na yanga , yanga wakafungwa wala hakuna ugomvi ni utani utani tu ,shabiki mmoja wa yanga akachomoa kisu akamdunga aliyekua anawatania yanga kwenye shingo, pasina hata ugomvi, kuna watu zimefyatuka unaweza kumbana nao tu
 
Kuna jamaa miaka ya nyuma tulikua kwenye banda la mpira mechi ya simba na yanga , yanga wakafungwa wala hakuna ugomvi ni utani utani tu ,shabiki mmoja wa yanga akachomoa kisu akamdunga aliyekua anawatania yanga kwenye shingo, pasina hata ugonjwa kuna watu zimefyatuka unaweza kumbana nao tu
Kuna watu ni makatili, ukishaona mtu anapenda visasi, hana huruma kaa nae mbali
 
Video ya mama yake akikukumbatia jeneza na kuwafukuza watu wanaotaka kumtoa iliniumiza sana. Nikakumbuka maneno ya mama

"Uchungu wa mtoto kumzika mzazi ni mdogo ukilinganisha na mzazi kumzika mtoto"

Halafu on top of that, mtoto wako atendewe vile.. Kuna maumivu hayamithiliki na Mungu aniepushe nayo 🙏🏽
 
Visasi na mengine mengine tata ndio hupelekea haya mambo kutokea kuna dogo alihamia mtaani kwetu akawa anajihusisha na ufundi viatu mpaka akawa amezoeleka mtaani hiyo siku asubuhi mwili wake ukakutwa umetenganishwa na kichwa alafu wakaenda kumlaza katikati ya reli. Kwamba treni ya asubuhi ikipita imsagesage nadhani ili kupoteza ushahidi sasa cha kushangaza zaidi ujue damu ya mtu ilivyo nzito siku hiyo treni wala haikupita. Asubuhi watu wanaenda makazini wanaona mwili umetupwa hauna kichwa kuja kuangalia mbele zaidi ndio kukiona kichwa na kumtambua marehemu. Haya mambo yanasikitisha stori za mtaani nikasikia dogo aliwahi korofishana na wakubwa "mangori" kama na yeye alikuwa punda wa ngori hatujui. Ndio sababu ya yeye kuhamia Dar kumbe miaka yote mangori walikuwa wanamtafuta. Ikawa hivyo so sad haya mambo sio poa kabisa
 
Kuna watu ni makatili, ukishaona mtu anapenda visasi, hana huruma kaa nae mbali
Washashiii a.k.a wakurya ogopa sana hao jamaa.

Ukikutana na mtu moral zake zime under go moral erosion... Ni Bora ukutane na Simba alie Shiba porini atakuacha uende ZAKOOO.

Kuna watu ni wanyama sana katili hatarii Bora ukutane na mnyama poriii
 
Ndo maana mimi sipendi ugomvi na watu
Kuna watu ni makatili kitu kidogo tu anakuharibia maisha.
Hii dunia iache tu kama ilivyo kuna matukio ya kinyama unabaki kushangaa ...kuna familia moja kahama huko kijijini walibakwa kisha wakakatwa mapanga hayakuiba wala nini.
 
Back
Top Bottom